Je, 'Folic acid' ni ya lazima kwa kila mjamzito? Huku vijijini hawapewi

Folic acid is a pregnancy superhero! Taking a prenatal vitamin with the recommended 400 micrograms (mcg) of folic acid before and during pregnancy can help prevent birth defects of your baby's brain and spinal cord. Take it every day and go ahead and have a bowl of fortified cereal, too.Jun. 12, 2020

Cheers mkuu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ni lazima atumie aiseee musifanye utania. Unaweza kuuchukia uzazi. Mtoto akizaliwa na kasolo, radha ya kupata mtoto inapotea kabisa.
 
Ni muhimu sana kutumia. Pia ale vyakula vinavyochochea wingi wa damu. Kuna vidonge pia hua vina folic na iron mkipata hivyo pia ni better
 
Aende akanunue duka la madawa.

FeFo
anunue vip wakat tayar serikal ni lazima mjamzito apewe tena bure. Mim ni shahid lazima wanakupa na kadi unatiki.
serikal inatoa hizo tena ni bure na sasa huduma zimeboreshwa sana kila kitu bure.
wasikupotoshe labda kama huna mimba.ila hakuna clinic hawatoi hizo.tena wanakupa ya mwezi mzima vidobge 60.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hajapewa folic wala fefo. Hajapewa kidonge chochote zaidi ya chanjo moja tu TT aliyodungwa.

Na kipimo cha wingi wa damu wajawazito wanaambiwa wakapime kwenye dispensary private iliyoko pale jirani, TSH 5,000!
 
Kwa kuongezea tu km unataka wingi wa damu kunywa juice ya maua ya rozella, km atatumia hivyo vidonge ameze kwa kuruka siku mojamoja (nlimsikia mtaalamu wa hayo mambo juzi Itv akisema utafiti umeonyesha ufanisi wake ni mkubwa kuliko kumezwa kila siku).
 
Vidoge 10 ni buku 5 japokua vinatakiwa 30 hiyo 5alf ni hapa kigambon,sijui kwenu huko .tatizo lililopo kunamuda elimu ya uzazi,pimen kwanza kabla hamjabokoana.mmebokoana unakuja hapa na malalamiko.kijinin hivovitu haviko mlitakiw mkapime hospitali za rufaa
 
Kwanza jifunze kuandika kwa ufasaha ili msomaji akuelewe. Acha uandishi wa darasa la pili.

Pili, mie sijaja hapa kulalamika. Lengo la uzi wangu ni kutaka kujua endapo Folic acid ni za LAZIMA kwa kila mjamzito, ama siyo lazima. Maana scenarios ni tofauti kwa eneo na eneo, kwa mtu na mtu. Zipo sehemu hospitals wanaprovide hizo dawa, lakini maeneo mengine hawapewi. Kuna akina mama waliotumia hizo dawa, baadhi wengine hawajawahi kutumia bila matatizo yoyote.

So uzi huu ni kutaka kufahamu, is folic acid compulsory or optional for pregnancy?

Ujifunze kusoma na ujifunze kuelewa ulichosoma.

Unajiita kina kirefu ... ni kina kirefu cha upunguani ama ujuha?

Elimu ya uzazi imekuaje? Unaishi jijini Dar halafu bado unaandika kishamba hivyo! Ama upo Kigamboni ya Geza Ulole kwa walima minazi?

Punguani wa head!!
 
Kwa kuongezea tu km unataka wingi wa damu kunywa juice ya maua ya rozella, km atatumia hivyo vidonge ameze kwa kuruka siku mojamoja (nlimsikia mtaalamu wa hayo mambo juzi Itv akisema utafiti umeonyesha ufanisi wake ni mkubwa kuliko kumezwa kila siku).

Thanks mkuu Darren2019 . Leo leo anaanza kuzitumia, itabidi tu akanunue pharmacy. Ni mimba ya week 8 now.

Hilo la kuruka siku moja moja umenipa elimu mpya. Ubarikiwe. Thanks
 
Thanks mkuu Darren2019 . Leo leo anaanza kuzitumia, itabidi tu akanunue pharmacy. Ni mimba ya week 8 now.

Hilo la kuruka siku moja moja umenipa elimu mpya. Ubarikiwe. Thanks
Ukipata muda pia ingia youtube search " umuhimu wa wanawake kuhudhuria kliniki meza huru itv" anzia dakika ya 18 wamezungumzia hizo folic acid.
Screenshot_20210301-112239_YouTube.jpg
 
Ni ujauzito wake wa kwanza. Ameenda clinic yake ya kwanza at government hospital (kituo cha afya) huku mkoani. Ujauzito week ya 8.

Wingi wa damu (HB)...
Muongozo unata mama atumia FEFO (ambayo ina folic acid na iron) toka pale anapotaka kupata ujauzi hadi kujifungua... hii itamsaidia mtt alye tumboni kupunguza risk za abnormalities km vile mgongo wazi lkn pia itamsaidia mama ongezeko la damu
 
Folic acid sio tu kupewa wakat wa ujauzito

Bali zinatakiwa kutolewa miezi mitatu kabla ya mama kubeba mimba...ila kibongo bongo kwakua mimba mnasema ni bahati mbaya sikujua ndo sababu zinatolewa mtu tayari ni mjamzito.

Lkn kwa wanandoa wanaoitaj kupata mtoto mwenye Afya zaidi, lazima Mwanamke azitumie miez mitatu kabla ya Kua mjamzito.

Folic acid zimesaidia sana kuepusha abnormalities kadhaa wa kadhaa ambazo mtoto angezaliwa nazo

Mfano , Mtoto kuzaliwa na Neural tube defect ( Spina bifida) yaan mgongo wazi ,unakuta mtoto ana tundu linaonekana, auhana tundu lkn uti wa mgongo umetengeza kama Lifundo au Hana lifundo lkn ukimkagua mtoto kuanzia mwanzo wa uti wa mgongo mpaka mwisho kuna mhali kuna Gap yaan Pingil ya uti wa mgongo haipo.

------Kwa Tatizo hili tu la NTD Linaeza pelekea mtoto pia kupata Congenital Hydrocephalus ( Kichwa kujaa maji).

Ukumbuke, Uti wa mgongo unajitengeneza na kukamilika nakujifunga vzur ndani ya wiki kadhaa tangu apate ujauzito.

Kwaivo kama Atakua hajaanza izo Folic, alafu uti wa mgongo ukawa hujajifunga vzur ndan ya hizo wiki, huyo mama ata atumie Folic vipi hazitasaidia mtoto.

Faida nyingine ya Folic kwa mjamzito ni kumsaidia mama kuongeza damu , kwaajili ya kutengeza Akiba kukidhi damu atakayoipoteza mama wakat wa kujifungua,lkn pia Damu ya kutosha kwa mama ndio inasaidia pia mtoto kupata Nutrients na Oxygen yakutosha.

Kwa bahat mbaya kwa sasa Tunahali mbaya, ivo Usipende vya bure.

Wewe kamnunulie dukani

Folic Acid anywe 400mcg kila siku ...nadhan kwa maduka wanauza kidonge kimoja shilingi 100.
asante kwa somo ntaanza kunywa
 
Back
Top Bottom