Jamani, tuache masihala na tuelezane ukweli, pamoja na kero za posho na uongo unaoendelea wa tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele, Dowans wamelipwa? au ndio maana TANESCO wanapandisha gharama za umeme? mambo haya tusiache kuyajadili pia!
Nina mtu wangu wa ndani sana yupo Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali (Accountant General -AG) aliniambia last week kuwa Dowans walishalipwa. Na akanidokeza kwamba malipo ya Dowans ni sehemu ya chanzo cha ukata serikali hivi sasa!
Kama kweli Dwn wameshalipwa bunge lituambie kwamba hiyo bajet ya kuilipa dwn ilipitishwa lini na ilipitishwaje bila bunge kulitolea tamko au kuiwekea mikono ya baraka. Tunahitaji transpance katika hili na tuache mizengwe!
Kama kweli Dowans wamelipwa basi watz wote including wabunge na wanaharakati wote ni hovyo, iweje wabunge wakae kimya wakati nchi inakuwa exploited? iweje wanaharakati nao tuwe kama wanasiasa? topic inadumu kwa msimu tu na baada ya hapo hatufuatilii na kuishinikiza serikali kuamua in favor of the poor Tanzanians?iweje tupotezwe na siasa na kusahau mambo muhimu? kama ndivyo nina mashaka na uanaharakati wetu!!!!!Nina mtu wangu wa ndani sana yupo Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali (Accountant General -AG) aliniambia last week kuwa Dowans walishalipwa. Na akanidokeza kwamba malipo ya Dowans ni sehemu ya chanzo cha ukata serikali hivi sasa!
Kama kawaida yetu Watanzania tumeishalisahau hilo!!
Iundwe kamati teule ya Bunge kuchunguza hili!