Je cwt simanjiro inawasaidia walimu wake?

HOJA YANGU

Member
Jul 31, 2011
47
19
Ndugu wapendwa, nimelazimika kuuliza swali hili kwa walimu wa SIMANJIRO baada ya kusikia minong'ono mingi sana ili nisikie walimu wanasemaje. Kilio cha walimu wa wilaya ya Simanjiro ambacho kimekuwa kikipazwa ni kwamba. 1. Katibu wa CWT- Simanjiro hafanyi vikao vya ngazi yeyote kinyume na katiba ya chama. 2. Katibu wa CWT-Simanjiro hatoi taarifa mhimu kwa wanachama wake zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari. 3. Katibu wa CWT-Simanjiro kuwa mkali kwa walimu wanaokuja kuripoti hasa wanapoomba msaada wa kujua haki za mtumishi 4. Katibu wa CWT-Simanjiro kuwa kimya katika harakati za walimu nchi nzima kutangaza mgogoro na serikali ktk kudai maslahi ya walimu. Walimu simanjiro, je hizi hizi ndizo allegations (madai) zenu? Au ni Uzushi?
 
Back
Top Bottom