Bob Dylan
JF-Expert Member
- Dec 28, 2011
- 206
- 216
Wanajamvi habarini, nimekutana na kisanga kutoka kwa dada wa kazi, yeye ni mzaliwa wa Dodoma na alikuja kufanya kazi nyumbani kwangu hapa Chugastan.
Siku moja tumeanika maharage baada ya kuvuna na tukaona kuna dalili za mvua mvua vimanyunyu kwa mbali tukaanza kutapa hofu kwamba mvua inaweza anguka na tukapata hasara.
Dada kuona tunahofu akasema hainashida akaingia jikoni akachukua chumvi akaweka kwenye kisosi akaenda kuweka nje.
Chakushangaza mvua haikunyesha tena pakawa kawaida tu na maharage yetu yakaendelea kukauka.
Sasa swali langu ni hii sayansi aliyoitumia kwakweli sijawahi kuiona na nilibaki nashangaa kweli kweli.
Je hii issue ya chumvi ni kweli inazuia mvua au ni kiini macho tu alitupiga ?