Je, CHADEMA ni Wabinafsi?

Je, CHADEMA ni Wabinafsi?

Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa kisiasa wa CHADEMA nchini na kujiuliza kwamba Je Viongozi wa CHADEMA ni Wabinafsi?
Ni kwa nini wamejikita sana kwenye kuchukua Dola (Uraisi) kwenye Uchaguzi ujao 2015 wakati ni ukweli ulio wazi kwa mtu yoyote anayeelewa mambo yalivyo nchini Tanzania kwamba 2015 ni mapema mno kwa CHADEMA au chama chochote cha Upinzani kushinda Uraisi?

Ni kwa nini wasianzie kujijenga polepole kutoka chini kwenda juu? wana haraka gani? kwani ni ukweli ulio wazi kwamba wanahitaji kama Chaguzi mbili zijazo ili waweze kushinda Uraisi (kama wakibakia na kasi walio nayo sasa hivi) sasa ni kwa nini wasiwekeze zaidi kwa sasa kwenye kushinda kwa mfano Chaguzi za Serikali za Vijiji/Mitaa, Udiwani na mpaka Ubunge na mwishowe kwa mfano kufanikiwa kwanza kuongoza Halmashauri na Miji na kuhakikisha kwamba hizo Halmashauri au Miji wanayoiongoza inakuwa mfano ili wapate kithibitisho/kigezo cha kuwashawishi wananchi kwamba Halmashauri wanazoziongoza zinafanya vizuri kulinganisha na Halmashauri zinazooongozwa na vyama vingine.

Kigezo cha kusema 2015 ni mapema mno kwa mfano ukiangalia tu Chaguzi 2 zilizopita Arumeru na Igunga ingawaje ni kweli kwamba watu wengi wameanza kuchoshwa na baadhi ya Viongozi wa CCM lakini bado chaguzi hizo kwa kiasi fulani zimethibitisha kwamba bado watu wengi sana aidha bado wanaamini kwamba CCM ikipewa nafasi bado inaweza kujirekebisha na kufanya vizuri au bado hawajawaamini Wapinzani kiasi hicho cha kuweza kuwapa ushindi mkubwa sana kwani Arumeru ambako ndio mtu angetegemea labda CCM isiambulie kitu lakini bado waliweza kuchuana na CHADEMA sembuse sehemu nyingine za nchi?

Kwa hali ilivyo sasa hata kama CCM wakimsimamisha Bibi Kidude na wakaungana wote na kuanza kumkampenia hakuna Chama kitakachoishinda huo ni ukweli ulio wazi sasa Ni kwa nini Viongozi wa CHADEMA wamejikita sana kwenye kitu ambacho ni wazi hawawezi kushinda wana haraka gani? kwa nini wasiende pole pole?

Licha ya makaripio hayo, Rais
Kikwete alibainisha kuwa CCM
kinasemwa na watu kuwa
kinakithiri rushwa katika chaguzi
zake hivyo akawataka
wagombea kubadilika kabla ya
kukamatwa na Takukuru.
“Zipo taarifa ingawa
hatujazithibitisha kwamba wapo
baadhi ya wagombea
wanamwaga fedha sijawahi
kuona…
Takukuru wapo wanaendelea na
kazi. Chama chetu kinasemwa
tujipe fursa ya kubadilika,
tusisubiri kukamatwa na kuanza
kuilaumu PCCB.”
...je kuna ubinafsi zaidi ya huu?...
 
Lakini mwisho wa siku kwa mfumo wa Uchaguzi wetu mwenye watu wengi ndio mshindi!

Na sijasema kwamba watu hawaikubali CHADEMA nimesema tu kwamba watu wanaanza kuikubali CHADEMA ila itachukua muda kwa mahesabu yangu kama Chaguzi mbili (2) hivi zijazo kama wakienda na mwendo huu wa sasa bila ya mtu kuwachanganya hapo katikati ili kuweza kuchukua Dola na ndio maana ni muhimu kwao kusahau Uraisi kwa sasa na kuelekeza nguvu zote kwenye Vijiji, Serikali za Mitaa Udiwani na Ubunge kwa mfano wakifanikiwa tu kupata Wabunge na Madiwani wengi zaidi ndio hapo sasa unapoweza kuanza kutabiri kifo cha CCM na hiyo inahitaji miujiza kufanyika ndani ya miaka miwili (2) iliyobaki kabla ya Uchaguzi mkuu 2015!

Hii ni game,mwamuzi mzuri ni dakika tisini,we subiri,kama unaona inaanza kukubalika huo ni mtizamo wako,maana kama utatumia vizuri kumbukumbu utakubali ya kuwa CDM wako sawa tu ku-contest uraisi,wakati hawajawa tayari walikuwa hawakuweka mgombea,pili CDM imepamnda chati kwa ghafla,imepata abrupt publicity baada ya uchaguzi wa 2010,leo hii i takribani miaka 2 tu lakini hata watawala tumewaona wanalalamika huko bungeni kuwa inawanyima usingizi,sasa sijui wewe ni vipi hutaki kuamini kuwa CDM inaweza kuchukua nchi 2015.Nimekushauri kuwa na subira uone M4C inaenda kuanza.
 
Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa kisiasa wa CHADEMA nchini na kujiuliza kwamba Je Viongozi wa CHADEMA ni Wabinafsi?
Ni kwa nini wamejikita sana kwenye kuchukua Dola (Uraisi) kwenye Uchaguzi ujao 2015 wakati ni ukweli ulio wazi kwa mtu yoyote anayeelewa mambo yalivyo nchini Tanzania kwamba 2015 ni mapema mno kwa CHADEMA au chama chochote cha Upinzani kushinda Uraisi?

Ni kwa nini wasianzie kujijenga polepole kutoka chini kwenda juu? wana haraka gani? kwani ni ukweli ulio wazi kwamba wanahitaji kama Chaguzi mbili zijazo ili waweze kushinda Uraisi (kama wakibakia na kasi walio nayo sasa hivi) sasa ni kwa nini wasiwekeze zaidi kwa sasa kwenye kushinda kwa mfano Chaguzi za Serikali za Vijiji/Mitaa, Udiwani na mpaka Ubunge na mwishowe kwa mfano kufanikiwa kwanza kuongoza Halmashauri na Miji na kuhakikisha kwamba hizo Halmashauri au Miji wanayoiongoza inakuwa mfano ili wapate kithibitisho/kigezo cha kuwashawishi wananchi kwamba Halmashauri wanazoziongoza zinafanya vizuri kulinganisha na Halmashauri zinazooongozwa na vyama vingine.

Kigezo cha kusema 2015 ni mapema mno kwa mfano ukiangalia tu Chaguzi 2 zilizopita Arumeru na Igunga ingawaje ni kweli kwamba watu wengi wameanza kuchoshwa na baadhi ya Viongozi wa CCM lakini bado chaguzi hizo kwa kiasi fulani zimethibitisha kwamba bado watu wengi sana aidha bado wanaamini kwamba CCM ikipewa nafasi bado inaweza kujirekebisha na kufanya vizuri au bado hawajawaamini Wapinzani kiasi hicho cha kuweza kuwapa ushindi mkubwa sana kwani Arumeru ambako ndio mtu angetegemea labda CCM isiambulie kitu lakini bado waliweza kuchuana na CHADEMA sembuse sehemu nyingine za nchi?

Kwa hali ilivyo sasa hata kama CCM wakimsimamisha Bibi Kidude na wakaungana wote na kuanza kumkampenia hakuna Chama kitakachoishinda huo ni ukweli ulio wazi sasa Ni kwa nini Viongozi wa CHADEMA wamejikita sana kwenye kitu ambacho ni wazi hawawezi kushinda wana haraka gani? kwa nini wasiende pole pole?

Wewe ni mtanzania kweli?? Utaratibu wa nchi yetu ulivyo ambao umehasisiwa na KATIBA, Raisi ndio mteuzi wa karibu maeneo yote yanayogusa kazi za kila siku za wananchi pamoja na shughuli za kisiasa kwahiyo ili uweze kupenya na kupata hizo nafasi za matawi, vijiji inakuwa ngumu sana unless katiba ibadilishwe. Mfano wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 meneja kampeni wa CCM, Kinana alitoa idadi ya majimbo ambayo CCM imeshindwa hata kabla Tume ya Uchaguzi haijatangaza rasmi na Tume ikapigia mstari matokeo hayo. KWA HIYO TUNAELEWA NGUVU KUBWA INABIDI IELEKEZWE KWENYE HIGH OFFICE MAANA HATA PROCESS ZA UBADILISHAJI WA KATIBA UMECHAKACHULIWA!
 
Kwa hali ilivyo sasa hata kama CCM wakimsimamisha Bibi Kidude na wakaungana wote na kuanza kumkampenia hakuna Chama kitakachoishinda huo ni ukweli ulio wazi

Huo ndio ukweli wenyewe bro.

Mwaka 2015 mungu akitupa uhai tutarejea post yako hii wakati huo uchaguzi umeisha wana Chadema wanatafuta mchawi mara Zitto, mara Shibuda, mara Chadema maandamano ,mara chadema M4C ,mara Josephine. Hakika itakuwa tafrani.
 
Wewe ni mtanzania kweli?? Utaratibu wa nchi yetu ulivyo ambao umehasisiwa na KATIBA, Raisi ndio mteuzi wa karibu maeneo yote yanayogusa kazi za kila siku za wananchi pamoja na shughuli za kisiasa kwahiyo ili uweze kupenya na kupata hizo nafasi za matawi, vijiji inakuwa ngumu sana unless katiba ibadilishwe. Mfano wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 meneja kampeni wa CCM, Kinana alitoa idadi ya majimbo ambayo CCM imeshindwa hata kabla Tume ya Uchaguzi haijatangaza rasmi na Tume ikapigia mstari matokeo hayo. KWA HIYO TUNAELEWA NGUVU KUBWA INABIDI IELEKEZWE KWENYE HIGH OFFICE MAANA HATA PROCESS ZA UBADILISHAJI WA KATIBA UMECHAKACHULIWA!

Hiyo hoja ya katiba mpya kwa sasa haipo tena maana tume inazunguka kukusanya maoni. Na mtu wa Chadema yupo mule ndani kwenye tume ,sasa sijui na yeye mna question credibility yake?

Tafuteni hoja nyingine zenye mashiko, hususan hizi za kuvumbua mbinu za ufisadi huwa zinatoa air time sana kwa Chadema.
 
Mkuu kwa hiyo unasema CCM hata wakimsimamisha Bi Kidude, Chadema hawawezi kushinda...maneno mazito haya.

CCM ipi? Familia BMW, Asilia,kampuni au matumaini ? Unamaanisha ipi Kati ya hizo CCM nne? Na wewe uko ipi Kati ya hizo?
 
Wewe ni mtanzania kweli?? Utaratibu wa nchi yetu ulivyo ambao umehasisiwa na KATIBA, Raisi ndio mteuzi wa karibu maeneo yote yanayogusa kazi za kila siku za wananchi pamoja na shughuli za kisiasa kwahiyo ili uweze kupenya na kupata hizo nafasi za matawi, vijiji inakuwa ngumu sana unless katiba ibadilishwe. Mfano wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 meneja kampeni wa CCM, Kinana alitoa idadi ya majimbo ambayo CCM imeshindwa hata kabla Tume ya Uchaguzi haijatangaza rasmi na Tume ikapigia mstari matokeo hayo. KWA HIYO TUNAELEWA NGUVU KUBWA INABIDI IELEKEZWE KWENYE HIGH OFFICE MAANA HATA PROCESS ZA UBADILISHAJI WA KATIBA UMECHAKACHULIWA!

Na ndio maana nasema ni ngumu sana kwa CHADEMA au Upinzani kuwashinda CCM kwenye Uraisi 2015 wewe mwenyewe umesema jinsi gani walivyokuwa na nguvu na hata hiyo Katiba mpya yenyewe inayotegemewa ni lazima CCM waipitie kwanza na wakiiona inafaa ndio waikubali vinginevyo hawawezi kuikubali kwa hiyo kinachobaki ni kuwalazimisha CCM wakubali kuachia madaraka na utawalamizisha vipi? ndio hapo nasema ni lazima CHADEMA/ Upinzani wajenge Msingi Imara sana chini kwanza kwani huko ndiko nguvu ya CCM iliko, na ndiko wapiga kura wengi waliko ikifika wakati wa Uchaguzi CCM wanawapa Mahindi au tu kuwadanganya na mwishowe wanaipigia kura CCM kwa hiyo ni lazima kazi kubwa ifanyike kuwashawishi hawa watu wa vijijini kuwa kuna maisha pia baada ya CCM bila hivyo hamna kitu!

 
CCM ipi? Familia BMW, Asilia,kampuni au matumaini ? Unamaanisha ipi Kati ya hizo CCM nne? Na wewe uko ipi Kati ya hizo?

CCM ambayo inaoongozwa na Mwenyekiti ambaye ndiye Raisi wa nchi hao wengine wote sijui mtandao au makundi hawana lolote mwisho wa siku Raisi Tanzania ndio kila kitu na ndio maana kutokana na madaraka yake makubwa aliyokuwa nayo anaweza kumfukuza yoyote ktk CCM hakuna wa kumfanya lolote na yoyote atakayetoka na kuanza kushindana na Raisi hawezi kushinda na hilo hao wanamtandao wanalijua na ndio maana hakuna wa kubreak up, Bw. Mkono kapigwa chini na Bw. Kikwete na Raisi kwa Ujeuri kasema ngoja sasa tuone patachimbika vipi kama alivyosema Bw. Mkono!

 

Na ndio maana nasema ni ngumu sana kwa CHADEMA au Upinzani kuwashinda CCM kwenye Uraisi 2015 wewe mwenyewe umesema jinsi gani walivyokuwa na nguvu na hata hiyo Katiba mpya yenyewe inayotegemewa ni lazima CCM waipitie kwanza na wakiiona inafaa ndio waikubali vinginevyo hawawezi kuikubali kwa hiyo kinachobaki ni kuwalazimisha CCM wakubali kuachia madaraka na utawalamizisha vipi? ndio hapo nasema ni lazima CHADEMA/ Upinzani wajenge Msingi Imara sana chini kwanza kwani huko ndiko nguvu ya CCM iliko, na ndiko wapiga kura wengi waliko ikifika wakati wa Uchaguzi CCM wanawapa Mahindi au tu kuwadanganya na mwishowe wanaipigia kura CCM kwa hiyo ni lazima kazi kubwa ifanyike kuwashawishi hawa watu wa vijijini kuwa kuna maisha pia baada ya CCM bila hivyo hamna kitu!


Hoja Yao inanikumbusha hoja za REDET kuwa Vyama vya upinzani waende vijijini, ila Juzi mtaalamu wa Redet yuleyule BAna a kasema kuwa Huu sio wakati muafaka kwa CDM Kwenda vijijini kwani ni wakati aw kutekeleza ilani ya uchaguzi , sasa na wewe unasema CDM waachane na Urais ili Muendelee kutawala ? Hilo Sahau kwani watz Ndio Wenye maamuzi na wameshaamua
 
nafikiri wewe unamatatizo ya kuona mbali.subiri 2015.
 
Back
Top Bottom