Je, CHADEMA ni Wabinafsi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, CHADEMA ni Wabinafsi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kijakazi, Sep 26, 2012.

 1. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa kisiasa wa CHADEMA nchini na kujiuliza kwamba Je Viongozi wa CHADEMA ni Wabinafsi?
  Ni kwa nini wamejikita sana kwenye kuchukua Dola (Uraisi) kwenye Uchaguzi ujao 2015 wakati ni ukweli ulio wazi kwa mtu yoyote anayeelewa mambo yalivyo nchini Tanzania kwamba 2015 ni mapema mno kwa CHADEMA au chama chochote cha Upinzani kushinda Uraisi?

  Ni kwa nini wasianzie kujijenga polepole kutoka chini kwenda juu? wana haraka gani? kwani ni ukweli ulio wazi kwamba wanahitaji kama Chaguzi mbili zijazo ili waweze kushinda Uraisi (kama wakibakia na kasi walio nayo sasa hivi) sasa ni kwa nini wasiwekeze zaidi kwa sasa kwenye kushinda kwa mfano Chaguzi za Serikali za Vijiji/Mitaa, Udiwani na mpaka Ubunge na mwishowe kwa mfano kufanikiwa kwanza kuongoza Halmashauri na Miji na kuhakikisha kwamba hizo Halmashauri au Miji wanayoiongoza inakuwa mfano ili wapate kithibitisho/kigezo cha kuwashawishi wananchi kwamba Halmashauri wanazoziongoza zinafanya vizuri kulinganisha na Halmashauri zinazooongozwa na vyama vingine.

  Kigezo cha kusema 2015 ni mapema mno kwa mfano ukiangalia tu Chaguzi 2 zilizopita Arumeru na Igunga ingawaje ni kweli kwamba watu wengi wameanza kuchoshwa na baadhi ya Viongozi wa CCM lakini bado chaguzi hizo kwa kiasi fulani zimethibitisha kwamba bado watu wengi sana aidha bado wanaamini kwamba CCM ikipewa nafasi bado inaweza kujirekebisha na kufanya vizuri au bado hawajawaamini Wapinzani kiasi hicho cha kuweza kuwapa ushindi mkubwa sana kwani Arumeru ambako ndio mtu angetegemea labda CCM isiambulie kitu lakini bado waliweza kuchuana na CHADEMA sembuse sehemu nyingine za nchi?

  Kwa hali ilivyo sasa hata kama CCM wakimsimamisha Bibi Kidude na wakaungana wote na kuanza kumkampenia hakuna Chama kitakachoishinda huo ni ukweli ulio wazi sasa Ni kwa nini Viongozi wa CHADEMA wamejikita sana kwenye kitu ambacho ni wazi hawawezi kushinda wana haraka gani? kwa nini wasiende pole pole?
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Aisee?
   
 3. MR. ABLE

  MR. ABLE JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,476
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mi naona wewe uko nje ya tanzania na pengine hata habari hazikufikii, we kaa kimya subiri 2015. Kama huoni kwa macho papasa kwa mkono utapata majibu.
   
 4. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Najaribu kutafakuri title na maelezo/mada kuu nikifanikiwa kuviunganisha nitarudi kuchangia.
   
 5. Root

  Root JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,307
  Likes Received: 13,016
  Trophy Points: 280
  chadema ni chama na chama huundwa na watu wa dini,kabila,rangi tofauti so hapa sidhani kama wote ni wabinafsi.
  Muhimu fanya research kuhusu ubinafsi wao then utaelewa
   
 6. e

  emgitty06 Senior Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Teheeeeeh! Mapema mno??? Hapo ndipo utakapowekea (??) elimu ya mbongo. Kwamba kweli kuna haja ya watu kuhitimu? Kama unajifunza kusoma na kuandika kisha unajifunza kutumia kompyuta, ukatumia JF, bado unakuwa huwezi kung'amua mambo tu?
   
 7. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,598
  Likes Received: 2,408
  Trophy Points: 280
  Duh! Kijakazi nakuona hapa nashindwa hata nikuambie nini, hizo chaguzi mbili unazotaka zipite angalau ndio CDM ichukue Nchi kwa speed hii ya CCM nakuhakikishia hii Nchi haitakuwa ya maziwa na asali tena.

  Nimetoka katika vijiji kadhaa vya kimasai kama wiki 3 zilizopita,kila sehemu ni kilio wamasai wanalia ardhi yao imeuzwa kwa waarabu wanajiita OBC wanawinda kiala aina ya mnyama na mdudu unayemjua wewe na serikali kuu imebariki haya pamoja na wanakijiji kupinga ardhi yao isitwaliwe, sasa ndugu yangu unaposema CDM ni wabinafsi cjui CCM tuwaiteje.
   
 8. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  sifongo

  Kwa kuuliza kama ni Wabinafsi nilichomaanisha ni kwamba labda katika Uongozi wa CHADEMA kuna watu wenye Ubinafsi maana yake ni kwamba labda wana nia tu ya kuongoza nchi, na si vinginenvyo, kwa maana sioni jinsi ambavyo katika hali ya kawaida wanaweza kushinda Uraisi 2015.

  Kama ulivyosema umetoka Umasaini na watu wanalia, vilio kila mahali kwa hiyo katika hali ya kawaida ungetegemea kwamba katika Uchaguzi wangepeleka hasira zao na kuiondoa CCM lakini wapi bado pamoja na maovu yote ya CCM na vilio vyao bado CCM inapata kura nyingi sana tu mfano Igunga na Arumeru Mashariki.

  Ndio maana mimi nafikiri pamoja na shida watu walizonazo lakini bado hawaiamini CHADEMA au Upinzani kuwaongoza hivyo kwangu mimi ni bora CHADEMA wangeanzia kwanza huko kwa wanakijiji kwa mfano huko Umasaini ulikokusema na kuhakikisha labda Mwenyekiti wa Kijiji mpaka Diwani ni wa CHADEMA na kama kweli wakiwathibitishia watu katika maeneo wanayoyaongoza kuna mabadiliko watu watawachagua tena kwa nguvu zote lakini kujikita kwenye Uraisi 2015 ni kujidanganya tu hawana uwezo wa kuwashinda CCM there are just too strong kwa sasa hivi!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Muda huu aongoze nani???
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mleta thread anafikiri CDM ilisajiliwa 2009. Nafikiri hili ni tatizo la kufakamia pombe za kienyeji kabla ya kuja hapa jamvin
   
 11. gimmy's

  gimmy's JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 2,362
  Likes Received: 1,145
  Trophy Points: 280
  Naamini nitapata changamoto nyingi sana lakini naamini hili lazma litajitokeza kwa mapana na zaidi ya sasa kama itatokea CDM imeshika dola.

  Sifa za kuajiriwa ktk nchi yetu si uanachama wa CCM bali ni uraia hivyo waajiriwa serikalini wapo kwa vyama vyote hapa Tanzania wakiwemo na kutoka CDM. Tutakubaliana kwamba wizi na ufisadi si lazma uwe waziri hata waajiriwa wa chini pia ni wezi na mafisadi wakubwa.Binafsi nimeshuhudia wana CDM lukuki wakihujumu mali za uma,wala rushwa wazuri tu, nimeshuhudia maraisi vyuoni wa CDM wakifisadi mifuko ya wanafunzi pamoja na mifano mingine mingi tuu inayo tuzunguka mitaani.

  Jiulize wewe ni wa chama gani na je kweli ni muadilifu kiasi gani kwa watanzania?

  wengi wao wanafuja mali za uma kwakisingizio kwamba mbona waziri kaiba!

  Hivyo kinachosumbua hapa ni sehemu ya kula ila CDM hakuna ukweli wowote zaidi ya njaaa zinazowasumbua!
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa hiyo unasema CCM hata wakimsimamisha Bi Kidude, Chadema hawawezi kushinda...maneno mazito haya.
   
 13. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kijakazi,CDM haina mtazamo wa mbali na wala haitatokea mpaka wabadilishe waliopo sasa.Hiki chama kama ni mfano wa kiumbe basi hakina tofauti na akili za kuku.
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hivi bado unaamini CDM ni chama, this a company my dear. Nadhani unajua sifa za kampuni yoyote duniani ni uongozi wa juu tu do unajulikana
   
 15. t

  thatha JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Anaweza kushinda, unajua kwenye siasa kinachoangaliwa na mfumo na siyo maguvu, wakimsimamisha Binti Hamisi anaweza kushinda, CCM wana mfumo unaoleweka wa kuwapata viongozi wao. Hebu angalia kule Mwanza, kajimbo kamoja tu kmpata Meya imekua tabu. Unategemea nini katika kumpata Rais au mawaziri?
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  MBOWE na SLAA ni janga ndani ya CDM, na sijui kwa nini wanachama na viongozi hawataki kulikiri hili.
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280

  JULIUS MALEMA,
  Nakubaliana na wewe ni kweli tumeona kule Mwanza wanataka kutoana roho, mpaka leo bado hawajapata jina la Meya.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Vipi mkuu, ukweli unauma ile mbaya, hawa jamaa mimi wananiboa ile mbaya. Hivi kwa mtindo huo wataacha kuitwa kampuni? manake kampuni ndo uongozi wa juu pekee unajulikana, utasikia mkurugenzi, meneja masoko wakati wawezeshaji wa kampuni ni watu wa chini sana tena vitengo vingi.
   
 19. sembo

  sembo JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 3,350
  Likes Received: 1,202
  Trophy Points: 280
  Hapana, CHADEMA si wabinafsi.
   
 20. MWILI NYUMBA

  MWILI NYUMBA JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kila siku naamini kuwa chama cha upinzani chenye nia ya kuleta maendeleo ya kweli Tanganyika bado sijakiona!! Porojo,vijembe,ubinafsi na uchu wa madaraka ndiyo vyama vyote vimetawaliwa na hivyo vitu. Ooh My poor Tanganyika!!!!
   
Loading...