Je, CHADEMA ni Wabinafsi?

Muhogo wa Jang'ombe nani kakuambia Bi Kidude anataka propaganda chafu? Yeye siku nyingi alishaukwaa urais katika fani ya muziki wa taarabu duniani. Sasa leo wanamagamba mnataka kumnadi na kuutumia umaarufu wa Bi Kidude kusafisha nyota yenu?

Kweli mumechoka sana kama Bi Kidude alivyochoka kwa uzee,faraja yake ikiwa sigara na bia baada ya serikali yake kutoutambua na kuuthamini mchango wake katika fani ya muziki wa taarabu kwa muda wote wa miaka 50 ya uhuru.
 
Najua ni vigumu kwa wana ccm kuamini kama kweli hii nchi inaenda kwenye mabadiliko ya kiutawala, hata hivyo mabadiliko hayawezi yakasubiri hisia zenu ziwe tayari, itabidi hisia zenu zikubali pale mabadiliko yatakapokuwa yameshafanyika.

Kwa hiyo kaeni mkijua, lazima mabadiliko yafanyike, halafu nyinyi ndo mtalazimika kuyakubali maana ndo yatakuwa yameshatokea, hamtakuwa tena na hiari ya kuchagua kama mkubali au msikubali.

CCM, pigeni porojo tuu, ila mjue watanzania wamechoka na utawala wenu mbovu, na katika hali kama hii wanaweza kuchagua hata jiwe kuliko ccm. Kama huamini, jikumbushe nini kiliwapata kule pemba.
 
Watu wenye mawazo mgando kama hawa wanamatatizo sana, wanatoa maada zisizo na msingi ili mpoteze muda kwenye kuzi jadili.

Viongozi wao walisema huuni upepo utapita tu lakini wameshaanza kutapatapa,waliviita vyama vya msimiu lakini msimu wake haupiti tu.

Hawa watawala inawapasa wakaee pembeni wawaachie na wengine sasa kwani miaka 50 waliokaa madarakani inawatosha by nw inaonekana uwezo wao umefika mwisho cz hawana jipya, ahadi lukuki hakuna wanazotekeleza,wanasema serikali haina pesa bt safari za rais ziko palepale.
 
Sio kwamba mimi naichukia CHADEMA au Upinzani bali ni jinsi nikiangalia mfumo wetu ulivyo na jamii yetu ya Kitanzania kwa ujumla tusiongelee vitu kutoka hewani tuchukue Mifano hai kama ni kweli unavyosema kwamba Watz wameichoka CCM hivyo ni kwa nini Chaguzi hizi za juzi tu CCM walishinda au CHADEMA kama walishinda ni kwa shida sana kama uko sahihi kwamba wananchi wameichoka CCM?

Chukulia mfano Dar ambako ndiko wasomi wengi na waelewa wa mambo yanavyokwenda nchini mwetu wanaishi lakini bado inaongozwa na CCM sasa kuchokwa huko unakokuongelea ni kupi? lete mifano hai na sio kutoka hewani!

Tatizo ninaloliona ni kwamba kwa kuwa CHADEMA wanawekeza sana katika kushinda Uraisi na sio kujenga Chama kutoka chini watakaposhindwa kwenye Uchaguzi ujao wa 2015 huo ndio unaweza ukawa mwanzo wa mwisho wa CHADEMA.

Ni Viongozi wengi watakaopoteza matumaini tena hawatakuwa na moyo na mori tena ya kuanza kupambana upya kwa kasi waliokuwa nayo sasa hivi, na kama walikuwa vitani basi wataweka silaha chini na kurudi nyumbani kama tu NCCR ilivyokuwa lakini kama wakiwekeza zaidi kwenye kukijenga Chama sasa hivi tangu chini hata kama ikitokea wameshindwa Uchaguzi bado watakuwa na nguvu huku chini na Chama kuendelea kuwepo.

 
Unachoongea ni kweli CDM ni kama kampuni. Is for profit company.
 
Watu wenye mawazo mgando kama hawa wanamatatizo sana, wanatoa maada zisizo na msingi ili mpoteze muda kwenye kuzi jadili.

Viongozi wao walisema huuni upepo utapita tu lakini wameshaanza kutapatapa,waliviita vyama vya msimiu lakini msimu wake haupiti tu.

Hawa watawala inawapasa wakaee pembeni wawaachie na wengine sasa kwani miaka 50 waliokaa madarakani inawatosha by nw inaonekana uwezo wao umefika mwisho cz hawana jipya, ahadi lukuki hakuna wanazotekeleza,wanasema serikali haina pesa bt safari za rais ziko palepale.

Watu kama nyinyi hasa ndio shida na mzigo mkubwa kwa CHADEMA, kwa maana mtu yoyote anayejaribu kutoa maoni yake hata kama mwisho wa siku ana nia ya kuiboresha hiyo hiyo CHADEMA mnaojifanya kama mnaipenda mnamuona adui, mambo hayaendi hivyo andika vitu na na kuambatanisha na ushaidi kuongea tu kila mtu anaweza, kusema tu CCM imechokwa hoja hiyo haina mshiko kwa maana ushahidi pekee unaoweza kusimama ni kwenye Uchaguzi, na tumeona Chaguzi ndogo mbalimbali zinazofanyika sehemu mbalimbali nchini CHADEMA hata kama wakishinda ni kwa msuli mkubwa sana na sio landslide kama wanavyosema wazungu sasa huko kuchokwa gani unakokuongelea? nipe mfano wa Uchaguzi ambao CHADEMA wamepata landslide ushindi! Dhidi ya hapo ni blah blah tu


 
Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa kisiasa wa CHADEMA nchini na kujiuliza kwamba Je Viongozi wa CHADEMA ni Wabinafsi? Ni kwa nini wamejikita sana kwenye kuchukua Dola (Uraisi) kwenye Uchaguzi ujao 2015 wakati ni ukweli ulio wazi kwa mtu yoyote anayeelewa mambo yalivyo nchini Tanzania kwamba 2015 ni mapema mno kwa CHADEMA au chama chochote cha Upinzani kushinda Uraisi?Ni kwa nini wasianzie kujijenga polepole kutoka chini kwenda juu?......
1. Unapozungumzia CDM ni mapema sana fuatilia Kenya chama kilichoiangusha KANU kilianza lini, kilianzaje

2. Kuhusu kujijenga huoni chama kinavyozidi kuimarika? kwa mfano katika uchaguzi wa Igunga kuna kijiji kimoja polini kabisa kituo kimoja cha Kura CCM walipata kura 1 na CDM 102 huoni kama CDM inakubarika hadi vijijini.

3. Kwa chaguzi za Igunga na Arumeru kwa mawazo yako sio sahihi kabisa, chaguzi hizo ni kipimo tosha kabisa cha anguko la CCM. kwa Igunga CCM walishindwa na kuchakachua matokeo na mungu ametoa haki yake Ubunge wa Kafumu umetenguliwa, Kwa Arumeru CCM walijitahidi kuchakachua lakini na wizi wote huo Kura hazikutosha.

3. Nimesikitika sana ulipotumia jina la Bi Kidude katika siasa za humu JF na mfano ulioutoa si sahihi kiubinadamu huko ni kumdhalilisha Mzee wetu ambaye kwa hivi sasa ni mgonjwa. Namuombea mungu amsaidie apone.
 
Wewe uliyeandika topic hii siajakuelewa nakuona kama unatumika na magamba.Fuatilia siasa za nchi ndipo utakapofahamu kwamba watu wamebadilika. CCM kwa sasa ni chama kinachotegemea dola ili kuweza kuendelea kukaa madarakani.
 
kwa mambo yalivyo sasa hapa nchini, kama CDM ni wabinafsi je ccm tuwaiteje?
 
1. Unapozungumzia CDM ni mapema sana fuatilia Kenya chama kilichoiangusha KANU kilianza lini, kilianzaje 2. Kuhusu kujijenga huoni chama kinavyozidi kuimarika? kwa mfano katika uchaguzi wa Igunga kuna kijiji kimoja polini kabisa kituo kimoja cha Kura CCM walipata kura 1 na CDM 102 huoni kama CDM inakubarika hadi vijijini.3. Kwa chaguzi za Igunga na Arumeru kwa mawazo yako sio sahihi kabisa, chaguzi hizo ni kipimo tosha kabisa cha anguko la CCM. kwa Igunga CCM walishindwa na kuchakachua matokeo na mungu ametoa haki yake Ubunge wa Kafumu umetenguliwa, Kwa Arumeru CCM walijitahidi kuchakachua lakini na wizi wote huo Kura hazikutosha.3. Nimesikitika sana ulipotumia jina la Bi Kidude katika siasa za humu JF na mfano ulioutoa si sahihi kiubinadamu huko ni kumdhalilisha Mzee wetu ambaye kwa hivi sasa ni mgonjwa. Namuombea mungu amsaidie apone.

Kwanza kuhusu Bibi Kidude sikumdhalilisha bali nimetumia mfano wake yeye kama mwana sanaa na mimi namheshimu sana!

Yote uliyoongelea kuhusu CHADEMA kuendelea kufanya vizuri hadi kwenye ngazi ya vijiji nakubaliana na wewe na ni ishara nzuri na ndio maana mimi naona wangewekeza huko zaidi kwanza kwani kazi inayotakiwa kufanywa bado ni kubwa sana ili waweze kushinda Uraisi na sioni jinsi gani wanavyoweza kuifanya hiyo kazi ndani ya miaka 2 iliyobaki mpaka 2015 kwa maana huko kote kwa jinsi CCM walivyoharibu walipaswa wasiambulie (CCM) kitu kama CUF lakini maadam bado wanashinda au kugawana kura karibu sawa na CHADEMA hiyo inaonyesha kwamba pengo bado ni kubwa sana kuweza kuliziba 2015.

Kuhusu uibaji wa kura hilo halina mshiko kwani mwisho anayeshinda ndiye mshindi na anaongoza nchi na huwezi kupinga mahali popote na ndio maana nasema kazi bado ni ngumu sana na 2015 ni karibu sana na ukisema uhasishe watu waingie barabarani hiyo litabackfire kwa maana bado Watz hawako tayari kupigwa risasi kwa ajil ya Chama!

Kuhusu Kenya, Siasa za Kenya ni tofauti sana na za Tanzania, na tuna mifumo tofauti jinsi CCM ilivyojikita vijijini sio kama KANU ilivyokuwa halafu kingine na pengine muhimu kuliko vyote Siasa za Kenya ni za Ukabila na watu Kabila fulani wanampigia kura mtu wa Kabila lao kwa mfano Raila ni Mjaluo kwa hiyo Wajaluo karibu wote bila kuangalia sera watamfwata popote atakapokwenda kama akianzisha Chama watamfwata, na wengine nao hivyo hivyo sijui Wakikuyu n.k.

Lakini Siasa zetu hatuna hayo mambo, labda kidogo Dini kitu ambacho CUF wanataka kuanza kutumia na kama wakifanikiwa ndio unaweza sasa ukalinganisha na Kenya kwamba watu wa Dini fulani wanaungana kwa umoja wao dhidi ya adui fulani ambaye labda wao watamtambua kama CCM au CHADEMA lakini bado hatujafika huko na kilichopo sasa hivi ni kuwashawishi tu wananchi kwamba CCM haiwafai na CHADEMA au Upinzani ndio unawafaa na hiyo sio kazi rahisi!

 
sifongo

Kwa kuuliza kama ni Wabinafsi nilichomaanisha ni kwamba labda katika Uongozi wa CHADEMA kuna watu wenye Ubinafsi maana yake ni kwamba labda wana nia tu ya kuongoza nchi, na si vinginenvyo, kwa maana sioni jinsi ambavyo katika hali ya kawaida wanaweza kushinda Uraisi 2015....!
Watu gani unaosema hawaiamini CDM? napata tabu kuamini kama uko TZ na unapata habari,juzi kauwawa mwandishi unadhani kama watu hawaikubali CDM huko wangelienda kufanya nini?

Si walienda kufungua matawi ya chama? Na kwa akili yako unadhani watu wote kabisa watakuja kuipenda CDM? Au watu wote kabisa wanaipenda CCM?

Na ndio maana huwa kuna itishwa uchaguzi maana watu wanaitikadi tofauti.
Ukiataka kuamini na kujifunza subiri M4C itakapoanza tena wiki kama mbili zijazo
 
Watu gani unaosema hawaiamini CDM? napata tabu kuamini kama uko TZ na unapata habari,juzi kauwawa mwandishi unadhani kama watu hawaikubali CDM huko wangelienda kufanya nini?si walienda kufungua matawi ya chama?na kwa akili yako unadhani watu wote kabisa watakuja kuipenda CDM?au watu wote kabisa wanaipenda CCM? na ndio maana huwa kuna itishwa uchaguzi maana watu wanaitikadi tofauti.
Ukiataka kuamini na kujifunza subiri M4C itakapoanza tena wiki kama mbili zijazo

Lakini mwisho wa siku kwa mfumo wa Uchaguzi wetu mwenye watu wengi ndio mshindi!

Na sijasema kwamba watu hawaikubali CHADEMA nimesema tu kwamba watu wanaanza kuikubali CHADEMA ila itachukua muda kwa mahesabu yangu kama Chaguzi mbili (2) hivi zijazo kama wakienda na mwendo huu wa sasa bila ya mtu kuwachanganya hapo katikati ili kuweza kuchukua Dola na ndio maana ni muhimu kwao kusahau Uraisi kwa sasa na kuelekeza nguvu zote kwenye Vijiji, Serikali za Mitaa Udiwani na Ubunge kwa mfano wakifanikiwa tu kupata Wabunge na Madiwani wengi zaidi ndio hapo sasa unapoweza kuanza kutabiri kifo cha CCM na hiyo inahitaji miujiza kufanyika ndani ya miaka miwili (2) iliyobaki kabla ya Uchaguzi mkuu 2015!

 
Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa kisiasa wa CHADEMA nchini na kujiuliza kwamba Je Viongozi wa CHADEMA ni Wabinafsi?
Ni kwa nini wamejikita sana kwenye kuchukua Dola (Uraisi) kwenye Uchaguzi ujao 2015 wakati ni ukweli ulio wazi kwa mtu yoyote anayeelewa mambo yalivyo nchini Tanzania kwamba 2015 ni mapema mno kwa CHADEMA au chama chochote cha Upinzani kushinda Uraisi?

Ni kwa nini wasianzie kujijenga polepole kutoka chini kwenda juu? wana haraka gani? kwani ni ukweli ulio wazi kwamba wanahitaji kama Chaguzi mbili zijazo ili waweze kushinda Uraisi (kama wakibakia na kasi walio nayo sasa hivi) sasa ni kwa nini wasiwekeze zaidi kwa sasa kwenye kushinda kwa mfano Chaguzi za Serikali za Vijiji/Mitaa, Udiwani na mpaka Ubunge na mwishowe kwa mfano kufanikiwa kwanza kuongoza Halmashauri na Miji na kuhakikisha kwamba hizo Halmashauri au Miji wanayoiongoza inakuwa mfano ili wapate kithibitisho/kigezo cha kuwashawishi wananchi kwamba Halmashauri wanazoziongoza zinafanya vizuri kulinganisha na Halmashauri zinazooongozwa na vyama vingine.

Kigezo cha kusema 2015 ni mapema mno kwa mfano ukiangalia tu Chaguzi 2 zilizopita Arumeru na Igunga ingawaje ni kweli kwamba watu wengi wameanza kuchoshwa na baadhi ya Viongozi wa CCM lakini bado chaguzi hizo kwa kiasi fulani zimethibitisha kwamba bado watu wengi sana aidha bado wanaamini kwamba CCM ikipewa nafasi bado inaweza kujirekebisha na kufanya vizuri au bado hawajawaamini Wapinzani kiasi hicho cha kuweza kuwapa ushindi mkubwa sana kwani Arumeru ambako ndio mtu angetegemea labda CCM isiambulie kitu lakini bado waliweza kuchuana na CHADEMA sembuse sehemu nyingine za nchi?

Kwa hali ilivyo sasa hata kama CCM wakimsimamisha Bibi Kidude na wakaungana wote na kuanza kumkampenia hakuna Chama kitakachoishinda huo ni ukweli ulio wazi sasa Ni kwa nini Viongozi wa CHADEMA wamejikita sana kwenye kitu ambacho ni wazi hawawezi kushinda wana haraka gani? kwa nini wasiende pole pole?


Umeona CCM wanachaguana na kufukuzana kuwa TAYARI na UCHAGUZI wa 2015?

Wale wote wa CCM waliomuunga MKONO ZITTO KABWE watapoteza MADARAKA YAO SASA HIVI

MWAKA 2015 CCM inataka kuwa SAFI na bila MCHAFUKO WA NDANI; Sasa wakati CCM inafanya HIVYO

Kwanini CHADEMA isijiimarishe na kusaka WANACHAMA ? CCM wana stratergy yao na Inafanikiwa

Kwanini CHADEMA wasifanye hivyo - AU UNATAKA wakae kima kama CHAMA CHA CCK ?
 
Back
Top Bottom