Je, CHADEMA inasubiri "Makapi" ya wagombea ubunge kutoka CCM?

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Waungwana salaam!

Chama kikuu cha upinzani nchini yaani CHADEMA kimekwisha fungua dirisha la wanaotaka kugombea urais kupitia chama hicho kuanza kuomba. Dirisha hilo limefunguliwa mapema zaidi ya chama tawala cha CCM tofauti kabisa na ilivyokuwa uchaguzi uliopita wa mwaka 2015. Ikumbukwe kuwa mwaka 2015 CHADEMA/ UKAWA hawakufungua dirisha la wagombea urais mapema badala yake walifungua dirisha la udiwani na ubunge tu.Ilkuwa mpaka CCM walipomaliza mchakato wao wa kumpata mgombea urais ndipo CHADEMA walipoibuka na "kapi" kutoka CCM kama mgombea urais yaani Edward Ngoyai Lowassa.

Lakini kwa mwaka huu hali ni tofauti CHADEMA imefungua dirisha la urais mapema zaidi na kuacha dirisha la ubunge na udiwani likiwa limefungwa. Hii maana yake nini? Je tayari CHADEMA imeshaona kwamba mchakato wa urais ndani ya CCM mwaka huu hautatoa "kapi" lolote la maana? Ama tayari CHADEMA inaye mgombea wa Urais hivyo haioni haja ya kusubiri "kapi" kutoka CCM?. Hii ni dhahiri kwamba mgombea wa urais wa CHADEMA hivi tunavyozungumza hayupo ndani ya CCM.

Je vipi kwenye ubunge na udiwani?
Ni dhahiri kwamba kwa huu mfumo mpya wa CCM hasa uongozi wa Magufuli anayetaka kukidhibiti chama kwa kuweka watu anaowataka basi ubunge na udiwani utaacha wagombea wengi ndani ya CCM wasioridhika ambao wataamua kutimkia upinzani. Hili litachangiwa zaidi kwa kanuni hizi mpya za uteuzi wa wagombea ndani ya CCM, ambapo kamati kuu ya CCM ndiyo itakayoteua majina matatu ya wagombea na kuyapeleka kwa wajumbe kwa kura za maoni. Ni wazi wagombea ambao watahisi wanakubalika na hawajateuliwa kwa vile tu siyo vipenzi au watu wa Magufuli watataka kwenda vyama vingine huku CHADEMA ikiwa destination muhimu.

Hivyo basi kwa CHADEMA kutokufungua dirisha la ubunge na udiwani mapema ni kujaribu kusubiri majeruhi watakaotokana na mchakato wa ndani wa CCM, naam "makapi".

Angalizo;

CHADEMA inapaswa kuwa makini kuepuka makosa waliyoyafanya mwaka 2015, kwani wengi wa makapi hawajiungi na chama kiitikadi bali kimaslahi zaidi.
 
Hizo nafasi za ubunge na udiwani zilishatangazwa kitambo kidogo kupitia office za kanda.
 
Huwa tukichukua makapi tunayapika yakiiva na kuwa chakula kinacholika CCM wanarudi kuyachukua... CHADEMA ni chuo kikuu cha SIASA nchini

Jr
 
Back
Top Bottom