Tangia Rais Magufuli aingie madarakani, ameonyesha wazi kuchukizwa na utawala wa serikali ya awamu ya nne jinsi ilivyo shindwa kusimamia mapato ya nchi na kusababisha wananchi kunyonywa na kikundi cha watu wachache na asilimia kubwa ya viongozi waandamizi waliotumia madaraka yao kujilimbikizia mali na kuwaacha wananchi katika ufukara mkubwa.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wabunge na mawaziri wa serikali ya nne walionekana wazi kutetea serikali ya awamu ya nne pale iliposhambuliwa na wapinzani kwamba ni dhaifu na imekuwa ikitumia vibaya mali za umma na hasa safari za Rais na viongozi waandamizi nje ya nchi kwamba zinaingizia nchi hasara..wabunge wa ccm na mawaziri walisema wazi kwamba safari hizo zinaletea nchi faida na kwamba wapinzani walikuwa wana wivu na waongo.
Lakini mwaka huu wamebadilika ghafla na kujifanya kwamba walikuwa siyo wao waliokuwa wakitetea kwa nguvu zote na ile serikali iliyokuwa madarakani wala haikuwa ya ccm bali ya watu wa Chalinze tu, je huu siyo unafiki au ni kusahau?
Mliwasikia wakisema kwamba hata kama hujui kusoma unashindwa hata kuona picha? wakimaanisha kwamba serikali ya awamu ya nne imeleta maendeleo makubwa sana na kuboresha maisha ya watanzania, leo hii wamebadilika wanaonesha kwamba ile serikali ilikuwa mbaya na kiongozi wa awamu ya tano ndiye anajuwa kuongoza na kusimamia mali za umma.
Je huu ni unafiki au ni kujisahulisha?