absolutely! kwa sababu hatujaathirika moja kwa moja na hayo yote unayoyasema. Sasa hivi tunaishi kwa misingi kuwa endapo mimi na familia yangu tumepata chakula cha jioni, na watoto waemeenda shule na tuna nguo na mahali pa kulala hayo mengine mimi sijali. Hatukasirishwi na kuona mwingine anahangaika na mahitaji yake ya kila siku.
Wakati mwalimu aliongoza kwa sera ya "kabla wachache hawajishi katika anasa, wengi wapate mahitaji yao muhimu" leo hii kina Kikwete wanahakikisha "wachache wanazidi kuishi katika anasa huku wengi wakiahidiwa mahitaji yao muhimu". Matokeo yake, leo hii tunategemea wageni kutuchimbia visima; tunatarajia watu binafsi kuendesha shule za msingi na sekondari, n.k
Watu wakikataa kuridhika na wakatamani makubwa zaidi, mazuri zaidi na mema zaidi kwa sababu wanastahili wataona umuhimu wa cha kufanya. Lakini tukipewa kanga na tsheti huku tunaburudishwa na wimbo wa "nambari wani eeh" tunaridhika na kufurahia kuwa na sisi tumepata vikofia vya chama!

Mzee Mwanakijiji pamoja na majibu yako mazuri lakini bado nikuulize:Hivi Tanzania kuna middle class?Asilimia ngapi vile?Na masikini kwa kiwango cha chini ya dola moja kwa siku ni asilimia ngapi vile?
Kwa mtazamo wangu naona wengi ndiyo wanaathirika moja kwa moja na huu ubinafsi wa kina Chenge na Ndulu manake masikini ndiyo wengi na siyo vijijini tu hata mijini kama Dar Es Salaam ambayo mara nyingi ndiyo inatumika kama kioo cha Tanzania bado kuna watu wanaishi maisha ya dhiki sana.
Sasa tatizo letu nini mpaka tukaridhika kiasi hiki hata Tanesco wanapandisha bei ya umeme kisa kuilipa Richmond lakini tunaishia kulalamika tu na tusichukue hatua yoyote?Kuridhika gani huku tunajua viongozi wetu wanapoteza mabilioni ya shilingi kujiagizia magari ya kifahari,wanalipana posho nzitonzito kwenye vikao visivyo na tija wakati sisi hatujui jioni tutakula nini au lini dawa zitakuwepo kwenye zahanati zetu ya kata?Kwavile hatujui haki zetu au?Yaani pamoja na utandawazi wote huu,utitiri wote huu wa habari na mawasiliano?Hao wazee waliokuwa wanagoma kuburuzwa na Nyerere wangepata bahati kama tuliyokuwa nayo sisi,hii nchi ingenyooka haraka sana.Mkuu mimi naona hatujaridhika.Tuna donge zito sana katika mioyo yetu isipokuwa tunaogopa kulitoa na kuliweka katika vitendo.Tunataka mabadiliko isipokuwa bado tuna uoga katika kuchukua hatua na ndiyo maana tunaishia kunung'unika chinichini.

Mkjj umesema kitu kikubwa sana hapo. Nimeliona hili kwa marafiki wengi sana ambao ukiongelea matatizo yanayotokana na uongozi mbovu nchini mweru wanakuwa hawakuelewi kabisa na kutaka kukuonyesha kwamba hujui unaongea nini basi watakwambia "Wewe unaishi nje hali hapa nyumbani si mbaya kiasi hicho usiyaamini sana yote unayoyasikia au kusoma kwenye magazeti." Wengi wa hawa ni wale ambao wameridhika na maisha yao wana mishahara minono wanaweza kuafford shule za kulipia wana magari wengine zaidi mawili. Mimi huwaambia kwamba mficha ugonjwa maradhi yatamuumbua kwa maana kwamba ncghi yetu ina matatizo makubwa sana na Watanzania wengi wamekata tamaa ya maisha kutokana na utendaji mbovu wa Vuongozi wa juu ndani ya Serikali ambao wameweka mbele maslahi yao au ya CCM na kuwasahau kabisa mabilioni ya Watanzania ambao wanaishi maisha ya dhiki ya kutisha, siku ambayo hawa waliokata tamaa ya maisha wakisema sasa basi liwalo na liwe hata hao ambao wana maisha mazuri basi maisha yao yatakuwa hatarini na watajuta kwa nini walifumbia macho uongozi mbovu kwa miaka mingi nchini kwetu.
Wakuu:
Halafu picha ya juu walioshika mabango ya sita na kikwete utaona wengi waliojitokeza ni vijana ambao huko juu nimetoa hoja kwamba hao ndio nguvu ya mabadiliko.
Hao wakipewa kofia ya buku 2 na flana ya buku jero wanauza uhuru wao
- Mkuu wangu hata mimi I am lost kama wewe if you will, I mean ninaona jinsi Health Care bill ilivyokwama tena over the most popular ever president wa US, na hii inafanywa na the minority party, sasa swali langu ni kwamba sisi tunashindwa nini?
- Look kina Raila Odinga sasa hivi, hawa ni nini they are doing right mpaka wanasikilizwa na watawala wao ambacho sisi tunashindwa?
Respect.
FMEs!
Mkuu tupeane pole, maana kwa kweli haya majambo yanauma. !
Mkuu naona umekula maji ya bendera mtatawala milele maana wadanganyika wamesha lewa na maji ya bendera ya kijani.
Mkuu tupeane pole, maana kwa kweli haya majambo yanauma. Nafikiri jambo moja ambalo hatujafanikiwa kulifanya ni kuhusisha ubovu wa uongozi tulio nao na shida ambazo wananchi wanazipata. Kila nipitapo vijijini nikiongea na wananchi unawaona wanavyosononeka, lakini ukiwauliza mnafikiri tufanyeje hatuongei lugha moja kama hii hapa JF. Hawaoni kabisa kama mazira yaliyopo yamesababishwa au yanasabishwa na uongozi na serikali tuliyo nayo kwa kiasi kikubwa na hawaoni kama hii serikali ndiyo inapaswa kuwa kinara wa kuyatatua. Ndio kusema wanapoenda kupiga kura hawaendi kuchagua mtu wa kutatua matatizo yao na ya taifa; wanaangalia vigezo vingine--mostly the most visible party and we all know which party this is. Na kama kuna sehemu watawala wamefanikiwa ni hapa-'keep them in dark for ever strategy'. Na hapa ndipo walipoanzia akina Raila. Leo hii wakenya wapo clear na kipi cha serikali na kipi cha mwananchi, na wanajua wanapokwama wapi wajilaumu wao na wapi waijabishe serikali yao.
Leo hii watanzania, tena wasomi kabisa, hata kazi za bunge hatuzijui--kama umefuatilia mjadala wa wanabidii. Utachoka!!
- CCM inazidi kujitandaza mpaka majuu jamani! sasa hawa sio wananchi wa vijijini ndio maana ninasema sometimes huwa ninawaza sana kwamba hapa JF huenda hatuwakilishi mawazo ya wananchi wengi wa Tanzania, au?CCM london
Shoto ni katibu siasa na uenezi Bw. M Katega akiwakabidhi katiba ya chama cha Mapinduzi viongozi wa tawi la South London Mwenyekiti Bw. Kassim Hassan na katikati mjumbe wa tawi hilo Bw. Seth Mdendemi
katibu siasa na uenezi Bw. M Katega akiwakabidhi katiba ya chama cha Mapinduzi viongozi wa tawi la East london Katibu wa tawi Bi Mariamu Mungula na Mjumbe Bw. Iddy Mwanga
kushoto Bw. Frank Mukiza, Kassim Hassan, Mariamu Mungula, M Katega, Seth Mdendeni na aliyekaa ni Pashency Linus
kutoka shoto ni Neema Kumba, mwandishi wa Tanzaniaone UK Bw. Ally Muhdin na Katibu wa tawi la East London Bi. Mariamu Mungula
Chama cha Mapinduzi CCM jana jumamosi ya tarehe 27 mwezi wa pili mwaka 2010 kilifungua mashina mawili na kuchagua viongozi wa kuongoza mashina hayo jijini London Uingereza. Mashina hayo yalifunguliwa na katibu siasa na uenezi Bw. Katega. Mashina yaliyofunguliwa ni sina la South London na Shina la East London.