Je, CCM imeweza kutuletea maendeleo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, CCM imeweza kutuletea maendeleo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chapakazi, Jun 23, 2011.

 1. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Great Thinkers naomba tujadili maendeleo CCM iliyotuletea toka ichukue madaraka. Ivi kuna kitu CCM imefanya 'beyond the ordinary'? Ni sera gani CCM imeweza kusimamia kwa nguvu zake zote kuhakikisha hiyo sera inafanikiwa? Hapa tunaweza kuweka mfano wa ELIMU, Maji safi, Umeme, Kilimo, nk?
  Tunapoongelea maendeleo na ninachomaanisha kwa phrase ya 'beyond the ordinary' ni kama Dr Slaa alivyoeleza wakati wa uchaguzi. CCM kama chama kilichoko madarakani na chenye nguvu ya kisheria ya kukusanya kodi, kwa wao kusema tumejenga barabara sio kuleta maendeleo. Hilo ni jambo ambalo ni lazima lifanywe na 'the government of the day'. Ni sawa na baba mwenye nyumba aseme nimelisha familia yangu.
  Hapa tunaongelea maendeleo in the sense of eradicating a specific problem (eg: malaria) or dealing with a certain issue and resolving it completely (eg: unemployment). Kwa hiyo swali linakuja, CCM imeweza kutuletea maendeleo gani? Kuna tatizo gani ambalo CCM imeweza kulikalia kinaganaga na kulimaliza? Kama hakuna, kwa nini bado tunaimba na kukenua nao mpaka leo? Au ndio ujinga wetu ambao iliahidi kuuondoa mwaka 1961? (mind you, ccm = TANU + ASP)
   
 2. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Nashukuru kwa hoja nzuri sana na kwa wakati muhafaka

  jibu ni ccm kwa kaliba ya watu iliyonayo kwa sasa hawawezi kutuletea maendeleo.

  Viongozi wa nchi wanaokumbatia ufisidai kamwe hawawezi kuwa chachu ya maendeleo sababu juhudi zao siku zote zitakuwa ni kuchota fedha badala ya kufikiria matatizo ya wananchi.

  Nchi yenye misamaha ya kodi mpaka kwa mwekezaji mwenye mtaji wa milioni mia moja na nusu kwa muda wa miaka kumi kamwe maendeleo hayatapatikana kirahisi.

  Nchi amabayo toka baba wa taifa afariki hakuna kiongozi anakuja na priority ya jambo analokusidia kulifanya na kulikamilisha kwa ufanisi ni dhahiri kwamba maendeleo ni ndoto.

  Nchi yenye mfumo wa elimu usioeleweka hata kwa shule za msingi ni dhahiri hii ni hujuma ya kuwafanya watanzania wakose uwezo wa kutafakari kwa maendeleo yao.
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Uliyosema yana ukweli, lakini je na wakati wa huyo baba wa taifa, alituletea maendeleo gani?
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sasa wewe umeleta point alafu unataka mimi niifanyie uchunguzi? Ndio namna gani tena hiyo? Na kama sikubaliani na point yako from the start?
  Viwanda gani vimejengwa? Toa mfano tafadhali na fafanua maendeleo yake...
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi ccm ni ya kijamaa au kibepari, au hata wenyewe hawajui. Naona kama wamepoteza dira (Network). Hawana falsafa, itikadi wala sera. Sijui lakini.
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Inaelekea ccm wameiga mfumo wa china. Ijapokuwa hawajakaa kuwa wajamaa, wame-embrace capitalism!
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,122
  Likes Received: 6,606
  Trophy Points: 280
  CCM imeweza kuwaletea maendeleo watu wachache sana ambao imewapa madaraka makubwa serkalini na kwenye chama na kuwaangalia jinsi wanavyoneemeka.
   
 8. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM
  1. inapambambana na malaria kwa kusambaza vyandarua badala ya kupambana na mbu anaesambaza hayo malaria
  2. inanunua bajaji kwa wajawazito badala kua kuhakikisha kuna zahanati za kutosha karibu na wananchi ili tusihitaji hata hizo bajaji ambazo wala haziwezi kupita kwenye barabara zetu zenye mashimo
  3. iliweka miundombinu ya maji taka DSM tena kipindi hicho walisababisha foleni kubwa sana dar lkn hadi leo huo mfumo haujaanza kutumika la sivyo tusingeona maji kujaa nyakati za mvua
  4. n.k
   
 9. notmar

  notmar Member

  #9
  Jun 24, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  baada ya miaka 50 ccm imeweza kufanya yafuatayo.
  1. kuua miundombinu ya reli
  2. kushindwa kuendeleza bandari za tanga,dar,mwanza,mtwara,kigoma,na zanzibar .
  3. kuua shirika la ndege ATC na mifumo yote ya usafirishaji wa anga na kutugeuza sissi abiria wa kenya,ethiopia ,na south africa.
  4. kukaribisha uwekezaji holela na kugeuza viwanda vyetu kuwa magodown
  5. kushindwa kusimamia rasilimali za taifa kama madini ,ardhi,na mbuga za wanyama na kuzifanya kuwa ni mitaji ya wageni
  6. kuigeuza tanzania soko la bidhaa feki kutoka china
  7. kuigeuza tanzania kuwa shamba la bibi la wakenya na south africa
  8. kuiingiza nchi kwenye mikataba mibovu km ricmond dowans,symbion,rada ,meremeta,kagoda,tangold etc.
  9. kuwafanya watanzania wahanga wa mauaji yanayofanywa na wawekezaji na polisi.
  10. kuendeleza ujinga kwa kutoa elimu duni ambayo haikidhi viwango vya kimataifa.eg.shule za kata.
  11. kuwageuza vijana kuwa wamachinga na kutetea hali hiyo kwa kujenga machinga complex ambayo hata hivyo hawafaaidiki nayo.
  12. kuedelea kuutukuza mwenge na kutumia pesa nyingi za watanzania kuuzungusha nchi nzima
  13. kuendelea kutetea uzembe ktk jeshi hata wanapofanya madudu kama ya mbagala na gongo la mboto.
  14. kuifanya tanzania kuwa matonya(ombaomba)wa dunia hivyo kupoteza heshima kimataifa.
  na sasa wanaandaa bonge la sherehe ambayo haijawahi kushuhudiwa duniani ya kutimiza miaka hamsini.
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mgao masaa 18
  BAE wapate kuliko watanzania
  Epa?
  Kagoda?
  Reli?
  NK

  Haya ndio wanayoweza CCM
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo ccm haina chochote cha kujivunia? Sasa hao wasomi huko ccm wanafanya nini? Hao ma-professor na madokta? Au ni njaa tu? Elimu yao wameipata wapi kiasi wanaitupa na kuweka tumbo mbele?

   
Loading...