Je, CAG alichakachua hata taarifa ya ukaguzi UDOM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, CAG alichakachua hata taarifa ya ukaguzi UDOM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by miradibubu, Nov 20, 2011.

 1. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana jamvi, kwa taarifa nilizozipata toka kwa wafanyakazi wa chuo kikuu cha Dodoma, wamefurahia sana namna ambavyo CAG na Katibu kiongozi walivyoumbuliwa na kamati teule ya bunge.
  Furaha hii ya wanaudom inadaiwa ni kutokana na kuthibitishwa kwa hisia zao kuwa ukaguzi uliofanywa na CAG hapo UDOM katika kipindi cha mgomo wa wahadhiri ulilenga kuficha ukweli ndio maana CAG alitanganza kutoona ubadhirifu wowote.

  Mambo yanayosababisha wanajumuiya hiyo wakose imani na CAG pamoja na Katibu kiongozi ni kutolewa kwa salary slip mbili tofauti kwa mtumishi mmoja na zote zina mishahara miwili tofauti hii kwa baadhi ya watumishi limefanyika kwa zaidi ya miaka miwili na ushahidi upo kabisa wa salary slip hizi.

  Salary slip moja ni ya kutoka hazina ambayo inamshahara sahihi(mkubwa) na nyingine ni ya Udom yenye mshahara wanaojua wao(sio sahihi). katika hili pia wanajumuiya walijiuliza je uongozi wa chuo ulitumia utaratibu gani kubadilisha mishahara ya watumishi kwani hata watu wa hazina walipohojiwa juu ya hili walionekana kushangaa na kuonekana kuutambua mshahara unaotoka hazina pasipo mashaka yeyote, lakini huyu CAG hakuona tatizo lolote.

  Matokeo ya kuwepo kwa salary slip mbili kumewafanya wafanyakazi wa chuo kikuu cha Dodoma kulipwa kwa kiwango cha chini tofauti na vyuo vingine vya umma. Ushahidi upo wazi, kwani mhadhiri msaidizi wa Udom(anayeanza bila kujali uzoefu PUTS 13) analipwa sawa na mkufunzi msaidizi wa chuo kingine cha uma(tutorial assistant) -angalia OUT AU UDSM

  Jambo jingine linalojitokeza katika kuwepo kwa salary slip mbili ni je baada ya kuwa kata mshahara hawa wafanyakazi wa udom hicho kinachokatwa kinaenda wapi wapi?

  Katika mateso yanayowakabili wafanyakazi wa UDOM imebainika kuwa katibu mkuu kiongozi ana mkono wake. Hili linadaiwa ni kutokana na mahusiano yake na makamu mkuu wa chuo ndugu Kikula hawa wote wanatokea sehemu moja huko Iringa(ukanda na ukabila). Kutokana na mahusiano haya ya karibu inadaiwa kuwa katibu mkuu kiongozi alitoa maelekezo ambayo si sahihi ya namna ambavyo ukaguzi wa kubaini ubadhirifu udom ufanyike. Matokeo yake ni kutoa mwanya wa ofisi ya fedha na utawala ya ndg Mlacha kuonekana kuwa ni safi. Kwani inadhaniwa kwamba isingekuwa rahisi kwa mlacha kuwa mchafu na kikula kawa msafi tumia mfano wa jairo na ngeleja.

  Katika kutangazwa kuwa hakuna kosa lolote Pinda alionekana pia kudharirishwa(huenda ya bungeni kuhusu jairo ni ya pili) kwani alipokuja kutatua mgogoro wa wahadhiri aliwahakikishia wanajumuiya kuwa suala la Mlacha ni suala la muda. Kutokana na hali hii tunaona kwamba tabia ya katibu kiongozi kulinda au kujihusisha na ufisadi ni suala ambalo amebobea na matokeo yake ni kuidhalilisha serikali hii ya ccm.

  Katika nsakata la udom, Huenda kutokana na madudu ya CAG na katibu kiongozi(mtazamo wangu) imesababisha kuleta hisia kwamba huenda mheshimiwa raisi anajikuta analinda mafisadi kwa kigezo cha udini( hoja iliyatawala kipindi fulani miongoni mwa wanajumuiya kwamba Mlacha anaandamwa kwa sababu ya dini yake), Kutokana na kazi nzuri ya kamati teule hata kwa baadhi ya waislamu wameanza kuona namna ambavyo dini yao nzuri inavyotumika kama kichaka cha kufichia mafisadi na watendaji wenye kiburi cha ajabu.

  Hivyo basi wanajumuiya ya UDOM wananaiomba kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma kuipitia vema ripoti ya CAG ili kubaini ufusadi wake. CAG na Luhanjo dhambi ya UDOM imewaumbua! Ninawasilisha
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  It is obvious.....
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Jamaa kapakaa 'mavi' mwili mzima. Nadhani UN inabidi wajiulize mara 2 kuhusu uteuzi wa huyo 'mwizi' ktk ofisi zao. Hii inchi yote imeoza kabisa, hata wale wanaoonekana ni nafuu kumbe ni syndicate wa ikulu ktk wizi, mweeeeeeeeeee!
   
 4. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ndiyo madhara ya Uteuzi wa Rasi. Lazima ufuate anachotaka hata kama ni kuidhalilisha Fani yako.
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Yaani mzee Utoh na alivyo msimamo...na maadili amebadilikia uzeeni baada kupewa panono!!aibu sana sana kwake na Luhanjo wake??shame on you babus
   
 6. p

  politiki JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  yaani kama hata ofisi ya CAG haiaminiki sasa nchi jamani tutamwani nani jamani ??
   
 7. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #7
  Nov 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli nchi yetu mahala ilipofika kwa sasa inasikitisha sana, aibu kama taifa, wasomi ndo wanahiujumu hii nchi wala sio babu yangu mkulima kule kijijini. Alafu inatia kinyaa pale ninapowaona wabunge wa c.c.m wanapounga mkono hoja.
  Nachoweza kueleza kwa sasa, hii nchi tutakuja kupigana mapanga wenyewe kwa wenyewe, the day is coming soon, keki ya taifa letu wanatafuna kikundi kidogo cha watu. Wait
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mi mamionaga huyu cag naye ni jizi tu la kutupwa..miezi lukuki wanashinda hotelini pale girrafe kujifanya wanapitia report badala yakukaa ofisini...
   
 9. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Hilo la udom nlishangaa sana ofisi ya CAG ilivyowasafisha,na mpaka sasa hv kwa mujibu wa taarifa nlizozipata kutoka kwa mdau anayefanya kaz pale ni kwamba uongoz wa udom unalipiza visasi kila kukicha kwa kufukuza wahadhiri!taifa linakwenda wap kwa mtindo huu?
   
 10. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  CAG ni mtu mzima hovyo!!!!!!!!!!
   
 11. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli suala la UDOM hata angepewa darasa la saba kukagua angegundua ubadhirifu mkubwa.Sio siri nilishtushwa sana na majibu ya CAG ktk suala lile na ndio hapo nilpojua kuwa ameshaharibiwa.Sasa sijui sasa hivi ktk serikali yetu ni nani aliyemsafi.
   
 12. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Wadau hebu tuwasidieni hawa wanajumuiya ya UDOM wafanye nini kuwawajibisha hawa mafisadi waliopo katika sakata zima la mgogoro wa wahadhiri. Kwani nionavyo mimi kama salary slip mbili kila mfanyakazi anazo na zina malipo tofauti na wakati huo huo pesa iliyokatwa haijawahi kurejeshwa hazina. Je wakienda mahakamani wanaweza kupata haki yao. Kwani kuna ushauri nilioutoa wa kuiomba kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma kuiangalia ripoti ya CAG KUHUSU UDOM linaonekana kuwa na udhaifu mkubwa kwani ndani ya kamati hiyo kuna home boy wa makamu mkuu wa chuo Kikula ambaye ni Deo filikunjombe anayemtetea kikula kwa nguvu zote, Ndio maana kamati hii ilipopewa taarifa na menejimenti ya UDOM kwamba kila mfanyakazi wa UDOM anapewa pesa ya "mazingira magumu" wamekubali kiurahisi licha ya kuthibitishiwa na wafanyakazi kwamba kama hiyo pesa inatolewa labda ni kwa menejimenti peke yake na wao hawataki kuwaamini wafanyakazi. Tuwasidieni jamani wana UDOM kukabiliana na hii hali ngumu iwakabiliyo
   
 13. m

  mbweta JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mlianzaje kuiamin ofisi ya CAG jaman ile inatumika kama sabuni ya kusafishia wachafu. Mie naamin uwez kuwa msafi wakati mazingira yanayokuzunguka sio safi. Tatizo ni kuteuliwa na Rais lazima awe royal kwa bosi wake. Hapa tubadilishe kabisa system za watu kuteuliwa tutafute njia mbadala. CAG anaweza kua mwadilifu lakin bos wake akamvuruga. Kwenye public audit act inaonesha anafanya kazh on behalf of national assembly lakin uteuzi wake anafanya raisi hapa si sawa.
   
 14. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Cag ataibeba dhambi hii ya udom
   
 15. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Uchakachuaji uko wazi kabisa tukumbuke kwamba ofisi ya CAG haiko independent inafanya kazi kwa shinikizo. Nakumbuka ofisi hiyo iliwahi kulalamika kwamba inapata wakati mgumu kwa kuwa wakati mwingine wanalazimika kuwakagua wakubwa wao. Msingi wa yote haya ni katiba ya sasa hivi ambayo inampa madaraka makubwa rais ya kuteua watendaji mbalimbali wa serikali ambao wanawajibika kwake moja kwa moja. Katika mazingira kama haya inakuwa vigumu kwa CAG kuanika uozo unaofanywa na watendaji waliokaribu na rais au uozo unaohusisha viongozi wa ngazi za juu wa serikali.

  Tunaweza tukamlaumu sana CAG lakini tunapaswa kufahamu kwamba yeye ni mteule wa rais na watumishi wanaobainika kutenda madudu licha ya kuwa wengi ni wateule wa rais lakini bado pia wana uhusiano wa karibu sana na hivyo mkuu wa kaya anaweza ku-influence matokeo ya uchunguzi. Kwa maana hiyo CAG nae analazimika kulinda ugali wake kama ambavyo watu wengi wangefanya. Tatizo kubwa lililopo hapa ni MFUMO uliopo unaompa rais madaraka makubwa sana ya uteuzi kiasi cha kuweza kuathiri chunguzi mbali mbali zinazogusa watu wake wa karibu.

  Bahati mbaya sana wanasiasa na watendaji wengi hawana moyo wa kizalendo wa kuchukua maamuzi magumu ikiwa ni pamoja na kupingana na mashinikizo na hivyo kuchukua uamuzi wa kujiudhuru ili kulinda heshima zao kama ambavyo viongozi kadhaa wa nchi jirani ya Kenya wamekua wakifanya wanapotofautiana na wakubwa wao. Viongozi kama waziri mkuu Pinda alipaswa kuwa amejiuzuru siku nyingi maana amekuwa akitamka maneno mazito kama kwenye sakata la UDOM na lile la Jairo lakini Mkuu wa kaya kampotezea na yeye ameendelea kuonekana kama mropokaji ambaye anazungumza mambo ambayo hana uhakika nayo.

  Alipoenda UDOM baada ya kuelezwa issue yenyewe na kupewa vielelezo alikili kuwa issue ile ilikuwa nzito lakini mwisho wa siku CAG akasema hakuna madudu yoyote yaliyofanyika UDOM na Pinda akanywea. Hali kama hiyo ilijirudia kwenye sakata la JAIRO. Siku za mwizi ni arobaini hatimae sakata la JAIRO limemuumbua CAG.Ukweli ni kwamba kama kamati teule ya bunge itakwenda kufanya uchunguzi pale UDOM watugundua uozo mwingi sana ambao hauta waacha viongozi wa juu salama.

  Namuomba spika Makinda afanye kama alivyoahidi jana wakati akiahirisha kikao chabunge kwamba kamati za iana hiyo zitaendelea kuundwa nyingi zaidi ili kuchunguza masuala kadhaa yanayohusu matumizi mabaya ya pesa za umma. In gekuwa ni busara zaidi aanze kuunda kamati kwenda kuchunguza UDO M ambapo inaonekana watu wameamua kutumia upya wa chuo kujineemesha wenyewe.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,877
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Simfahamu kwa karibu huyu CAG lakini mara tu baada ya kuteuliwa kama Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA nilianza kusikia sifa mbali mbali mbaya kuhusu huyu jamaa na wengi kutoridhika kwa yeye kupewa wadhifa ule. Pamoja na shinikizo la Ikulu huyu jamaa hayuko makini kabisa katika utendaji wake wa kazi anaweza kabisa kupindisha sheria na taratibu ili kuuficha ukweli. Kama sikosei huyu CAG pia hakuona tatizo lolote baada ya ukaguzi wa gharama za ujenzi wa nyumba ya gavana wa BoT ambayo iligharimu shilingi bilioni 1.4 pesa za walipa kodi. Pia huyu ndiye aliyemsafisha Jairo katika kashfa ya kukusanya pesa na kuwalipa Wabunge ili waipitishe bajeti ya Madini na Nishati.

  CAG amekwishachafuka hastahili tena kuendelea kushika wadhifa huo, lakini kama mjuavyo ndani ya Serikali ya msanii kuna wengi ambao hawastahili kuendelea kushika nyadhifa zao kutokana na madudu chungu nzima waliyoyafanya lakini bado wanaendelea kupeta tu na sia ajabu wataendelea kupeta hadi 2015 (akiwemo huyu CAG).

   
 17. T

  Taso JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Kuna sehemu huyu fisadi alibanwa mbavu na Mwenyekiti wa Kamati Teule kuhusu ripoti yake iliyogeuka kujibu magazeti badala ya Hadidu za Rejea za Bunge. Akaambiwa awasomee vipengele alivyoandika, akaanza kidogo halafu akatema, "hapa nilichemka! Mwenyekiti akamuuliza, ulichemka? Akasema kwa upole, yah!
  Pathetic
   
 18. L

  Luiz JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu CAG nilikuwa namwamini sana ila toka apewe kazi ya kufanya ukaguzi pale udom na kuja na report yake kuwa hamna maovu yaliyotendwa pale udom ndipo nimwona madudu lakini mungu si athumani akidhihili mbele umma wa watanzania kuwa yeye ni madudu kwa report ya Jairo cjui haya magamba yaipeleka wapi hii nchi maana hii ni wizara moja je! hizo nyingine.
   
 19. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jamani tuwasaidieni hawa watu wa UDOM ili kup[atahaki yao je waende mahakamani au kuna uwezekano wa kutumia njia gani ili ripotiya CAG kwanza iweze kupatikana ili tuone mahitimisho yaliyotolewa na CAG yamefikiwa kwa kuegemezwa katika hoja zipi. CAG wanaUDOM hawatakusamehe kwa dhambi hii kubwa ulioifanya kwa pamoja na Luhanjo hapa UDOM
   
 20. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #20
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ofisi ya cag inanuka rushwa mbaya ule ni mtandao wa kupiga pesa za umma,uttoh ndiye aliyekagua juu ya kashfa ya bot kuhusu ukarabati wa nyumba ya gavana ambao ulifikia bill.1.4 akasema kawaida tu hiyo,akaenda udom akaja na majibu mepesi sana,funga kazi ilikua kwa jairo,kuna jamaa yangu anafanya kazi pale ofisi ya cag anasema kampuni zake uttoh ndio zinafanya audit na yeye anasaini tu,ile ya udom alichakachua k'bu pinda alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwa maslahi ya umma watachukua hatua k'bu uongozi umeshindwa kujibu maswali yake!
   
Loading...