Je, Benki ya CRDB inashirikiana na Wezi wa Mitandaoni?

Kama kitu hufahamu nyamaza, Mdogo wangu ni Mama wa watoto lakini pia tangu kuzaliwa kwake hajawahi kuonja pombe so be ken.
Wewe acha kumuamini huyo mdogo wako, fanya udadisi utakuta anakudanganya, lazima kuna uzembe aliufanya.

Usisite kuleta mrejesho wa malalamiko yako!
 
Pesa imehamishwa kwenda laini za tiGO na Vodacom kama muda wa maongezi (airtime)
 
Kama kitu hufahamu nyamaza, Mdogo wangu ni Mama wa watoto lakini pia tangu kuzaliwa kwake hajawahi kuonja pombe so be ken.
Kumbe huyo mdogo wako ni wa kike? Ebu tupiako kapicha basi humu tena sasa hivi wana tujiridhishe tuingie chimbo tumsaidie hela zake zirudi.
 
Si salama kuiweka account namba yake hapo, pili hapo hela imetolewa tolewaje? Kuna mtu alichukua simu yake? Au ameibiwa au meseji imekuja tu katoa hela?

Vingine unaweza sema bank inashirikiana na wezi kumbe uzembe wa mmiliki, nasema uzembe sababu mtu akiijua namba yako ya siri au ikaweka mwaka wa kuzaliwa unapigwa kweupe na tulishakutana nayo
 
Pesa imehamishwa kwa njia gani? Chukueni bank statement,

Kama imehamishwa kwa sim banking kuna uwezekano kuna mtu kamcheza....

Si rahisi sana benk kutoa pesa zako...
 
Pesa imehamishwa kwenda laini za tiGO na Vodacom kama muda wa maongezi (airtime)
Yaani unakuja kulalamika hapa jf!

Bafala ya kuwaandikia Benki husika barua/email ya malalamiko yako unawakopi Mamlaka inayosimamia hizi.benki nadhani Benki Kuu na KM wa Wizara husika.

Yaani ingefanyiwa kazi mapema na kupewa mrejezho wa malalamiko yako.
 
Wasalaam,

Hii inaumiza sana, hivi majuzi mdogo wangu alinipigia simu akilia kwamba pesa ya boss wake imeibwa kupitia simu.

Akiwa angalia anasema kutoka kwenye Akaunti yake namba 0152631907400 zilitolewa TZS 2,800,000.

Mdogo wangu anasema, pesa hiyo ni pesa ilikuwa kwaajili ya mishahara ya wafanyakazi wenzake.

Mdogo wangu yeye hana kadi ya Benki anatumia Simbank tu lakini pesa imechomolewa.

Mdogo wangu ameenda Polisi Dodoma nao wanasema hawana wapelelezi mpaka watoke mikoani.

Naomba uongozi wa CRDB ufuatilie swala hili kwa makini kwani linaipaka Benki yetu pendwa matope sana.

Abdulmajid Nsenkela wewe kama CEO tunakufahamu kuwa wewe ni mtu makini haya yanayoendelea yasipo dhibitiwa CRDB itapoteza Uungwaji mkono chini yako.

Natarajia kuanzia kesho mdogo wangu atarudishiwa pesa yake ili aweze kuwalipa wafanyakazi wenzake kwani wamegoma kuendelea kufanya kazi.

Pesa yote imehamishwa tena imehamishwa kama muda wa maongezi wa pesa yote TZS 2,800,00.

===
Mliokaribu na uongozi wa bank ya CRDB nifikishieni ujumbe wao huu.

​
MDOGO wako Kaa naye vizuri mhoji anahusika Moja kwa Moja.
Simu yake imehusika Moja kwa Moja hata maelezo yake hayafungi kwani Kuna maswali mengi ambayo majibu anayo yeye.
 
Pesa imehamishwa kwa njia gani? Chukueni bank statement,

Kama imehamishwa kwa sim banking kuna uwezekano kuna mtu kamcheza....

Si rahisi sana benk kutoa pesa zako...
Labda inawezekana!

Mimi kuna tukio liliwahi kunitokea kwenye akaunti yangu ya CRDB ya pesa kiasi cha sh. 1,000,000 kutolewa.

Kuna mshikaji wangu yeye alikuwa Dar alinikopa milioni 1, ilipofika mwisho wa mwezi tena ilikuwa siku ya Jumamosi kama saa 1 asubuhi aliniomba akaunti namba yangu ya crdb kwa ajili ya kwenda benki ya CRDB kuweka pesa niliyomkopesha, nikamtumia, mimi wakati huo niko mkoani.

Mimi nilipoamka nikapiga shughuli za nyumbani, baadae kwenye saa 4 asubuhi ikaingia sms ya CRDB kiasi cha 1 milioni kimetolewa kwenye akaunti yangu, nikahamua kujiridhisha kwa simbanking kama pesa imetolewa, kweli pesa imetolewa.

Nikasema huu ni wizi, nikaoga haraka nikabeba kadi yangu ya benki nikachukua gari nikawa naelekea tawi lao lilipo kwenye mkoa niliokuwepo.

Wakati niko njiani nikakumbuka mshikaji aliniomba akaunti namba yangu kwa ajili ya kwenda kuniwekea milioni 1, ngoja nimcheki. Nikampigia simu nikamuuliza ulifanikiwa kuweka ile pesa kwenye akaunti yangu, akasema ndio.

Nikamwambia mbona pesa haijawekwa bali imetolewa milioni 1, akasema ngoja aangalie akaunti yake, akasema kweli akaunti yake imeongezeka milioni 1, akasema bank teller mjinga sana sababu nimejaza form ya kutoa pesa kwenye akaunti yangu ya crdb kwenda kwenye akaunti yako ya crdb na nikampa na kadi yangu. Akarudi kwenye tawi husika akamfuata yule bank teller akamuelezea akaomba samahani akarekebisha makosa aliyoyafanya, akarudisha pesa aliyoitoa kwenye akaunti yangu na pia kuingiza milioni 1 kutoka kwenye akaunti ya mshikaji.

CRDB kuna changamoto nyingine nilishakutana nayo baada ya kulalamika mpaka kwa meneja wa tawi la ilo benki wakalitatua.
 
Sure, nadhani bado issue yao sio ya polisi. Bank wana uwezo wa kueleza pesa imetokaje....
 
Pesa imehamishwa kwa njia gani? Chukueni bank statement,

Kama imehamishwa kwa sim banking kuna uwezekano kuna mtu kamcheza....

Si rahisi sana benk kutoa pesa zako...
Pesa imehamishwa kwa njia ya simu na simu usiku na simu alikuwa naye tena ni miamala ya 200,000 na 50,000 mpaka 2,800,000
 
Back
Top Bottom