Je, Benki ya CRDB inashirikiana na Wezi wa Mitandaoni?

Je, Benki ya CRDB inashirikiana na Wezi wa Mitandaoni?

TWELVE12

Senior Member
Joined
Jun 5, 2024
Posts
150
Reaction score
137
Wasalaam,

Hii inaumiza sana, hivi majuzi mdogo wangu alinipigia simu akilia kwamba pesa ya boss wake imeibwa kupitia simu.

Akiwa angalia anasema kutoka kwenye Akaunti yake namba 0152631907400 zilitolewa TZS 2,800,000.

Mdogo wangu anasema, pesa hiyo ni pesa ilikuwa kwaajili ya mishahara ya wafanyakazi wenzake.

Mdogo wangu yeye hana kadi ya Benki anatumia Simbank tu lakini pesa imechomolewa.

Mdogo wangu ameenda Polisi Dodoma nao wanasema hawana wapelelezi mpaka watoke mikoani.

Naomba uongozi wa CRDB ufuatilie swala hili kwa makini kwani linaipaka Benki yetu pendwa matope sana.

Abdulmajid Nsenkela wewe kama CEO tunakufahamu kuwa wewe ni mtu makini haya yanayoendelea yasipo dhibitiwa CRDB itapoteza Uungwaji mkono chini yako.

Natarajia kuanzia kesho mdogo wangu atarudishiwa pesa yake ili aweze kuwalipa wafanyakazi wenzake kwani wamegoma kuendelea kufanya kazi.

Pesa yote imehamishwa tena imehamishwa kama muda wa maongezi wa pesa yote TZS 2,800,00.

===
Mliokaribu na uongozi wa bank ya CRDB nifikishieni ujumbe wao huu.

​
 
Back
Top Bottom