fullcup
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 809
- 2,216
Si jambo jema kuanza kurithi Mali au vitu vya marehem kabla hajazikwa au hajamaliza siku arobaini tangu kuzikwa kwake. Lakini katika maisha ya siasa na utumishi michakato huanza mapema sana Mara tu baada ya kifo kutokea. Yaani kama ni waziri uteuzi utafanyika. Kama ni raisi uapisho ni chap Kwa haraka, mtumishi, kibarua, mfanyakazi au hata kiongozi wa taasisi mfumo ni huohuo wa kutafuta mbadala mapema.
Mbarali tumepoteza kiongozi muhimu na mchapakazi haswa. Lakini haitufungi kufikiria mbadala wake. Kwa muda mrefu kumekua na dalili za mh Bahati Ndingo mbunge wa viti maalumu kupitia jumuia ya Wazazi kuonesha dalili na maandalizi ya kuchukua Jimbo. Amekua akijiandaa kimya kimya na chinichini sana kuanzia kwenye mashina na matawi na kuzungumzia sana mbarali bungeni.
Alikua akijiandaa Kwa kinyang'anyilo Cha 2025, baada ya hili kutokea atakua tayari kuchukua mikoba kuanzia Sasa au atabaki na msimamo wa 2025? Wana mbarali wanaweza kumpa ridhaa? Iwapo atahitaji kuomba ridhaa afanye Nini Ili kushinda?
Mpaka Sasa anaonekana kupewa nafasi kubwa ya kunyakua Jimbo. Hata kupewa nafasi ya kusoma wasifu wa marehem mbele ya waziri mkuu na Spika Nahisi ni Moja ya mkakati wa kumfanya aonekane Kwa wananchi Ili kivumbi kikianza asiwe mgeni machoni Pao.
Kidumu chama Cha Mapinduzi