Je, ACT-Wazalendo ya Zitto Kabwe kuwa kama UDP ya John Cheyo

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Kwa mtu anayefahamu vizuri historia ya siasa za Tanzania lazima atakuwa anafahamu vizuri historia ya UDP na sera yake ya Kujaza Mapesa.

UDP ilitikisa katika Mkoa wa Shinyanga na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza ambapo katika Uchaguzi Mkuu wa 1995 na 2000 ilijikuta ikipata Wabunge watatu wa kuchaguliwa na mmoja wa viti maalum. Cheyo alipata kura zaidi ya 250,000 ambayo ni asilimia 6.4 ya kura zilizopigwa.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 ulikuwa ni mwanzo wa kuifuta UDP kama chama hai kwa sababu kilipoteza Madiwani wengi huku Mbunge akibakia mmoja.

Tatizo Kuu la UDP ilikuwa ni sera zake za kuwajaza Watanzania Mapesa ambazo zilijibiwa na Rais Kikwete baada ya kuanzisha na kusimamia sera ya kuwapa uwezo wa kifedha wajasiliamali kwenye vikundi mbali mbali. Huu ndio wakati ambapo wananchi walipokea pesa zilizoitwa "Mabilioni ya JK". Hili lilikuwa ni jeneza la kisiasa la UDP. Mwaka 2010 ikawa ndio maziko ya UDP.

Kama ilivyokuwa kwa UDP, Jeneza la kisiasa la ACT-Wazalendo naliona pia liko njiani kutokana na sera zao za Unyerere. Sera za Unyerere zimeanza kujibiwa na Rais Magufuli ndio maana viongozi wengi wa ACT-Wazalendo wanajiunga CCM.

ACT-Wazalendo ya sasa imekuwa ni chama cha mtu mmoja. Zitto Kabwe ndio Mkuu wa Chama, Katibu Mkuu, Katibu Mwenezi, Mweka Hazina, Ofisa wa mambo ya nchi za nje na Mbunge.

Kama ilivyokuwa kwa UDP iliyokuwa na Mbunge 1 na Madiwani wengi kutoka Mkoa wa Shinyanga, kwa sasa ACT-Wazalendo ina Mbunge 1 na Madiwani ambao wengi wao wako katika Mkoa wa Kigoma.

Hakuna asiyejua kuwa CCM ilikuwa inamsaidia Zitto ili ashinde chaguzi lakini kwa sasa imeanza kuachana naye!

Tumeona kwa sasa CCM wameanza kupeleka nguvu za kisiasa katika Mkoa wa Kigoma huku wakicheza michezo ya kisiasa ambayo ACT-Wazalendo hawana uzoefu nayo.

Mchezo mmoja wa kisiasa ni pale ambapo ACT-Wazalendo wamejikuta wakiingia kwenye mtego wa kisiasa kwa kupandisha malipo ya kodi za vibanda kwenye Manispaa ya Kigoma Ujiji bila kufanya makubaliano na wafanyabiashara halafu CCM wakamtuma Katibu Mwenezi, Polepole kwenda kuongea na "wanaCCM" wa mkoa wa Kigoma kwa kigezo cha ufuatiliaji wa Ilani ya Uchaguzi.

ACT-Wazalendo walichoshindwa kuelewa ni kuwa pamoja na kwamba wao ndio wanaongoza Manispaa lakini hawana nguvu za mwisho kisheria katika utungaji wa sheria ndogo ndogo na utekelezaji wake lakini kikubwa zaidi waliomba kuchaguliwa ili kuondoa kero na sio kuongeza kero.

Polepole atatoa tamko la kuiamuru serikali izifute sheria hizo mpya kwa sababu ni kero na zinaumiza wafanyabiashara na serikali itakubali huku lawama za kisiasa zitawaangukia ACT-Wazalendo. Huu ni mtaji wa CCM katika Uchaguzi 2019 na 2020 kwenye Udiwani na bunge. ACT-Wazalendo iliyokuwa inaonekana ni mkombozi wa wana Kigoma itajikuta inaonekana ni chama kisichosikiliza kilio cha wananchi na kinaongeza kero.

Hakuna asiyejua kuwa wana Kigoma huwa hawakopeshi kwenye siasa. Hawana tabia ya kumchagua Diwani au Mbunge zaidi ya vipindi viwili ndio maana Zitto alikimbia Jimbo la Kigoma Kaskazini na kwenda Kigoma Mjini.

Takwimu pia zinaonyesha Mkoa wa Kigoma ni moja ya Mikoa ambayo Rais Magufuli anapendwa sana na watu wengi.

Zitto na ACT-Wazalendo wanapambana na msemo wa Waingereza usemao, " If your adversaries are stronger than you, it is better to join their side".
 
Zitto alipomaliza Shule tu alipata zali la kuwa Mbunge!

Muda umefika wa kupumzishwa aende akaitumie taaluma yake ya Uchumi kwenye mambo mengine
 
Zitto alipomaliza Shule tu alipata zali la kuwa Mbunge!

Muda umefika wa kupumzishwa aende akaitumie taaluma yake ya Uchumi kwenye mambo mengine
Nina uhakika mwaka 2020 kuna uwezekano mkubwa wa kupumzishwa.

CCM imeishaanza kujipanga vizuri ili kulichukua Jimbo na kata nyingi za Kigoma Ujiji.
 
Labda ila inaonekana Zitto analong term plan, na kinachomkwamisha kwa sasa ni lebo ya Usaliti na kama sio hiyo lebo leo anageweza kuwa chama mbadala ya CUF na CDM.

All in all bado anafututre kama akiendelea kuwekeza kama afanyavyo sasa, japo namuona anakoma azaidi na wasio wasomi na kusahahu na kuacha wasomi na hapo ni kugombea wanchama na CCM kitu ambacho ni ngumu sana maana CCM wao wana resource nyingi sana za kuweza ku Lobby hawa masikini.
 
Labda ila inaonekana Zitto analong term plan, na kinachomkwamisha kwa sasa ni lebo ya Usaliti na kama sio hiyo lebo leo anageweza kuwa chama mbadala ya CUF na CDM.

All in all bado anafututre kama akiendelea kuwekeza kama afanyavyo sasa, japo namuona anakoma azaidi na wasio wasomi na kusahahu na kuacha wasomi na hapo ni kugombea wanchama na CCM kitu ambacho ni ngumu sana maana CCM wao wana resource nyingi sana za kuweza ku Lobby hawa masikini.

Tatizo lake anataka aonekane statesman wakati chama chake na yeye bado wako kwenye local politics.

Kwa siasa za Tanzania huwezi kushika vyote wakati huna hata resources achilia mbali uzoefu halisi.
 
Tatizo lake anataka aonekane statesman walati yuko kwenye local politics.

Kwa siasa za Tanzania huwezi kushika vyote wakati huna hata resources achilia mbali uzoefu halisi.

Mkuu fafanua zaidi sijakuelewa unaposema STATE man, unamaanisha nini?
Anakosje resource mtu ambaye ni project ya Kitengo?
 
Kama tungekuwa wakweli nadhani tungemsifu na kumtia moyo zitto kwa aina ya siasa anazofanya.SIASA ZA MAENDELEO.Tatizo kubwa nchi hii ni siasa za hila,ghiliba,unafiki na ulaghai.Zitto atabaki kuwa mwanasiasa makini sana tukubali au tukatae.
 
Back
Top Bottom