Je, aachwe aseme tu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Angalizo la Utangulizi
Naianza thread hii kwa angalizo la utangulizi kuwa hii ni thread ya swali!, nimeuliza kitu, na sijatoa statement yoyote hapa!. Nimeanza hivi ili kuweka caveat ya kuzuia mimi kuitwa tena mahali kwa kosa la kuuliza maswali ambayo watu hawayapendi!, kufuatia huko nyuma niliwahi kuuliza swali fulani, ile alama ya kuuliza kwenye swali lile haikuonekana, hivyo nikahesabika nimetoa statement, iliyopelekea mimi kuitwa mahali na kuhojiwa na watu wazito!, hivyo ili kuzuia hilo lisijirudie, naomba kukujulisha kabla kuwa kwenye uzi huu hakuna statements zozote, bali ni maswali tuu, maana unaweza kujikuta unaitwa mahali kuhojiwa kwa nini umetoa statement fulani, wakati wewe hujatoa statement yoyote bali umeuliza tuu swali.

Swali lenyewe ni "Je, aachwe tuu aongee hivyo anavyo ongea, aachwe aendelee kuongea hivyo hivyo kwa sababu hivyo ndivyo alivyo na hiyo ndio ongea yake?. Yaani hizo ndizo kauli zake na hayo ndio maneno yake na hivyo anavyoongea ndio ongea yake na ndivyo anavyozungumzaga siku zote huongea chochote, popote na hizo ndio zake?.

Je inawezekana anaongea hivyo kwa sababu hapo mwanzo hakuwa presidentiale materiale?. Lakini hata kama mwanzo mtu haukuwa presidentiale materiale, ikatokea ukaupata u president kwa kubeeb tuu!, ukiishaupata na kuwa president si ni lazima sasa ubadilike uwe presidential material?, kwa sababu sasa hata tembea yako, unatembea ki presidential!, hata vaa yako, sasa unavaa ki president, hata miwani sasa ni ya ki president!, si mnakumbuka ile dress code yake na zile miwani?.

Mtu ambaye sio presidential material, ukiwa president inakubidi ubadilike uwe ki president president, hata kuongea sasa, lazima ubadilike na uongee ki president!.

Should We Help Out, or Just Sit and Watch?.
Hali yetu kwa sasa ndio hii, na kwa maoni yangu, honestly naona kama kuna tatizo mahali!. Swali kwa sisi wenye uoni kama wa kwangu kuwa kuna tatizo mahali na mtu wetu huyu, tunajiuliza "Jee should we do something to help out or we don't have to do anything to help out, but just to sit and watch kumsubiria aliyemleta ndio afanye kitu?, kwa sababu hata ukisaidia, hataki kusaidiwa! na kuna wenzetu waliojaribu kusaidia wakajikuta.... such that we just have to sit and watch by "Take The Bitter With The Sweet", kwa kunyamaza tuu, au baadhi yetu tujitoe muhanga kwa kuusimamia ukweli, tujitoe na kujitolea kusaidia tuu kwa kuusema ukweli, no matter what, lolote na liwe, tujitokeze, tujitolee, tumwambie ukweli kwa lengo la kumsaidia, au kwa kushauri tuu basi atumie busara hata kama yeye mwenyewe hataki kusaidiwa, na kwa bahati mbaya sana kuna baadhi ya mambo, kunahitajika kiwango fulani cha busara, kuyabaini kwa sababu busara mtu hazaliwi nayo, ni acquired, jee asaidiwe kupata angalau hiyo acquired busara ya kiwango fulani, ili aitumie hiyo busara achague maneno ya busara ya kuongea kwa kuangalia aongee nini na wapi na shughuli gani, walengwa ni nani, na ni ujumbe gani kusudiwa, sio kujiongelea tuu chochote popote?.

Declaration of interest.
"Mimi Paskali, I'm nobody!, kwa vile mimi ni nobody, naweza kusema chochote, popote hata kitu cha hovyo, na kukirudia rudia hadi kuwa "msema chochote" yaani MC, na nisionekane ni mtu wa ajabu, lakini ukiwa somebody, huwezi kusema tuu chochote, popote!, kuna positions fulani fulani, mfano presidential position, huwezi tuu kujisemea chochote popote, ukiwa president, unategemewa kuwa wewe ni presidential material, hivyo hata ukiongea, unaongea ki presidential, na hata ikitokea mtu ambaye sio presidential material, akiukwa u president, then ni lazima mtu huyo abadilike na kuwa ki president president, hata kuongea ni ki presidential.

NB. "Kusema chochote popote sio kosa bali ni busara zaidi kuchagua maneno ya kusema au kutamka kutokana na tukio na mahali kwa kuzingatia the consequences of matamshi yako.
.
Naomba kuanza na angalizo.
Simple Mind Discuss People.
Ordinary Mind Discuss Events
Great Mind Discuss Ideas.

Hatujadili Mtu, Tunajadili Idea ya Kutumia Busara
Hii ni thread kuhusu ideas, naomba sana tusitaje jina la mtu yoyote kwa sababu hatujadili mtu hapa, bali tunajadili matumizi ya kutumia busara kwa kuchagua kwa makini maneno ya kutumia katika kuongea, unaongea nini, unaongea wapi, na unaongea na nani hivyo automatically uchague maneno gani ya kuongea wapi ili kufikisha ujumbe kusudiwa kwa wahusika bila kuwakera, kuwaudhi na kuwaheshimu, hivyo watakupenda, hata ukiwa mkali vipi, ukali wako utapokelewa kwa nia njema na sio unaonekana kila siku wewe ni kugomba tuu!, ukali mwanzo mwisho, sometimes katika hotuba nyingine, sio lazima ugombe na kuzungumza kwa ukali, sometimes, cheka, chekesha, sometimes make jokes, etc, and it is healthy!.
Msema Chochote ni Nani? .
Mtu anayeongea chochote a lolote popote, bila kujali anaongea nini wapi na nani na hivyo atumie maneno gani, huyu ni msema chochote na neno hili hutumiwa kwa ma MC.

Jee ikitokea watu tukabahatika kumpata mtu safi mwenye uwezo wa kunyoosha kila palipopinda, na mwenye nía njema na dhamira safi lakini ni msema chochote, tunafanyaje?. Tumuache tuu aendelee kusema chochote au tumsaidie kubadilika ili achague maneno ya kuzungumza, azungumze nini na wapi na nani?.

Jee Tumwache Tuu Aendelee Kusema Chochote Popote?, au Tumsaidie?.
Jee tumuache tuu aendelee kusema chochote simply because he is the best on what he does, au tumsaidie afundishwe namna ya kuchagua maneno gani azungumze wapi na nani ili kufikisha ujumbe kusudiwa ukiwa sahihi bila kuzusha sintofahamu yoyote?, na ndio maana taifa linamgharimia kuajiri watu mahirI kwa jina la speech writers ili wamshauri, wamuandikie nini cha kusema wapi, na kumuepushia na kusema chochote popote?. Jee sasa hawa watu wanafanya nini?.

Au kwa vile dawa chungu ndio iponyeshayo ugonjwa, Tanzania kama taifa lazima tukiri tunaugonjwa, amepatikana daktari bingwa wa kutibu ugonjwa wetu ila dawa zake chungu kwa kudunga sindano zenye maumivu makali, kutoa vidonge vichungu kumesa na hata kutumbua majipu bila ganzi, tatizo pía ni msema chochote!, hivyo jee tuuchukulie huo usema chochote wake kama ndio tamu ya chungu ya dose yake?, hivyo tuvumilie tuu, tumeze tuu hivi vidonge vichungu na kuvimeza kwa uchungu ili tupone?, ili siku vikija vidonge vitamu baada ya kupona, pia tuvimeze kwa furaha kwa sababu sasa tumepona?.

Sasa ili tupone, do we have to take the bitter with the sweet!, or to choose to take only the sweet na kumeza lakini the bitter tuteme? . Ule msemo wa "wape wape vidonge vyao, wakimeza, wakitema shauri yao" una apply hapa, jee hivi ndio vidonge vyenyewe vichungu tunavyotakiwa kupewa na mtoa dose ameisha toa hiyo dose, vidonge tumepewa, auamuzi wa kumeza au kutema ni shauri yetu au Tanzania ni yetu sote hivyo tunajukumu kusaidia? .
.
JF Has A Duty!.
JF we have a duty of care to help out this situation kwa kusaidia kufundisha how to do the right thing at the right time and do it right ikiwemo namna ya kusema the right thing, at the right time, and to the right people, and how to do it right and how to go about it.

Jee Atafutiwe Waalimu wa Kumfundisha! .
Hakuna binadamu yoyote ambaye ni mkamilifu na anayejua kila kitu, hivyo kitu kama hukijui, hakuna ubaya wowote, wakijitokeza watu wanaojua, wakasaidia kukufundisha na wewe ukajua. Tumeisha gundua na kujua kuwa mtu wetu ni mchapakazi kwel kwel lakini hana busara!, hivyo nauliza, Jee aachwe hivyo hivyo aendelee kuchapa kazi huku akiongea bila busara kwa sababu hana? au watafutiwe waalimu wa somo la busara kujaribu kuingiza busara japo kidogo ndani ya kichwa cha l mtu wetu huyu ili angalau atumie busara japo kidogo kwenye matamshi yake?, au tuendelee tuu kumuacha akisema chochote popote huku akishangiliwa na umati wa watu ilihali anaidhalilisha taasisi ile takatifu?.

Nani wa Kumfundisha na kumsaidia?.
Mwanzo wa mwaka nilishauri humu, jf tukiona tatizo mahali tusiishie kuandika tuu kwa kutaja tatizo au makosa ili tuu watu wajue kuna tatizo, bali tupendekeze na njia za utatuzi, wa tatizo hilo kwa nia ya kujenga (a constructive criticism). 2017 JF Tubadilike, Tupunguze Kuwa "Barking Dogs, Seldom ...

Kwa tatizo hili la Kusema Chochote Tumpatie waalimu Watano.
1. Wasidizi Wake wa Hotuba.

Kwa mujibu wa wadhifa wake, huyu mtu amewekewa wasaidizi wa kumsaidia kwenye kila eneo, kwenye eneo la kusema, ana wasaidizi hotuba, hawa watu wanalipwa kwa kodi zetu na kazi zao ni kumsaidia mtu wetu kwa kumuandikia, aseme nini na wapi. Hawa wamlazimishe kusoma walichomwandalia na kumwandikia kwa kumweleza, hata kama yeye ndie mkubwa kuliko wote, hawezi kujisemea tuu chochote popote!.

Hivyo ili kuepuka kujikwa kwaa ulimi, katika hotuba rasmi, asome alichoandikiwa, halafu ule uhuru wake wa kusema chochote, autumie katika zile hotuba za shughuli zake ambazo kwa awamu hii karibu shughuli zote za pale mahali zinatangazwa live, atumie free flow kwenye impromptu speeches lakini kwenye formal events, asome alichoandikiwa.
2. Yule Mama Anayemmudu.
Huyu mama ni mwalimu wa Grade A, by professional hivyo saikolojia ya kufundishia anaijua, bahati nzuri imetokea she is so humble and down to earth. Kutokana na majukumu yake mapya, imembidi kuiacha kazi yake ya ualimu. Tumchagize, kumshinikiza na kumuomba andelee na kazi yake ya ualimu ila ni kwa mwanafunzi mmoja tuu, tena kwa darasa moja tuu la kwenye kile chumba pale mahali, na kila wakati muafaka baada ya majukumu muafaka ampige somo la ustaarabu na busara yule mwanafunzi mkubwa anayemmudu. Japo huku mtaani anatajwa kuwa ni mbishi ajabu, lakini tukubali tukatae, hakuna mkate mgumu mbele ya chai, hivyo hakuna kiumbe chochote kinachoweza kuleta ubishi mbele ya 'lile somo', hivyo somo la busara liwe ni part & parcel ya 'lile somo', na amini usiamini, somo litamuingia!.

3. Yule Mama Msaidizi.
Hapa ni kujifunza kwa mifano, mbona yule mama msaidizi wake, ni so gentle na so humble? anazungumza kwa heshima, kwa busara na kwa unyenyekevu wa hali ya juu?!. Tumchagize na kumshinikiza huyu Mama Msaidizi, amfundishe bosi wake unyenyekevu, ustahimilivu, ustaarabu, kuwa na subra, kuepuka majivuno, majigambo, ukali uliopitiliza, kuleta utani kwenye mambo ya msingi, kuheshimu misiba ya watu, kuonesha kuguswa na matatizo, majanga na mateso ya watanzania, kutoongea kwa kujisikia kuwa yeye ndio yeye na ndio kila kitu! . Haijalishi anaogofya vipi au watu wananamuogopa vipi bosi wake, yeye ana duty of care kumsaidia kwa sababu ndio right hand man wake (japo female) lazima asaidie kuliko kumuacha bosi wake adhalilike na aidhalilishe hiyo taasisi aliyopo, kama hauwezi kumsaidia bosi wako achague maneno mazuri na yenye busara ya kuzungumza wapi na nani, unakuwa huna msaada wowote kwake zaidi ya kutumwa tuu kwenda kumwakilisha, ukiona kuna maeneo anakosea, mbishie hodi uzungumze nae face to face, nyinyi wawili tuu peke yenu, maana kuna watu wakiwekwa kwenye kona, pamba za masikio zinafumka na busara inawaingia hivyo kubadilika.

4. Kwenye Vile Vikao Vyao.
Kwa vile kila kinachozungumzwa kwenye vile vikao vyao ni siri, then ninaamini kuna mijitu very bold mule inaweza kumkabili na kumsaidia, msikubali mfalme aadhirike kwa kauli za uropokakaji, mna jukumu la kumstahi ili kumsaidia, hiyo taasisi ni tukufu, na hapo mahali ni patakatifu hivyo yampasa mmiliki kuwa mtakatifu na atoe matamshi ya kitakatifu yenye utukufu ndani yake. Mtakatifu hauwezi kuwa msema chochote.
5. JF Tuendelee Kusaidia Kwa Kusema Bila Kuchoka.
JF has proved to be a force to recon with, hivyo kila kinachoandikwa humu, kinafika kunakohusika!. Hivyo sisi jf kwa kutumia haki yetu ya kikatiba ya uhuru wa kujieleza, (freedom of expression), tuendelee kuutumia uhuru huo, kulisaidia taifa letu na viongozi wetu kujitambua, wakifanya makosa tuwakosoe kwa heshma, staha na unyenyekevu, tutoe ushauri kupitia jf, watasikia tuu kama wanavyosikia, japo huko majukwaani huwa hawasemi wala kuitaja jf, lakini kiukweli kabisa, tunasaidia!, hivyo tuendelee kusaidia kwa kusema sana bila woga!.

Hitimisho.
Lengo la uzi huu ni kuichagiza jamii na haswa wahusika waliotajwa humu, kumsaidia mtu wetu ambaye kiukweli kabisa, hakuwa presidential materia, lakini hakuna anayezaliwa presidential material, hivyo asaidiwe kugeuka presidential material kwa kuchunga kauli zake kwa kuchagua maneno ya kusema, hili la kumwacha kuendelea kusema tuu chochote anachojisikia kusema, popote, kuna wakati atakuja kuonekana kama anapayuka au anaropoka, kitu ambacho sii kizuri na sii heshma kwa nafasi ile, kwa sababu baadhi ya kauli hizo hazilisaidii taifa kwa sababu kauli zinaumba!, kuna siku anaweza kutoa kauli zenye madhara makubwa hata kwake mwenyewe bila ya yeye kujijua, matokeo ya kauli hizo zikaumba a bad karma, ikaja ku hit back. When karma hit back, watu watashangalia tuu matokeo ya mapigo ya karma, lakini hakuna atakayejiuliza chanzo ni nini, kumbe ni kauli tuu!.

Kuna siku atakuja kuropoka jambo baya, halafu hilo jambo baya likaja kutokea kweli, hata kama chanzo sio yeye, lakini watu waliomsikia akitamka, wataamini ni yeye tuu anahusika kwa sababu alitamka, na hili likitokea, atakuwa hawezi kukwepa lawama, ataonekana kweli ni yeye!, hivyo sometimes kauli mbaya huumba mabaya na huponza, badala ya kuleta upendo na mshikamano, zinaweza kuleta chuki, utengano, mifarakano na kuibomoa nchi yetu, hivyo kauli njema huumba mema na kauli mbaya huumba uovu.

Tuwasisitize viongozi wetu, kutumia the power of speech, kwa kauli zao kuumba mema kwa kauli njema ili kuleta upendo, amani na mshikamano, ambayo yataleta mafanikio na kuijenga nchi kuendelea kuwa kisiwa cha amani na kielelezo cha mafanikio.

Mwenye masikio na asikie.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
 
Mkuu, nadhani hapo ulimanisha "declaration" of interest na sio "decration" of interest

Back to the topic.Kuna umri mtu ukifia ni vigumu sana kufundishika labda tuombe sana Mungu.

Alafu mbona nasikia kama harufu ya Ben saatisa vile!!
 
Paskali hivi wewe hauna unacho simamia ? Leo unaandika hivi kesho unasema ni dikteta mzuri
Sasa kama ulisema ni dikteta mzuri kinacho kushangaza nini yeye akiropoka ?

Najua upo kama mbayuwayu ili baada ya muda uje hapa kusema oh mimi nilisema
 
Mkuu nahofia utapotezwa... Futa tu hizi thread zako za mashambulizi... Tuliambiwa jk alikuwa na visasi vya vificho huku anakuchekea ila huyu anakupoteza na watu wanajua hajifichi kwani hana unafiki... Be careful...
 
Paskali hivi wewe hauna unacho simamia ? Leo unaandika hivi kesho unasema ni dikteta mzuri
Sasa kama ulisema ni dikteta mzuri kinacho kushangaza nini yeye akiropoka ?

Najua upo kama mbayuwayu ili baada ya muda uje hapa kusema oh mimi nilisema
Huu ndio uzi wa mwisho wa pasco kwa mimi kuchangia , huyu ni mnafiki sana , wakikutana wanasalimiana kwa lugha yao !
 
Pascall Bandiko lako lina mashiko, lakini liko kinyume na angalizo ulilotoa. Naona umeanza kudiscuss watu badala ya Idea. nilitegemea ungejikita kwenye discussion ya 'UROPOKAJI'!

"Angalizo.
Naomba kuanza na angalizo.
Simple Mind Discuss People.
Ordinary Mind Discuss Events
Great Mind Discuss Ideas"
"..Hii ni thread kuhusu ideas, naomba sana tusitaje jina la mtu yoyote kwa sababu hatujadili mtu..." (Pascall Mayalla)
 
Mfalme kalewa ulevi mbaya sana, ulevi wa madaraka ni ulevi mbaya kuwahi kuripotiwa hapa ulimwenguni na wengi walianguka. Huu ulevi unaleta kiburi, unaleta dharau iliyoshiba na unaleta ubwanyenye kwa wanaotawala. Anaweza akafikia mda akaona kuua ni haki yake, kuumiza ni haki yake, kutusi na kukejeri vyote ni haki yake bila kusahau kutesa.

Biblia imeandika tujiadhari sana na 'ulimi'. Ulimi ni kiungo kidogo sana lakini chenye kuweza kuleta maangamizi makubwa, ulimi unaweza kuleta chuki, uhasama na vita. Tumehonywa kuwa makini na kiungo hiki.

Prof. Jay aliwahi kuimba na akatamka maneno haya " bunduki haziui watu bali watu uua watu, na maneno ni tiba huponya na maneno yanaua ". Yawezekana huyu mh. si msomaji na msikilizaji mzuri kwenye mambo haya ama labda huwa hatilii maanani sana ama labda anashindwa kufikia tafsiri nzuri katika mistari hii. Kitendo chake cha kutumia lugha isiyo rasmi katika hafra rasmi kunasababisha tafrani na mauaji, hawapigi risasi watu lakini maneno yake yanapelekea maangamizi. Anaua kwa kuzitesa nafsi za watu, anaua kupitia torturing, anaiangamiza jamii yake.

Nisisitize; vyuo vipo, mentors wapo, matrainers wapo na wasaikolojia wapo pia. Tunawasihi wahusika wa taasisi hii waamke walione hili. Maneno yake si tiba, maneno haya ni vilio na maangamizi kwa jamii.

Bado mda anao wa kubadirika na ni sasa.
 
Paskali hivi wewe hauna unacho simamia ? Leo unaandika hivi kesho unasema ni dikteta mzuri
Sasa kama ulisema ni dikteta mzuri kinacho kushangaza nini yeye akiropoka ?

Najua upo kama mbayuwayu ili baada ya muda uje hapa kusema oh mimi nilisema

...atakwambia hujamuelewa huwa anasema watu hawamuelewagi...

Mie najiuliza, hivi watu wengi wakiwa hawakuelewi, huwa ina 'imply' nini? Je?
1) ni kwasababu hao watu wengi ni wajinga sana na wewe ndio mwerevu kuliko wao au
2) ni kwasababu ujumbe unaoutoa hauleweki, kwasababu kuna 'conflict' ndani ya huo ujumbe na wewe mtoa ujumbe pia uko 'all over the place' kiasi kwamba inakua ngumu kwako kutoa ujumbe uliosimama, no matter how much you try bado unashindwa kueleweka kwasababu ujatulia...?
 
Back
Top Bottom