Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 27,706
- 66,747
Mpo salama!
Watanzania wengi wakikuambia unabusara nenda kajitafakari Sana. Kwani wao wanachanganya Unafiki na Busara.
Wengi wao wakikuambia unabusara Sana tambua wanamaanisha wewe ni Mnafiki Sana.
Hii ni Kwa sababu Watanzania wengi hawaupendi UKWELI. Hawapendi watu wa Moja kwa Moja.
Na mtu asiyependa Ukweli huyo lazima awe Mnafiki.
Watanzania wengi kwa sababu ya unafiki, ku-snichiana, kuzungukana, kufitinishana ni Jambo la kawaida na litegemee
Watanzania wengi wakifanya makosa hawataki uwaambie ukweli Wala hawataki kuwajibika. Hivyo ukinyamaza au kujifanya hujaona au kuwafichia maovu Yao hiyo kwao wataita BUSARA.
Unafiki unaenda sambamba na dhulma. Mtu yeyote Mnafiki lazima awe dhulmati.
Asiyeweza kutenda HAKI.
Mtu anayekataa Ukweli au anayeuogopa UKWELI hawezi kukupa Haki yako.
Usipokee chochote kwa Watu wanafiki kwa sababu kwao Hilo watalitumia kama mikopo na deni unalotakiwa kulilipa kwa kuwa Mnafiki na kutotenda HAKI.
Wanafiki kwao huona ni halali kumsema Mtu Maskini, Tabaka la chini, asiye na cheo akikosea. Hiyo kwao ni BUSARA.
Lakini haohao sio Busara kuusema na kumsema kwa ukweli mtu Mkubwa, mzazi, kiongozi, tajiri, mwenye cheo pale anapokosea. Huo ndio Unafiki wenyewe
Watu wakweli na wenye HAKI unaposimama mbele Yao wewe ni mtu kama watu wengine. Huna ukubwa wowote, huna tofauti yoyote Ile. Ukweli hautaangalia wewe ni Mkubwa au mdogo, maskini au tajiri, kiongozi au Mtumishi,
Kumsaidia mtu hakumfanyi mtu huyo awe Mnafiki.
Kumzaa Mtu haimaanishi awe Mnafiki wako. Yaani umgeuze Mnafiki.
Mfano, Mimi Taikon Master kwa vile nimemzaa Kijana wangu ZERUEL, ati pindi ninapokosea makosa na hakuna WA kuniambia, labda wengine wananiogopa kwa unafiki kwa sababu yoyote Ile labda Mimi ni boss wao, au wananitegemea kwa msaada Fulani ati mwanangu, Zeruel ashindwe kuniambia makosa yangu ati kisa mimi ni Baba yake.
Sisi watibeli hatupo hivyo.
Kama wewe ni Baba jiheshimu. Kama hutaki kuambiwa ukweli wa matakataka yako jizuie usifanye hayo matakataka.
Kama Baba au mama au mzazi ukakosa Busara ya kutenda Mema ukaamua kutenda Mabaya, usitake mtoto awe na busara kukuambia UKWELI.
Ukweli ni sehemu ya Heshima. Mtu asiyeweza kusema ukweli huyo Hana Heshima.
Mtoto asiyeweza kusema Ukweli kwa Baba au mama yake huyo hawezi kusema ukweli kwa Watu back. Huyo ni Mnafiki.
Viongozi wa kisiasa, hamwezi kuwaambia wananchi Ukweli ikiwa mnashindwa kuambiana Ukweli ninyi kwa ninyi. Ninyi ni Wanafiki Wakubwa.
Watu wakweli na wenye HAKI hawana mawe mawili ya kupimia.
Wewe kama huwezi kuusema UKWELI kwa baadhi ya watu. Jua wewe ni Mnafiki Mkubwa.
Kama unasema ukweli wa makosa ya wengine hadharani tena kwa kuwataja Kabisa, ikiwa wewe ni Mkweli huwezi kushindwa kutaja makosa yako MWENYEWE au ya watu wako wa karibu hadharani.
Mtu Mkweli huweza kujikosoa hata yeye mwenyewe. Kukiri makosa yako MWENYEWE ni dalili ya kuwa wewe ni mnyenyekevu.
Haiwezekani Baba ubake watoto wako alafu usiambiwe UKWELI ati utatoa Laana 😂😂 hizo ni hadithi za watu waliogizani. Wajinga, watumwa ambao hawaujui Ukweli.
Ukiona MTOTO WAKO anakuchana UKWELI, labda unatabia ya kunywa mapombe na kutukana hovyohovyo hapo nyumbani kila ukirudi, ujue watu wazima wenzako aidha wameshindwa kukuambia UKWELI au wamekuambia ukweli lakini umekuwa mkaidi.
Sasa ngoja watoto wakukosee heshima kwa sababu si umejivunjia mwenyewe hiyo heshima.
Na hakuna cha Laana wala nini.
Yaani wewe ni kiongozi wa dini alafu unakula wake za watu au unamambo ya kipumbavu alafu viongozi wenzako wanakuonea HAYA (aibu ya Kinafiki) alafu waumini nao kwa vile ni wanafiki wakaa Kimya, akatokea Mtibeli Mmoja akakuchana makavu alafu wewe kiongozi na kundi la wanafiki wenzako mnasema sio Busara sijui usimnyoshee kidole Mtumishi wa mungu, mungu yupi?
Labda hiyo miungu minafiki mnayoiabudu.
Watu Wema, watu wa KWELI, watu wenye HAKI. Hawaoni shida kuambiwa UKWELI ambao wao wenyewe wanaomoyoni mwao.
HAYA!