JB ataoa sababu ya Bongo movie kufa

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,940
19,130
Msanii mkongwe muigizaji wa Bongo movie Jacob Steven JB, ametoa sababu ya bongo movie kudorora kwa sasa. Amedai bado haijafa ila inapitia kipindi cha mpito, na kinachoifanya ikafifia ni kutokana na kufanya movie zinazofanana kila mara na watazamaji kuzizoea na kuona haina jipya.

Ametolea mfano kipindi cha uchekeshaji cha Komedi kilivyoanza na watu wakawa wanajazana kwenye TV kutazama lakini baada ya kuzoeleka wakaipotezea na hata Nigeria movie zao zilikuwa zinapendwa sana lakini nao wana tatizo kama la Bongo
Amedai haitakufa ila watakuja wasanii wapya na kiufanya tofauiti.

Jamaa katulia na kuzungumza ukweli kabisa hii kama jukwaa au jiwe la kukanyagia ili mtu afike juu
 
Bongo muvi ilianza kufa walipoanza kuamini kuwa kila msichana mwenye sura nzuri anaweza kuigiza,kilichofuata ni magwiji kama Monalisa,Johari,Waridi kupotea taratibu na kuwaachia 'ngonomuvi' kuongoza jahazi.
Kabis yaan ni hiyo ngono movie
 
Zitaachaje kufa wakati mnatudanganya kama watoto wadogo. Msanii wa kike anavaa nywele mwanzo wa muvi hadi mwisho hizo hizo, au maiti ina hema. Hebu tupia moja na wewe.
 
bongo movie walio wengi hasa dadaz wanatumia Tv kutangaza biashara zao za ngono huu ndio ukweli,sasa hivi vigogo wamedhibitiwa hawali sana uroda na wao wamedorora,hii ni sababu ya kwnza ya pili ni kuibuka kwa filamu za kihindi zinazouzwa mtaani kama njugu tena kwa bei nafuu na zina kiwango kikubwa ukilinganisha na za bongo movie zamani tulikuwa tunabebana tuu ila kulikuwa hakuna ufanisi mkubwa sana katika kuigiza
 
Bongo movie ilikufa walipomchagua steve nyerere kuwa mwenyekiti,jamaa alicheza kama messi au c ronaldo(huku anakuwadia wadada huku anawapeleka kwenye siasa) lazima wapotee
 
Bongo movie imekufa sababu haiwaangalii watu wenye vipaji asilia vya kuigiza, yaani watu wabunifu. Bongo movie ilianza kufa mlipoanza kuangalia matako, mahips na sura kama kigezo cha kuwa muigizaji bora na ndio maana Sanaa yenu kwa kipindi hiki imekuwa kimbilio la malaya, huku mkiwaacha waigizaji wenye vipaji vya ukweli kisa hawana mwonekano na sasa hivi upande wa wanaume wamejaa mashombeshombe na wauma lips kuigiza hawajui, sanaa mmeiuwa wenyewe. Mimi huwa najiuliza hivi mtu kama LUPITA NYONGO angezaliwa Tanzania kweli angepewa nafasi ya kuigiza ktk hizi movie zetu za bongo, sasa muangalie huko Hollywood LUPITA sasa hivi anavyokimbiza, badilikeni angalieni vipaji na si mwonekano la sivyo mtaendelea kufeli.
 
Bongo movie hakuna kitu kabisa ila nitoe pongezi kwa waliofanya SIRI YA MTUNGI walijitahidi sana mastaa wenye majina makubwa walikuwa wachache,story na ujumbe ulieleweka,sauti na picha ni HD kabisa walifanya vizuri.
Mkuu, usichanganye SIRI YA MTUNGI na huo upuuzi unaoitwa Bongo Movie. Siri ya mtungi ilitengenezwa na jamaa waliotengeneza "yellow card" na "Neria". Kama unazijua hizo movie utakuwa umenielewa.
 
Always mshika mawili moja humponyoka, kinachowaponza wasanii wetu mambo mengi, siasa wao, skendo zao. Nawashauri wakienda Dodoma waende na cd/dvd zao wakawauzie wanachama wenzao.
 
Bongo movie imekufa sababu haiwaangalii watu wenye vipaji asilia vya kuigiza, yaani watu wabunifu. Bongo movie ilianza kufa mlipoanza kuangalia matako, mahips na sura kama kigezo cha kuwa muigizaji bora na ndio maana Sanaa yenu kwa kipindi hiki imekuwa kimbilio la malaya, huku mkiwaacha waigizaji wenye vipaji vya ukweli kisa hawana mwonekano na sasa hivi upande wa wanaume wamejaa mashombeshombe na wauma lips kuigiza hawajui, sanaa mmeiuwa wenyewe. Mimi huwa najiuliza hivi mtu kama LUPITA NYONGO angezaliwa Tanzania kweli angepewa nafasi ya kuigiza ktk hizi movie zetu za bongo, sasa muangalie huko Hollywood LUPITA sasa hivi anavyokimbiza, badilikeni angalieni vipaji na si mwonekano la sivyo mtaendelea kufeli.
Umetoa mchango mubashara kabisa
 
Back
Top Bottom