Jasusi wa Rwanda akamatwa DR Congo, yupo jela sasa

Moronight walker

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
3,105
4,635
Anaitwa Fortunat Biselele
Alikuwa ni mshauri wa Rais wa Congo bwana Felix.

screen-shot-2023-01-15-at-163610-1256x628-1675263398.png

Fortunat Biselele alikuwa inner circle ndani ya serikali ya Congo.
Alikuwa anamshauri wa rais Felix kwa mambo MENGI.
Walimgundua kwa kupeleka siri za maongezi ya Serikali ya Congo na kwenda kwa PK.
Na walipopekua nyumbani kwake walimkuta ana hati ya kusafiria ya Rwanda.
Na walimkuta na document za hati za nyumba za Rwanda.
Hio ilionesha kuwa anamiliki nyumba baadhi Rwanda.

BISELELE-9.jpg

Kwa sasa yupo jela mjini Kinshasa

Video ikionyesha alivyokamatwa
👇
 
Huyu nadhani ni wa pili,mwaka jana pia walikamata jasusi, Tshisekedi akianzisha vita bila kuwa makini atauliwa akiwa Ikulu
Na NDOMAANA yupo kimya , mimi nawaambia watu ,congo sio rahisi kuanzisha vita na rwanda coz wanajijua wenyewe madhifu yao.
Kumbuka kuna Banyamulenge kule hata serikali wengi tuu.
 
avunje baraza lote la mawaziri amtoe Waziri wa Madini, Gavana kivu na Goma na aunde upya jeshi lake na avunje idara yake ya ujasusi aazime nchi rafiki wa damu TZ
Sio rahisi hivyo hasa kwenye kuvunja jeshi huoni wengi watarejea msituni ?..... isitoshe uchaguzi haupo mbali sana hivyo muda haupo upande wake.
 
avunje baraza lote la mawaziri amtoe Waziri wa Madini, Gavana kivu na Goma na aunde upya jeshi lake na avunje idara yake ya ujasusi aazime nchi rafiki wa damu TZ
Hivyo vitu vyote hawezi fanya kwani vitaharibu zaidi kuliko kujenga.
Akivunja jeshi hao wanajeshi wa sasa waende wapi, haijawahi tokea nchi yoyote ikavunja jeshi. Unabadili staff na maofisa tu napo ni baadhi.

Akivunja baraza la mawaziri anatengeneza destabilisation ya nchi na serikali itakayokuja itakuwa ngumu. Achomoe mawaziri wanafiki na magavana wao huwa na nguvu itakuwa ngumu kuwatoa kama wana back up.

Idara ya ujasusi akiivunja ni yaleyale ya jeshi. Hapo ni kuchomoa moles na double agents.

Btw Felix sio smart kivile. Nimeshakata tamaa juu yake hakuna maajabu atafanya
 
sawa, lakini idarani kwake daah jamaa kajua sana kuchafua
 
sawa, lakini idarani kwake daah jamaa kajua sana kuchafua
Congo inahitaji mtu kama Abiy Ahmed wa Ethiopia
Abiy_Ahmed_at_the_African_Union_2018.jpg
Unajua nchi zetu hizi za Afrika ni ngumu kupata sampuli kama yake. Viongozi waandamizi huchaguliwa wenye uwezo mdogo au wa wastani wasimzidi Rais, ikitokea kiongozi mwandamizi ana uwezo zaidi anaonekana tishio au kiherehere. Ndio yale ya Mrema akiwa Internal Minister anamzidi Mwinyi kuogopwa na kufanya maamuzi magumu.

Sasa Felix Tshisekedi kabebwa kwa kiasi kidogo na baba yake, Etiene. Etiene alikaa serikalini na kuwa Waziri Mkuu mara tatu na kabla alikuwa mpinzani tangu enzi za Mobutu. Etiene aliijua vizuri serikali, Felix alikijua chama chake sio serikali. Felix ndio Rais wa Congo kuchaguliwa kwa halali tangu wapate uhuru, chaguzi nyingine kunakuwepo na compromise, ingawa hata yeye kulikuwa na factions na inasemekana hakushinda uchaguzi ila alisaidiwa na team Kabila (kuliko Rais awe Martin Fayulu ambaye ni hardliner, bora awe Felix hana shida). Na kanisa inasemekana lilimtaka Felix. Bahati nzuri waliyokuwa nayo Congo ndio hii tu sidhani kama in near future wataipata.

Tofauti na Congo, pale Ethiopia Abiy Ahmed alikuwa mkuu wa usalama wa taifa kabla ya kuwa kiongozi wa nchi. Alipokuja alianza reforms mwaka uleule maana akitokea serikalini hivyo hakuanza kujifunza. Akapata na Nobel Peace Prize ila baadae akaona mageuzi aliyofanya yanamgeuka, mfano aliwafungulia maelfu ya wafungwa wa kisiasa ili nchi ipate reconciliation ila yale mafungwa yalipofunguliwa yakaanza chokochoko za kikabila tena.
Akaona sasa huu ujinga akaanza kuwaua na kuwaondoa kwenye nyadhifa nyeti za serikali wale wapuuzi. Pale Ethiopia kuna ukabila mkubwa sana ila Abiy amechanganya damu ya makabila mawili makuu na hasimu (hii ilimpa point kuwa mkuu wa nchi), ila bado makabila hayo kila moja linataka alipendelee. Mwishoni ikatokea vita kali Tigray na imeua watu wengi. Ethiopia ingejichanganya ikachagua mzembe tofauti na yeye sasahivi tungekuwa na Eritrea kama mbili za ziada. Na bahati yao wameitumia vizuri, kiongozi kijana in his 40s, katoka serikalini kidogo na ni smart hajabebwa.

Naona nchi nyingi huongozwa na vilaza, na sina imani na viongozi wazee kuanzia 65+ uko kwa nchi zetu zenye shida hizi. Na siamini kwenye viongozi waliokulia serikalini miaka zaidi ya 30 huwa hawana akili ila hawajui tu, hawana mawazo mapya. Na bado siamini mkuu wa nchi kutokea nje ya serikali kabisa kabisa yaani hajawahi ongoza hata mkoa au katoka jeshi. Huyo atapoteza miaka kujifunza kwanza au hatokuwa na busara au shida yoyote nyingine. Pale Marekani tumemuona Trump mfanyabiashara aliyeibukia Urais, ila sio lazima iwe hivyo maana Zelensky pale Ukraine kaonyesha ukomavu.
 
Congo inahitaji mtu kama Abiy Ahmed wa EthiopiaView attachment 2504230 Unajua nchi zetu hizi za Afrika ni ngumu kupata sampuli kama yake. Viongozi waandamizi huchaguliwa wenye uwezo mdogo au wa wastani wasimzidi Rais, ikitokea kiongozi mwandamizi ana uwezo zaidi anaonekana tishio au kiherehere. Ndio yale ya Mrema akiwa Internal Minister anamzidi Mwinyi kuogopwa na kufanya maamuzi magumu.

Sasa Felix Tshisekedi kabebwa kwa kiasi kidogo na baba yake, Etiene. Etiene alikaa serikalini na kuwa Waziri Mkuu mara tatu na kabla alikuwa mpinzani tangu enzi za Mobutu. Etiene aliijua vizuri serikali, Felix alikijua chama chake sio serikali. Felix ndio Rais wa Congo kuchaguliwa kwa halali tangu wapate uhuru, chaguzi nyingine kunakuwepo na compromise, ingawa hata yeye kulikuwa na factions na inasemekana hakushinda uchaguzi ila alisaidiwa na team Kabila (kuliko Rais awe Martin Fayulu ambaye ni hardliner, bora awe Felix hana shida). Na kanisa inasemekana lilimtaka Felix. Bahati nzuri waliyokuwa nayo Congo ndio hii tu sidhani kama future wataipata.

Tofauti na Congo, pale Ethiopia Abiy Ahmed alikuwa mkuu wa usalama wa taifa kabla ya kuwa kiongozi wa nchi. Alipokuja alianza reforms mwaka uleule maana akitokea serikalini hivyo hakuanza kujifunza. Akapata na Nobel Peace Prize ila baadae akaona mageuzi aliyofanya yanamgeuka, mfano aliwafungulia maelfu ya wafungwa wa kisiasa ili nchi ipate reconciliation ila yale mafungwa yalipofunguliwa yakaanza chokochoko za kikabila tena.
Akaona sasa huu ujinga akaanza kuwaua na kuwaondoa kwenye nyadhifa nyeti za serikali wale wapuuzi. Pale Ethiopia kuna ukabila mkubwa sana ila Abiy amechanganya damu ya makabila mawili makuu na hasimu (hii ilimpa point kuwa mkuu wa nchi), ila bado makabila hayo kila moja linataka alipendelee. Mwishoni ikatokea vita kali Tigray na imeua watu wengi. Ethiopia ingejichanganya ikachagua mzembe tofauti na yeye sasahivi tungekuwa na Eritrea kama mbili za ziada. Na bahati yao wameitumia vizuri, kiongozi kijana in his 40s, katoka serikalini kidogo na ni smart hajabebwa.

Naona nchi nyingi huongozwa na vilaza, na sina imani na viongozi wazee kuanzia 65+ uko kwa nchi zetu zenye shida hizi. Na siamini kwenye viongozi waliokulia serikalini miaka zaidi ya 30 huwa hawana akili ila hawajui tu, hawana mawazo mapya. Na bado siamini mkuu wa nchi kutokea nje ya serikali kabisa kabisa yaani hajawahi ongoza hata mkoa au katoka jeshi. Huyo atapoteza miaka kujifunza kwanza au hatokuwa na busara au shida yoyote nyingine. Pale Marekani tumemuona Trump mfanyabiashara aliyeibukia Urais, ila sio lazima iwe hivyo maana Zelensky pale Ukraine kaonyesha ukomavu.
NI kweli Congo walitengenezewa usaliti maka mingi mno hata Mkuu wao wa Usalama haaminiki pamoja na kuchujwa sana macho yake na masikio havilingani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom