Jaribu haya maisha, Utaona matokeo mazuri

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Najua kuna baadhi ya watu watahoji sana lakini huu ndio ukweli wenyewe.

1. Ili uwe tajiri, Toa

2. Ili ufanikiwe, Tumika

3. Ili ucheke, Mfanye mwingine acheke

4. Ili ustawi, Kuwa mwaminifu

5. Ili ufike mbali, Amka mapema

6. Ili umbadilishe mtu, Badilika wewe Kwanza

7. Ili uwe mkuu, Kuwa mwanafunzi kwanza

8. Ili uwe na nguvu, Omba sana

9. Ili ufanye mambo mengi, Ongea machache

10. Ili uishi vizuri, Samehe wanaokukosea

11. Ili uongee vizuri, Zuia hasira

12. Ili upendwe, Penda

13. Ili uheshimiwe, Kuwa mpole

14. Ili umfunge na kumkemea shetani, Jitakase kaa mbali na Dhambi

15. Ili ukuwe katika imani, Tafakari maneno yake mchana na usiku.
 
Ongeza hii:

16. Ili Tanzania i jinasue na janga hili la Corona, jiwe na awajibishwe.

NB: Kuwajibishwa ni kutakiwa kuzingatia misingi kamili ya utendaji kazi kwa mujibu wa taratibu au katiba kwa mustakabala wake.

Au nasema uongo ndugu zangu.
 
Una mapepo ndio yanayo kusumbua sio wewe unayeandika ni mapepo yaliyomo ndani yako.
 
Una mapepo ndio yanayo kusumbua sio wewe unayeandika ni mapepo yaliyomo ndani yako.

Kama nina mapepo yanayowakemea nyie kwenye harakati zenu za kuuwa watu, mapepo hayo ni mbona ni mazuri sana?

IMG_20210220_143229_708.jpg

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom