Japokuwa simkubali Ndugai, lakini katika hili ameonewa na kudhalilishwa isivyo sahihi na Rais

Ngoja niweke ushabiki na chuki zangu pembeni dhidi ya Ndugai, katika hili la sasa la Rais Samia kumfokea, kumdhihaki, kumbeza, kumnanga na kumzodoa hadharani Spika wa bunge la Tanzania, Job Ndugai binafsi ninaona sio haki, sio uungwana na sio heshima.

Spika Ndugai ameonewa na kudhalilishwa kisiasa isivyo halali. Kihisia Ndugai kwa sasa ni kama amekatwa mikono na miguu, akafungwa mdomo wake na mwisho akapondwa pondwa moyo wake. Kisaikolojia mtu wa namna hii ndani yake hujaa fikra nzito za visasi dhidi yake au watetesi wake, kuna kila dalili mtu wa namna hii kuja kufanya maamuzi ya hatari mnoo kwa kuwa ni muasi wa kifikra, tena fikra zake mwenyewe!

Katika mazingira ambayo, mwanaume mbabe mtu mzima wa kiafrika kama Ndugai, mwenye nafasi ya juu sana kisiasa kama Ndugai kuja hadharani na kuomba msamaha mbele ya Rais wa nchi mwenye jinsia ya kike, basi ilitosha kabisa kulinda heshima na utu wake kwenye jamii kwa kujizuia kusema chochote juu yake. Mtu akishasema nimekosa na ninaomba msamaha, basi mambo yote huishia hapo na hakuna sababu ya kuyafufua mengine.

Maneno aliyoyatumia Ndugai wakati akiomba radhi ni maneno yanayotumika pia kwa waumini (hususani wakatoliki )wakati wa kufanya toba mbele ya Mungu wao na hubakia sirini mwao ni kipi hukiombea msamaha, toba hiyo inapobezwa na kuanikwa hadharani ni fedheha kwa muumini kiasi hata cha kutamani kuasi imani yake milele.

Simkubali kabisa Ndugai kisiasa na kijamii, sipendi kabisa hulka yake ya kisiasa na kijamii, karibu siku zote ninamuona kama ni mtu roho mbaya, husuda na uongo, ni adui namba moja kwangu kisiasa baada ya Magufuli, lakini katika hili la sasa nampa pole, namtetea na kumuonea huruma kama binadamu mwingine yoyote anayehitaji kuheshimiwa na kulindwa utu wake.
Umenena vizuri tena kiungwana lakini usisahau dini zingine zinaruhusu kisasi tena wanasema ni halali. Ndugai hakuwa na sababu ya kuomba radhi kama alivyofanya Profesa Mkenda yupo tayari kwa lolote natumaini baraza jipya la mawaziri hatakuwemo kwani mama ni mtu wa visasi mtu wa majigambo mtu wa mipasho na yeye Mungu amembariki kwani anajua kila kitu.
 
Ngoja niweke ushabiki na chuki zangu pembeni dhidi ya Ndugai, katika hili la sasa la Rais Samia kumfokea, kumdhihaki, kumbeza, kumnanga na kumzodoa hadharani Spika wa bunge la Tanzania, Job Ndugai binafsi ninaona sio haki, sio uungwana na sio heshima.

Spika Ndugai ameonewa na kudhalilishwa kisiasa isivyo halali. Kihisia Ndugai kwa sasa ni kama amekatwa mikono na miguu, akafungwa mdomo wake na mwisho akapondwa pondwa moyo wake. Kisaikolojia mtu wa namna hii ndani yake hujaa fikra nzito za visasi dhidi yake au watetesi wake, kuna kila dalili mtu wa namna hii kuja kufanya maamuzi ya hatari mnoo kwa kuwa ni muasi wa kifikra, tena fikra zake mwenyewe!

Katika mazingira ambayo, mwanaume mbabe mtu mzima wa kiafrika kama Ndugai, mwenye nafasi ya juu sana kisiasa kama Ndugai kuja hadharani na kuomba msamaha mbele ya Rais wa nchi mwenye jinsia ya kike, basi ilitosha kabisa kulinda heshima na utu wake kwenye jamii kwa kujizuia kusema chochote juu yake. Mtu akishasema nimekosa na ninaomba msamaha, basi mambo yote huishia hapo na hakuna sababu ya kuyafufua mengine.

Maneno aliyoyatumia Ndugai wakati akiomba radhi ni maneno yanayotumika pia kwa waumini (hususani wakatoliki )wakati wa kufanya toba mbele ya Mungu wao na hubakia sirini mwao ni kipi hukiombea msamaha, toba hiyo inapobezwa na kuanikwa hadharani ni fedheha kwa muumini kiasi hata cha kutamani kuasi imani yake milele.

Simkubali kabisa Ndugai kisiasa na kijamii, sipendi kabisa hulka yake ya kisiasa na kijamii, karibu siku zote ninamuona kama ni mtu roho mbaya, husuda na uongo, ni adui namba moja kwangu kisiasa baada ya Magufuli, lakini katika hili la sasa nampa pole, namtetea na kumuonea huruma kama binadamu mwingine yoyote anayehitaji kuheshimiwa na kulindwa utu wake.
Ndugai hakuomba radhi kwani kosa lake pia hajalijua. 1. Anaposema KAMA kuna mtu nimemkwanza.. maana yake haelewi alipokosea. 2. Hakuishia hapo aliendelea kuisingizia mitandao kuwa ndiyo imesababisha kutafsiriwa tofauti. 3. Aliyakiwa moja kwa moja kukiri kweli nimemkosea rais na wananchi naomba wanisamehe.
 
Back
Top Bottom