Wanabodi,
Mara kwa mara Dr. Hamisi Kigwangala amekuwa akilamiwa mara kwa mara na kushutumiwa, leo ndia nimeanza kumkubali, kiukweli huyu jamaa ni kichwa maji kweli kweli!, yaani kichwani ni mtupu mweupe kabisa katika masuala ya katiba, labda kwenye udakitari!. Kama uelewa wake wa jambo dogo simple kama hili ameshindwa kulielewa, Dr. huyu aliwezaje, kupata udakitari?!.
Issue yenyewe ya ukichwa maji wa Dr. Kigwa, Lissu amezungumzia siku ya kusainiwa Mkataba wa Muungano kule Zanzibar, tarehe 22/04/1964 na ratification iliyofanywa na bunge la Tanganyika tarehe 25/04/1969.
Mkataba wa Muungano ni kitu kimoja na sheria ya muungano ni kitu kingine!. Lisu amewataja waliokuwepo siku ya kusaini mkataba!, Kingwa anawataja waliokuwepo siku ya ratification na kudai Lissu ni mpotoshaji!.
Pasco
Pasco, ndio siasa zao hizo! mbunge anaomba kuchangia bungeni baada ya kupata maneno aliyoyatoa mwenzie na anatumia dakika kumi kujibu, kukejeli alichosema mwenzie ili mradi asikike kuwa amechangia. Mbaya zaidi voters wetu huwa wanampigia kura mgombea aliyewapa kofia kanga na Tshirt sio mwenye uwezo wa ku-address issues zao vilivyo