January kwangu iko tofauti sana. Hapa nilipo nasubiri kujikamatia kitika changu cha dola 9,000 za Kimarekani. Mambo ya tax return hayo. IRS imeanza kupokea returns jana tarehe 17 na mimi nime file returns zangu jana hiyo hiyo.
Tarehe 27 ndo watazitumbukiza hela kwenye akaunti yangu! Halafu pia kuna state returns. Dola 1700 zitatumbukizwa kwenye akaunti yangu Ijumaa hii, tarehe 20.
Kwa hiyo Januari kwangu ni mwezi wa neema sana.
AAhh mie hawa washenzi hawajaniletea W2 forms zangu bana aaagrr!.
umenikumbusha aisee
nimeona hata wakenya wana tax returns
nikawa najiuliza bongo haya mambo vipi na lini??????
January kwa wafanya biashara mwanzo wa weeks unaenda lipa mapato pale TRA, Kama mmiliki wa magairi jiandae mambo lukuki kama TRA, mara sticker za usalama wa barabarani, mara Bima, mara ukaguzi mgogo mdogo na Sumatra na mambo kibao! Vivo hivo kama una vianzo vingine vya biashara... Kwa watu ambao tuna familia na responsibilities ni wakati wa kulipa ada za watoto, kuandaa sare na facilities zote ambazo zahitajika, ukiwa na watoto wawili tu nazaidi na ada sio chini ya Laki kadhaa ama M' or M kadhaa, kijasho kinakutoka. Kinakutoka na wasema next time I will prepare myself sooner lakini bado tu wachemka! lol
but hii ina maana wananchi wanaumizwa mno....
maana hata Kenya tu wameshashtuka....
ukiacha wenye tax returns naona unaomba jamvi msibani lol
duh, hali inatofautiana.
Inawezekana nyie mna majonzi
mie nimening'inizwa kabisa.
Wasiwasi wangu ni mafisadi kupata mianya mingine ya kuwafisadi wananchi!
Na pia ni bora na kuanza kujenga infrastructure kwanza ambayo italifanya zoezi zima liende vizuri. Sasa hivi hata sort of national ID wananchi hawana...au nimekosea?