January Makamba: Waliozaliwa kabla ya 1961 waachane na wazo la Urais 2015!

Niliwahi kusema Zitto na January wanaousaka urais kirahisi watatuingiza matatizoni.2wakatae hawa kula kulala.
 
January kawachana kina Lowassa,Membe na wengineo kuwa wote waliozaliwa kabla ya 1961 waachane na mawazo ya Urais maana watatupotezea muda ...tunahitaji rais wa dot.com atakayeendana na changamoto za leo

If the poor little political rookie deems he has what it takes let him jump into the fray and compete fair and square, why this tactical eleimination; January go beat them at the ballot box not from the political platform!!
 
Ukiingia Ofisi za Wizara ya Sayansi na Teknolojia pale Mtaa wa Jamhuri unaweza kufikiri labda umeingia Ofisi za TFF...! And yet huyu bwana mdogo ana ndoto za kuwa Rais...! St***d
 
Hivi Makamba katokea wap? mpaka atoe kauli kama hiyo kama siyo kubebwa na baba zake na shemeji yake RA, Ingawa sio chadema lkn ZIto alipotokea na Consistency yake ktk jimbo ni uwezo tosha wa yeye ni Mwanasiasa wa aina gani, Vijana wote walio ndani ya CCM wamewekwa pale majina ya baba zao au mama zao sasa wanataka tuwape nchi kwa mgongo wa Ujana Watanganyika tutakuwa tumekwishaaaaaaaaaaaa!

Busara zao ni ziro NCHI sio kampuni waongoze miradi ya baba zao kwanza kuwapa ajira watanganyika wengine siyo Taifa letu. Hili siyo taifa la MAISHA PLUS mshiriki atafutwi kijijini bali Kiongozi Uibuka miongon mwa Viongozi wengine ndani ya CCM hakuna hata Mmoja wote ni sehemu ya makundi
 
muasisi ni @Zito kabwe hakika kila siku napingana na wanajamvi humu wanaowasapoti hawa vijana wawili ambao kwangu nawaona mambo yao ni sawa na kikweete
 
Katika kongamano lililofanyika Nkrumah Hall UDSM jana tarehe 9 -12- 2012 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika huyu bwana akiwa kama moja ya wachokoza mada alimalizia mchango wake kwa msisitizo kuwa mtanzania aliyezaliwa kabla ya 1961 hawafai kuchaguliwa katika nafasi ya urais 2015. Binafsi nilishangazwa na kauli hii lakini kwa kuwa simfahamu vizuri huyu ndugu nashinwa kupata tafsiri ya kauli hii. Wana JF mnaomfahamu huyu mheshimiwa nisaidieni kunipa tafsiri. Nawasilisha.
 
muasisi ni @Zito kabwe hakika kila siku napingana na wanajamvi humu wanaowasapoti hawa vijana wawili ambao kwangu nawaona mambo yao ni sawa na kikweete

Unataka kususewa JM anatumia akili za Zitto.? Umesahau jk aliingiaje madarakani kwa staili gani.?
 
Last edited by a moderator:
Ngoma yake na Zitto inachekesha, wamepania kupeana tafu, kuwa atakayepata atajenga seriklai ya mseto. this stupid tritiny(Zitto,Jussa, January). funny enough ni watoto wa madrassa waliongia elimu dunia kwa fujo.
 
Hii ni hoja nyepesi sana ina maana waliozaliwa kabla ya uhuru hawatakiwi kuwa viongozi hebu tumsimamishe salim na makamba utamchangua nani?

Lakini ni vijana hawa hawa kila siku wanaiba bandarini,TRA,bank hivi mnataka kuniambia kati ya wazee nani wanapiga ishu za hela za wizi kila siku.

Niweke wazi hiki kizazi mnachokipingia kelele cha vijana ni cha mbwa kabisa tuchague kiongozi kwa uzalendo wake na uwezo wake sio umri wake.
 
wanaotaka uongozi kwa njia rahisi ndio huleta siasa za kuwatenga wengine, iwe kwa umri, dini au sehemu mtu anapotoka

Umenena Mkuu. Unanikumbusha machungu ya kampeni za 2010, zilizoratibiwa na CCM dhidi ya Dr Slaa ambazo madhira yake tumeanza kuyaona. Wanachowaza wanasiasa, hasa wa CCM ni kutawala tu, hawafikirii hatima yetu kesho, watoto wetu tutawaachia nchi ya namna gani.
 
Amesema na amesikika, hayo ni mawazo yake binafsi. Ila asipuuzwe kwa aliyoyasema.
 
January kawachana kina Lowassa,Membe na wengineo kuwa wote waliozaliwa kabla ya 1961 waachane na mawazo ya Urais maana watatupotezea muda ...tunahitaji rais wa dot.com atakayeendana na changamoto za leo

URAISi hauna kozi kwamba mitaala imebadilika! Ndg yangu JM fuata ushauri wa J Butiku utafanikiwa na sio sera ya ubaguzi unayotaka kutoka nayo. Nashauri sana usiingie kwenye mawazo kama ya wataka madaraka kwa sera za ubaguzi wa uzee na ujana. Jiulize nyumba inaweza kujengwa bila msingi? pigania vijana wengi wahusishwe katika mipango na kazi mbalimbali za maendeleo ya taifa ili kupata uzoefu wa kiungozi na kufahamu vizuri sera za nchi ili baadaye waje kuchukua huo URAIS.
 
Tunahitaji ueledi katika urais na si ujana.
Akina Makamba na Zitto waondoe mataputapu yao.
 
Last edited by a moderator:
Ngoma yake na Zitto inachekesha, wamepania kupeana tafu, kuwa atakayepata atajenga seriklai ya mseto. this stupid tritiny(Zitto,Jussa, January). funny enough ni watoto wa madrassa waliongia elimu dunia kwa fujo.

ALSHAABAB wale

 
Nilipozaliwa miaka hiyo taarifa ya habari iliongozwa na ngoma za Mzee Moris Nyunyusa akiwa anapiga ngoma 7. Kisha zinafuata; "nyot!, nyot!, nyot!, nyot!, nyot!, nyot!," Kisha wasomamaji; mmoja anataja muda (Eda Sanga: Hivi sasa ni saa 1 kamili) David Wakati anaitikia; "Na hii ni taarifa ya habari kutoka Radio Tanzania Dar es Salaam, Msomaji David Wakati, kwanza muhtasari wa habari.


1. "Waziri asiye na wizari maalum Bw Kingunge Ngombale Mwiru............"

2. "Waziri wa nchi ofisi ya Makamo (siyo Makamu) Bw Steven Meng'anyi Wassira leo ametembelea nyumbani kwa Mtukufu Rais Julius Kambarage Nyerere, huko Butiama..........."

Habari kamili, Dar es Salaam....


Basi majina hayo yametajwa hadi sasa tumekuwa wakubwa na sasa tunaelekea kuchungilia nusu karne lakini wapo tu. Wapo tu mpaka MENO YAO YA ASILI YAMETANGULIA MBELE YA HAKI WENYEWE WAPO TU. SASA HIVI HATA CHAI YA MOTO HAWAWEZI KUNYWA KWA SABABU HAWANA MENO ZIMEBAKI FIZI WANAKUNYWA CHAI BARIDI KAMA MTINDO (FASHION) KWA KUOGOPA KUUNGUA FIZI ZAO WAPO TU...

JAMANI PUMZIKENI SASA....... HAMNA JIPYA MTAKALOTUACHIA TUACHIENI NCHI TUANZE KUIKARABATI UPYA KAMA ALIVYOFANYA MWL NYERERE 1950S.

ASANTENI JAMANI.......!!!!!!???????
A%20S%20thumbs_up.gif
:horn:


Edit Post Reply Reply With Quote

 
January kawachana kina Lowassa,Membe na wengineo kuwa wote waliozaliwa kabla ya 1961 waachane na mawazo ya Urais maana watatupotezea muda ...tunahitaji rais wa dot.com atakayeendana na changamoto za leo

mimi nimezaliwa kabla ya uhuru lakini ninaunga mkono hoja ya Januari. hawa wanao jinadi hovyo hovyo wakionyesha nia zao kuutaka urais wa Tanzania na wengine wenye mawazo kama hayo ambayo hawaja yaweka wazi, wote hawafai! nadhani nchi hii ikipata kijana mwenye mawazo ya kisasa ya kuijenga nchi hii kiuchumi, kijamii na kisiasa tuta vuka janga hili la umaskini wa kutupa lililo tutafuna toka tupate uhuru. lakini lazima tuwe macho tupate kijana mwenye mawazo na mtizamo mpya wa kileo maana wako vijana wengi ndani ya mfumo serikali ya sasa wenye mawazo na mtizamo wa kizamani. Yaani tungeweza kumpata Mh. Januari, naamini hatungeyajutia maamuzi yetu.
 
Da kwa sie wote vijana hii ni aibu, kwa kuwa msemaje January Makamba [JM] na rafiki yake wa agenda Zitto Zuberi Kabwe [ZZK] hakika wanatuaibisha vijana.

Hii mada yake yake UDSM, inahitimisha kile ambacho siku za nyuma mshirika wake wa agenda ZZK alianzisha humu ndani ya Jamvi lakini kwa busara ya wanajamvi walimkaria kooni na atimae akajipumzisha na purukushani za kuimarisha agenda yake humu ndani ya jamvi.Ilifikia hatua ya kutaka kuharibu baadhi ya vjana ambao wanaonekana kuwa msaada mzuri ndani ya vyama, vijana nao wakapakwa mafuta ya matumaini ovyo ya ujana na sio bidii na ufahamu wa mhusika,almanusura wapagawe lakini kwa kuwa baadhi ni wasikivu walisikia maonyo ya wanajamvi na leo hii, wao wenyewe wameona tofauti na kujiunga katika kuhakikisha kuwa linapokuja swala la uongozi wa Taifa, mtu achaguliwe kwa kukidhi viwango hitajika kwa mujibu wa umma/jamii husika na sio kwa vigezo vya umri wa ujana au uzee, au sura nzuri.

Mwanzoni binafsi nilimkubali sana ZZK, rakini kwa sababu ya udadisi binafsi kama mtu ambae nasukumwa na UTAIFA na si vyama,nilijipatia baadhi ya mambo kiufahamu kumuhusu nakujua kabla sijasimamia kuunga mkono au kutetea hoja au issue yoyote anayoianzisha kijana mwenzangu huyo, ni lazima niwe nimejilizisha kuwa ZZK ni aina ya watu wa kuaminika kwangu.Da picha niyoiona siyo niliyotegemea binafsi nilianza kupata viashilia kwa upande wangu kuwa amebadilika.Siku ya siku nilikutana na mtihani, kuna siku Mzee wangu mmoja alipata kuniuliza swali "Do I think ZZK is a politician?"Hakika isingekuwa nimejiandaa kumjua ZZK,ningepata wakati mgumu kuaminika kiufahamu mbele ya wazee, kwa kuwa uwa tunabadilishana maongezi na baadhi ya wazee maswala ya jamii,kitaifa na kimataifa na ujio wa ZZK by then anaanza tulijadiliana na mimi kama kijana nilionekana very supportive kwa ZZK, kwa mujibu wa mwenendo wake mzima wakati anaanza harakati zake Bungeni mwanzoni.

Isingekuwa kufanya bidii binafsi wazee wangu wale wangeniweka kwenye kundi la wale wale ambao Mzee butiku anasema fanya kazi/chapa kazi jamii itakupima kwa mujibu wa kipimo cha kazi!!Bahati nzuri niliwajibu "he is not!!!!!!!"nikawapa vigezo vyangu.Nilikuja kuambiwa kale nako kalikuwa nikamtihami kangu wazee wangu kujua nami ni wale wale wapenda ujana kuwa vigezo au CONTENTS.

Alipokuja huyu nae January akitokea Mjengoni nikajua vijana [Wana] sasa wanapewa nafasi watuwakilishe vijana kisha wazee na jamii watupime ujana wetu kupitia watu aina ya vijana wenzetu wakina JM kisha pole pole wazee wawe wanawasongesha wana kwenye post njema zitakazo wapa fulsa za kufanya maamuzi yenye nguvu ya kuleta mabadiliko ya maisha ya Mtanzania na hasa yenye faida kubwa kwa kizazi kipya na kijacho.Aaaaaha toka huko huko mjengoni nikaanza kuona ndivyo sivyo mara huyu kaumizwa aka sugu analia,nikasema nilitegemea ambae hana chochote ndio ambae JM angemshika mkono nikimaanisha Sugu, ampe blessing aijalishi nini mwana asonge kupata hiyo ajira ya wageni.Matokeo yake naishia kumsikia Sugu [Bado Ajaitwa Mheshimiwa] ndani ya Radio Times FM akibubujikwa na machozi ya kudhulumiwa.

Kwangu ilikuwa ni kipimo tosha nacho cha kuanza kupunguza, credit zangu kwa huyu jamaa,na walipoungana na ZZK kwenye mikakati,ambayo kama ikiachwa hivi hivi, itavuluga mambo mengi ndani ya vyama vyao, hata mipango ya vyama vyao yani CCM na CDM, ya kuweza kutumia tulufu ya ujana kama njia ya kuvuta kura za wengi hasa kwenye nyakati sahihi za uchanguzi kipenga mezani.

Vyama kama vyama lazima viwe na Strategy hiyo ya VIJANA kama sehemu ya mbinu, lakini kamwe sio AGENDA KUU. UJANA ni mbinu ambayo kama ingetumiwa vizuri, ikatumika katika wakati mwafaka ingeweza kuleta ushindi kwa chama chochote kwa kuwa tunassume kuwa mpaka ifikapo mwaka 2015 panapo majaliwa kundi la wapiga kura wengi watakuwa ni vijana.Hivyo vyama vya siasa kucheza na MBINU hiyo ya UJANA kama sehemu ya kutafuta kura za kundi husika hakika mchango wa kura hizo ungekuwa na maana kubwa kwa ushindi.

Lakini kwa kinachojili sasa hivi, hata kama mkakati huo ulikuwepo hakika unakumbana na msemo it end before it start/yani imekwisha hata kabla ya kuanza.Uropokaji wa watu ambao tayari wanawafuasi na wanamamlaka ndani ya vyama vyao umechangia kuivua nguo agenda hii, hata wale King Makers uenda walikuwa na ajenda hiyo kwa waropokaji aina hii wameitia mchanga, hakika Ajenda itakuwa imechafuliwa vibaya sana.Manake siku ya siku hoja inawekwa mezani umma utajua kumbe RAIS mtalajiwa ametengenezwa na watu, na sio wao kupitia uratibishaji wamempata wanaeamini wao ni chaguo lao.

Na kwa vijana ni aibu!!!kuwa na watu ambao kila kukicha wao wanategemea ubaguzi wa umri kupata wasivyostahiki.Kwa kuwa wanajua bongoflava wengi hivyo ni lahsi wao kuegamia mgongo huo kuvuna kura.
 
nchi hii lazima viongozi na wataalamu wake waendelee kuwa vijana na watu wazima na wazee, huku vijana wakipewa nafasi zaidi lakini si lazima nafasi hiyo iwe kwenye urais. Kuna nafasi nyingi za uongozi na utaalamu zinazoweza kufanywa na vijana licha ya urais. Rais mzuri anaweza kuwa kijana au mzee mradi athibitishe uwezo mkubwa wa kuwa Rais.

unajua hii nchi, mfumo wa uongozi na utawala na katiba yetu vimetukremisha kwamba President is everything,tulishafikia kuwaita watukufu, tumeshasahu kwamba Rais ni ofisi yenye wataalam na washauri wengi ndani yake. kiukweli kama kila mtu akifanya kazi yake kwa uwezo aliojaliwa na Mwenyezi basi hata Rais akiwa 18 nchi itasonga mbele.
 
Back
Top Bottom