January Makamba Top The List of Most Interactive Politician in Tanzania!

daah kweli JK kaufanya urais kweny enchi hii uwe cheap mno?? yaani mpaka JM naye anawaza kuwa rais??? kweli kazi ipo ...mungu ibariki Tanzania
 
Mkuu Big Man, kujikomba komba ni kufanya jambo fulani au kusema maneno fulani favourable kwa upande fulani au kwa mtu fulani kwa sababu fulani!.

Mfano kwenye ile list ya Clouds, ni wazi kuwa No. 8 hakustahili kuingia kwenye top ten ila amewekwa kwa sababu!.

Sio kila ukiandika mazuri tuu au ukifuatilia habari fulani ni kujikomba komba, kujokomba komba ni pale tuu unapokuwa unafagilia tuu kwa sababu fulani!.

Media zinatakiwa kuwajibika kwa jamii with "truthfullness", "Objectivity", " Impartiality", and "Fairness and Balance".

Lakini ni ukweli uliowazi kuwa kuna media zinajulikana zinaegemea upande fulani kwa malengo fulani, huko ndiko kujikomba komba kwenyewe.

Laiti tungekuwa na sheria ya disclosure na transparency ya polical party funding towards election, ungeshuhudia jinsi ma********* walivyouchangia CCM!. Sio kuwa wanaichangia CCM kwa vile ndio wanaipenda sana, no!. Wanaichangia kwa sababu fulani!.

Hata humu jf, tunao wachache ambao tunasimama kwenye ukweli no matter what!. Hakuna ubishi kwa Chadema ndicho chama chenye mvuto na kasi ya ajabu ya kupanda chati kwa kasi ya upepo kuelekea ukombozi wa pili wa Mtanzania.

Kufuatia kasi hii ya Chadema kuna baadhi wataisifu na kuipongeza kwa dhati na kuna baadhi watajikomba komba kwa kusifu tuu hata pale Chadema inapofanya makosa!.

Vivyo hivyo kwa CCM, hakuna ubishi kuwa CCM imechokwa na kupoteza mvuto!. Wana CCM makini wanalijua hili na wanalitafutia ufumbuzi, wako wana CCM ambao nao wameichoka CCM lakini hawewezi kuiacha kwa sababu fulani fulani, hao watakuwa mstari wa mbele kuitetea CCM kwa nguvu zao zote kwa kujikomba komba kwa zile sababu zao japo kimoyo moyo wanajua CCM imekalia kuti kavu na iko mkao wa kifo!.

Ila pia lazima nikiri wazi kuwa "the deviding line btn kujokomba komba na kutetea genuinely is very thin"!.
 
Aliyekutuma amekudanganya. Hata kama hao uliowapendekeza hawafai na kama wanafaa ni kwako na wenzako lakini siyo watanzania. Inaonyesha wewe ni fisadi wa kunuka.
Mkuu Mpayukaji, sijakuelewa, ni aliyenituma mimi amenidanganya?!. Na hawa niliyewapendekeza mimi au hawa waliotajwa na Clouds?!. Kama hawafai, jee ni nani sasa wanaofaa?. Hili la mimi kuwa ni fisadi ni kweli!, nilikuwa natumia usafiri wa boda boda sasa natumia bajaj, nitapanda mpaka kutumia Starlet then Corolla then Benzi, the Hammer au Vogue na hapo ndipo sio nitanuka, nitanukia!.
 
Kwanza sio N/Waziri wa media yeye ni wa Mawasiliano!. Zamani ndio ilikuwa Habari na Mawasiliano, sasa Habari iko na Utamaduni na Michezo halafu Mawasiliano iko na Sayansi na Technolojia!.

Kwenye hilo la Clouds, January hajajitaja, ametajwa, ila pia kwenye kugombea urais wa CCM 2025 baada ya likizo fupi ya miaka 10!, January is the best that CCM has!.
 
Wadau mmesahau ba mwanasha aliingiaje????basi msimshangae na huyo Jr Ma-rope,,,, mnashangaa kwa yeye kupewa ea tym????wakat jk anautaka urais hao power breakfast walimfata kwake na kufanya nae live show,,,mmesahau kuwa clouds huwa wanamwandalia birthday mdau????
 

Duh, una kumbukumbuku nzuri sana.


Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
 

Nahisi ni kweli ,japo wengine hawakuelewi.
Bravo
 
@ Mkuu Mkandara, kuna jambo muhimu sana umelizungumza mwisho. ...Am not a hater!". Humu jf tuna hatters kibao!. Ukiuliza sababu za hizo hate hakuna!. People humu hates others for no apparent reasons!.

Wana jf tupendane kama familia moja hata wale ambao tunatofautiana nao!
 

Shallow minded. How can you link this with the 2015 general election? Kuwa great thinker
 

mjumbe hapo kwenye red umenacha,ina maana mh ana certficate tu!
 
Makamba akigombea urais nahama ndio itakuwa mwisho wangu CCM, maana utakuwa ni usela na sio akili kumwacha huyu braza men empty head agombee urais..nahamia chadema kipindi hicho..
 

Hii orodha inachekesha kweli kweli kama siyo kushangaza.

Kwanza swali ni WHO IS BEHIND Clouds TV? Hii yote ni Magamba style ya kujaribu kushawishi Watanzania kwa cheap politics and propagandas!
Hivi kwa akili tu ya kawaida unaweza kukubaliana na upuuzi huu kuwa JANUARI MAKAMBA ndiyo aew kinara kweli kati ya Wanasiasa wa nchi hii?? Tujaribu tu kujikumbusha kile kilichotokea Bungeni juzi baada ya Mhe. Zitto kuanzisha kura ya KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU! Kwanini basi mtu kama Zitto aliyeanzisha move iliyosambaratisha Baraza la Mawaziri la JK asiwe ndo nambari 1???? Basi kama ni upande wa Magamba wangelimweka hata DEO FILIKUNJOMBE au KANGI LUGOLA wabunge toka Magamba waliosaini kutokuwa na Waziri Mkuu wa Chama chao!!!

Januari Makamba was there but he was just a dumb dead in Parliament. Hakuunga mkono ile move si kwa ku-sign wala kwa maneno. Mimi sielewi Januari anawavutia watu kitu gani. Januari Makamba hana lolote zaidi ya kuwa amerithishwa mikoba na Baba yake Mzee Makamba lakini si chochote. Huyu ni mtu ameingizwa kwenye siasa simply because baba yake yuko kwenye system, same to Riz Kiwete,Nepi Nnauye na wengineo. Lazima watu wahoji ni kwa sifa zipi amewekwa wa 1 kwenye hii Top Ten?? Hivi tangu awe Mbunge na M/Kiti wa Kamati ya Bunge-Nishati/Madini amefanya nini cha maana? Waziri Nishati na madini kang'olewa wakti Kamati yake ipo pale inachapa uingizi. Haijwahi kutoa solution yoyote kwa matatizo tuliyo nayo kwenye Nishati na Madini. Nonsense!

Ukweli utabaki pale pale kuwa Top Ten hii ilitakiwa iwe imesheheni majina ya Viongozi na Wabunge wa CHADEMA tu. Full stop! Haya majina nje ya hapo ni longolongo tu za kutaka kuwaghilibu Watz.
 
Huyu ni mtu wa maajabu,ofisi ya kampuni yake eti anadai ni ofisi ya issue za ubunge wa bumbuli,kwanin asiiweke bumbuli huko huko? Huyu jamaa ni msanii.
 

Uelewa wako mdogo sana ndugu!!!!!!tathmini gani imekufanya useme miongoni mwa wana CCM milion 5 wanachama Makamba is the best!!!!Una matatizo sana wewe!!!Na wewe una tofauti naye,tatizo tu wewe labda maskin,na njia walizopitia wakina Makamba na wanazopitia kamwe wewe ni ngumu mpaka ujinafikishe na ujidharirishe vya kutosha kama ufanyavyo!!!ILA MWISHO WENU WAJA!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…