January Makamba on Dakika 45 ITV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

January Makamba on Dakika 45 ITV

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mchambuzi, Aug 6, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Januari Makamba ni kweli amejitahidi sana kujieleza ingawa binafsi nime ‘note’ mapungufu kadhaa ambayo nitayataja pengine kwa upeo wangu mdogo lakini nia ikiwa kumsaidia tu mawazo iwapo atapita kupata feedback kutoka kwetu sisi vijana wenzake ambao nia na lengo letu kuu ni kama yeye - kuhakikisha Tanzania ya kesho inakuwa bora kuliko Tanzania ya leo.

  Nitayataja mapungufu machache lakini niseme tu kwanza kwamba nadhani yote haya ni matokeo ya aidha January kutopata muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya kipindi kutokana na kutingwa shughuli za bunge dodoma; au pengine host hakumpa muda wa kutosha kujieleza ndani ya zile dakika 45; au labda January bado ni mgeni katika hii sekta, hivyo by default akajikuta ana focus zaidi katika kufafanua jinsi anavyoielewa sekta hii hivyo kukosa muda wa kutosha kuwa in touch na mwananchi wa kawaida ambae lengo lake kuu ni kajaribu kuelewa the role of TEHAMA katika Maendeleo yake na ya taifa kwa ujumla - uchumi na kijamii.

  Amejitahidi kidogo kugusia maeneo muhimu kwa mfano masuala ya mobile baking, gap between growth of the sector na kanuni/sheria za kudhibiti sekta, umuhimu wa National Backbone n.k. lakini overall, nadhani ni kutokana na haya yafuatayo ndio maana hakufanikiwa sana kumjengea mwananchi wa kawaida consistency na substance ya kutosha – hasa iwapo mwananchi alikuwa anajaribu kuelewa umuhimu wa sekta hii kimaendeleo - kiuchumi na kijamii(s):

  1. Kwanza, nimeshangaa kwanini hajagusia kabisa Sera ya Taifa ya TEHAMA (National ICT Policy), ambayo ina vision and mission zilizo very elaborate kuhusu nini watanzania kama taifa tunataka kufanya na wapi tunataka kwenda katika karne hii ya sayansi na tekinolojia. National ICT policy ingemsaidia kuwa na mtiririko mzuri sana.

  2. Pili, since kazi kubwa ya sekta hii ni kuchangia katika Maendeleo ya taifa, hajagusia lolote kuhusu Dira ya 2025 (Vision 2025), hasa juu ya umuhimu wa TEHAMA katika kufanikisha malengo mengi yaliyoainishwa kwenye Vision 2025, hasa lengo la kuifanya Tanzania iwe nchi yenye uchumi wa maendeleo ya kati ifikapo 2025. Kuna mengi ambayo angeyagusia hapa kwa mfano e-development: e-governance, e-health, e-education n.k.

  3. Tatu, hajagusia kabisa Tume Ya Sayansi na Tekinolojia (COSTECH). Taasisi hii inatakiwa kuwa a life blood ya wizara yake na ilitakiwa iwe ya kwanza kwenda kuitembelea alipoteuliwa, badala ya kwenda TCRA. Costech ni taasisi muhimu sana kwa sekta anayoiongoza, kwani inajihusisha na masuala ya Utafiti na Maendeleo ya Sayansi na Tekinolojia nchini. Chombo kama hiki kwa nchi za wenzetu ndio mshauri mkuu wa wa masuala yote yanayohusiana na Sayansi and Tekinolojia na matumiza yake katika Maendeleo (kiuchumi na kijamii), lakini pia usalama wa nchi.

  4. Nne, hajagusia suala la National Innovation Systems na umuhimu wake katika Maendeleo ya taifa. Nchini kwetu, suala hili linasimamiwa na Costech, lakini taasisi hii imekuwa inapata tabu sana kupata ushirikiano wa kutosha serikalini (hasa fedha), kwa mfano ukiangalia kiwango tunachotenga for Research and Development (R&D) Tanzania ikilinganishwa na wenzetu, unaweza kutokwa na machozi, hasa ukielewa umuhimu wa R&D katika Maendeleo ya uchumi. National Innovation Systems ndio siri ya mafanikio kwenye mataifa mengi ambayo yamefanikiwa kuingia katika uchumi wa kati kutokea uchumi wa chini.

  5. Mwisho, ni TTCL and its role katika uchumi wetu – changamoto zinazolikabili shirika hili, fursa zilizopo na mikakati iliyopo. Amejaribu kugusa TTCL lakini kidogo sana na juu juu; hakutumia nafasi yake vizuri kuelezea umuhimu wa shirika hili na mikakati ya serikali kuliinua tena. Hakuna taifa linalofanikiwa katika sekta ya TEHAMA bila ya kuwa na its national telecommunications services company. Suala la kuwa private, public au mixed ni mjadala mwingine lakini the bottom line ni kwamba mashirika kama British Telecoms (BT), Verizon (formerly Bell Atlantic), Telkom (South Africa), China Telecom na mengine mengi tu South East Asia na Latin America yamechangia maendeleo katika mataifa yao kwa kiasi kikubwa sana.
   
 2. Kyenju

  Kyenju JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 4,573
  Likes Received: 274
  Trophy Points: 180
  Katika kipindi cha dakika 45 ITV leo, Januari Makamba amefafanua na kujibu maswali kwa utulivu na umakini, ni kichwa.
   
 3. Kyenju

  Kyenju JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 4,573
  Likes Received: 274
  Trophy Points: 180
  Kweli umeeleza in deep, ila pia tatizo lingine naona dk 45 ni ndogo sana kwa sekta nyeti kama hii.
   
 4. s

  swanga Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Sikupata mda wa kumsikiliza ila sina imani nae, Siamini hivi vipindi recorded wanaweza kuedit, KUMBUKA KAMATI ALIYOKUWAMO NDO INAKASHFA:- Swali YEYE KAPONEA WAPI?
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi,

  Vitu vingine havigusiwi kwa sababu vita expose weakness ya uongozi.

  We sasa kama hatuna sera ya "TEHAMA", au ipo ya ajabu haitekelezwi/haitekelezeki, mtu mwingine anaona badala ya kujiingiza katika minefield ni bora apige talalila nyingine tu aache kuongelea such a central aspect of the question.

  Kigwangwalla ndio anawaita "smart" watu wanao divert mazungumzo kutoka central issues kupeleka kwenye political rhetoric and linguistic sommersaults kama balozi wa Jamaica UK. Anaongea sana mpaka mtangazaji anamkatisha lakini ukijiuliza alilosema nini mwisho wa kipindi unaona umeunganishiwa boilerplate bs na excuses mwanzo mpaka mwisho, complete with reference to all the blue books.

  Mwingine huyu hapa mchuuzi wa maneno, ahadi ahadi tu kila siku, hamna lolote.

  President Jakaya Kikwete at Seacom's Fibre Optic Cable station launch (MichuziBlog) - YouTube

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mi namwona kama mwanaharakati zaidi haja uvaa uwaziri na Sifa ya ccm ukiingia msafi utatoka Unanuka, na ukitaka utoke na usafi wako basi watakushushia zengwe la kukuchafua 2
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Vichwa halisi huwa havifutiwi matokeo kwenye mtihani kwa hatia ya kufanya udanganyifu kwenye mitihani...!
   
 8. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sasa kwanini unamwita kichwa!!.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Mimi mbona siuongi huo ukichwa wa huyo jamaa? Namuona wa kawaida sana. Sasa sijui nyie wengine mnaonaga nini ambacho mimi sikioni. Au basi tu mmejenga mazoea ya kusifia kawaida?

  Manake kila nikijaribu kuutafuta ukichwa wake siuoni. Ninachoona ni ordinary tu. Nothing extraordinary.
   
 10. RaiaMbishi

  RaiaMbishi JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 252
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ukichwa maana yake ni nini? Pengine tungejaribu kwanza kuja na consensus kuhusu maana ya hili neno ‘kichwa', then ndio tutazame kama January ni kichwa kwa uelewa utakaojiri. Mimi navyoelewa, kichwa kwa lugha ya wenzetu inakaribia na neno ‘intelligent'. Kama tunakubaliana juu ya hili, basi kusema January intelligent maana yake ni pamoja na:

  -Moja, exercising or showing good judgment.
  -Mbili, possessing sound knowledge.
  -Na tatu, having the capacity for thought and reason especially to a high degree.

  Mimi nadhani, hasa kuhusu mdahalo ule wa ITV ambao mimi pia niliutazama, tumpe January credit kwamba alijitahidi, lakini kwa kigezo cha ukichwa kwa maana ya tatu hapo juu…having the capacity for thought and reason especially to a high degree. Kwa maana ya kwanza na ya pili hapo juu sijawa convinced sana. Otherwise ni wazi na hakuna ubishi kwamba wapo vijana wengi humu Jamiiforums na kwingineko aidha wanafanana na January ukichwa au pengine hata kumzidi, tofauti ni kwamba tu hawajapata jukwaa kama la January kuonyesha makali yao.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  ukichwa gani wakati hatuoni performance yoyote? ushuzi at best..mpaka leo watu wanalipishwa bei za internet za ughali kuliko hata dunia ya kwanza na hata majirani zetu. ulipaji kodi wa mashirika ya simu za mkononi bado ni kizungumkuti kulinganisha na majirani zetu..
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Aug 14, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Kama January ni kichwa je, Tim Berners-Lee atakuwa nini?
   
 13. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,092
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  HANA KITU KAMA BABAK TU, anajisikia, msaliti, na anavaa uhalisia wa watu wengine, sio yeye, na yeye hasimami alone
   
 14. Bambo

  Bambo JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 237
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  tuna matatizo ya kujisifia au kutokujua mambo hata ya kawaida sana ndo maana mtu akijieleza kidogo tu basi oooh kichwa..huyo dogo ni kwamba tu ana access ya information lakini hana la ajabu analoongea.
   
 15. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Lakini kila mtu ana mapungufu yake, nadhani ingekuwa jambo la busara zaidi kumsaidia mawazo pia juu ya sekta yake hii, whether he takes the advice or not, hilo atajua yeye, otherwise nadhani if we take a step further na kumpa mawazo, sio tu itamsaidia yeye, bali hata wasaidizi wenzake ambao watakuwa na hamu ya kusikia watanzania wanasema nini. Mimi nina uhakika humu kuna wenzetu ambao ni wataalam katika nyanya ya TEHAMA na wametapakaa nchi mbalimbali duniani. Let us pick you brain katika hili.
   
Loading...