Gumzo na baadhi ya vijana kwenye kijiwe cha Bodaboda Kariakoo jioni ya leo. Kila mmoja ana historia na ndoto mahususi za maisha yake. Wote wana maoni mengi namna gani mtu mmoja mmoja na pia nchi inaweza kufika pale tunapotarajia katika ngazi ya maendeleo na uwajibikaji. Ni jambo jema na la kutia moyo sana kuona vijana wana mtazamo chanya na mpana namna hii kuhusu hatima yao na nchi yao.