January Makamba: amegawa simu, anakula matapishi yake

chuki

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
2,715
Reaction score
534
January Makamba(Mb)-Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia. Mwanasiasa Kijana ambaye tangu amejiunga na siasa mwaka 2010 na kuwa mbunge amekuwa akisimamia kile anachokiamini kuwa ni "Haki".
Itakumbukwa akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini alishiriki kikamilifu kumsulubu Ngeleja aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, hapo January kijana wa Makamba alionekana kuwa kiongozi wa CCM anyeweza kuikosoa serikali inayoongozwa na Chama chake. Alitoa matumaini kwa kazi ile.

Lahaulaa! January Makamba amekuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano kwa kipindi kifupi cha miaka miwili sasa amebadilika, January Makamba amekuwa akihusishwa na siasa za uchonganishi na harakati za kuusaka Urais wa Tanzania kwa kivuli cha ujana, maoni yake yamekuwa hayo, anatajwa kumuunga Mkono Lowassa -Waziri Mkuu alifukuzwa kwa Ufisadi, Mara taarifa zinaibuka sio hayo tu bali mwenyewe amekaririwa akijitaja kuwa ''anatosha 2015" kupitia Tamko la wanafunzi wa chuo wa mwaka wa kwanza, na wengine wakamgeuka kuwa sio kweli hao walitumwa baada ya malipo kutoka kwa Waziri huyo-TAHILISO ikaruka kimanga.

Makamba huyuhuyu amegawa simu nyingi zipatazo 150 aina ya Samsung Galaxy Grand yenye thamani ya Shiling laki Saba (700,000/-) kila moja sawa na Milioni Mia Moja na Tano (105,000,000/-) kwa vijana wa UVCCM katika Baraza kuu la Umoja huo lililofanyika Zanzibar siku ya Jumapili tarehe 01/09/2013.
Simu hizo zikaambatana na package "nono" Laini ya Airtel bure iliyosajiliwa bila gharama, Vocha na Bundle ya Kutumia kwa miezi Sita bure, discount ya kununua vifurushi kupitia mtandao huo 20% baada ya ofa ya awali ya miezi sita kuisha, warranty na Grantee ya miaka miwili ya kutumia simu hiyo bure ikipata tatizo ruksa kubadilisha mpya kwa muda wote huo.

Makamba ametumia nafasi hiyo kuwatumia vijana hao wamsaidie katika kampeni yake ya kutafuta madaraka "Makubwa', Kinachosumbua duru za habari, Makamba katoa wapi fedha hizi? anafanya hivi kwa Haki au kwa Tamaa?
Makamba anakula Matapishi yake, anatumia Influence hiyo ya Nafasi ya Unaibu Waziri-Mawasiliano kuyatisha Makampuni ya Simu kufadhili 'mradi' wake wa madaraka.
Kampuni inakupa simu, inakupa ofa ya Mamilioni kwa mkataba gani? kesho Kampuni hiyo ikikwepa kulipa kodi au ikivunja sheria utakuwa upande gani kwa maslahi ya nani? Makamba amekula Matapishi yake kwa hifadhi ya madaraka 'Makubwa'. " Haya Mambo Madogo sana kwa Waziri wa Wizara hii" amenukuliwa Makamba katika Kikao hicho.

Hii inatoa picha kuwa kama hayo ni mambo madogo basi Waziri wa Maliasili na Utalii agawe Pembe za Ndovu kwa kundi lake kwakuwa hayo ni mambo anayoyasimamia kwahiyo ni 'rahisi' kuyapata, Waziri wa Nishati apewe Mapipa Mia moja na Hamsini na Makampuni ya Mafuta kama TOTAL na GAPCO kwakuwa hiyo ni Wizara anayoisimamia, Waziri wa Fedha ajichotee Mamilioni kila siku akitaka kwakuwa yeye anasimamia 'Hazina'. Waziri wa Afya apewe Kontena la dawa na Vifaa kwakuwa MSD iko chini yake kwahiyo ni rahisi kuzipata, n.k katika Wizara nyingine pia. Je hapo kuna serikali? nani atasimamia walipa kodi? Hii ni AIBU KUBWA KWA KIONGOZI HUYO KIJANA, Hii haipishani na Kashfa ya "SUKARI" ya aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Enzi hizo ndugu Iddy Simba wakati wa Mkapa, Mpaka leo bwana huyu yuko katika kashfa ya kuifilisi UDA, Ufisadi wa 'TAIKUNI' Simba ulianza kama alivyoanza January Makamba.

Makamba umekula Matapishi,Umeiweka Rehani Serikali ya Chama Chako ni vyema 'uwajibike' la hasha Tangaza una ubia gani na Makampuni ya simu.
 
huyu jamaa inabidi aamshwe, naona yuko usingizini.
 
Hizo simu amegawa ili wawe wanajibu, kuzipinga na kuzichafua thread zote zinazoonyesha kuibana CCM hapa JF kwani wote kujazana Lumumba inakuwa ngumu kwa hiyo wamepewa wawe wanajibu wakiwa popote. Pia wawe wanaandika mambo ya kumsifia na kumjenga katika mitandao ya kijamii ili afanikishe ndoto za alinacha alizonazo eti kugombea Urais.
 
inasemekana mwenyekiti wa UVCCM hawezi hata kutuma sms sembuse JF?
 
huyu jamaa inabidi aamshwe, naona yuko usingizini.

nilikutana naye kipindi fulani Washington DC ktk mazungumzo yetu alikubali kuwa ccm na serikali vina matatizo makubwa lakini yeye akadai ataingia ndani na kujaribu kubadili hali hiyo. sasa kwa mtaji huu badala ya yeye kuibadili CCM, inaelekea CCM Imembadili yeye.i was very skeptical with his explaination na uwezo wake wa kuibadili CCM. I am glad he has rest my case for me.
 
Hizo simu amegawa ili wawe wanajibu, kuzipinga na kuzichafua thread zote zinazoonyesha kuibana CCM hapa JF kwani wote kujazana Lumumba inakuwa ngumu kwa hiyo wamepewa wawe wanajibu wakiwa popote. Pia wawe wanaandika mambo ya kumsifia na kumjenga katika mitandao ya kijamii ili afanikishe ndoto za alinacha alizonazo eti kugombea Urais.

Sasa ataweza kuwadanganya watu wa huku JF The Great Thinkers? wacha aingie hasara, naona na yeye anajaribu bahati yake kwani Nchemba alitumia mahela kibao ya CCM na Ya sembe lkn sasa anasambaratika
 
chuki - Ungonyesha alipoiba hizo simu ungekwua na hoja nzito, otheerwise ni majungu kama kawaida yenu umri wa Januari hauruhusu kugombea urais, yaani huna facts wala dataz poleni sana!!!

Le Mutuz
 
Last edited by a moderator:
- Yaaap tumejionea kweli jinsi Mkurugenzi wa kampuni ya kigeni nchini kama vodacom anavyotakiwa kuishi, sio kama mkulima wa kijijini halafu next time lete picha za nyumbani kwa MWenyekiti wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema tuone kama wanafanana na wananchi wanaodai wanataka kuwakomboa!!

Le Mutuz

Ha!ha!ha!ha!ha!...You know, kama vipi sishangazwi ni kwa nini wengine wanakuitaga kubwa jinga....First of all, hizo picha ni kwa hisani ya mtoto wa dadako. Mange Kimavi. I did not take them. Nenda kamuulize

Mambo yako ni ya kijinga jinga tu....Unajuaje kama mimi ni mwana CCM damu aliyechoka na ufisadi. At 54, nilidhania ungekuwa unafikiri vizuri badala ya kukurupuka

Lemutuz, you know. Unadhalilisha wanawake Tanzania, ndio maana CCm tumekuona gunia la kokoto. Juu ya kujikomba kwa kila mtu, umebaki unachukiwa kama panya. Wewe lazima huko kwenye hukoo wa panya. Licha ya kutumia jina la Malechela, hata ukuu wa wilaya haupati. Mimi CCM tangu 1989, kwa hiyo kapige picha mibebs alafu urudi kuropoka !

Habari ndo hiyo......!
 
Re: January Makamba: AMEGAWA SIMU,ANAKULA MATAPISHI YAKE.
Mambo yako ni ya kijinga jinga tu....Unajuaje kama mimi ni mwana CCM damu aliyechoka na ufisadi. At 54, nilidhania ungekuwa unafikiri vizuri badala ya kukurupuka

Lemutuz, you know. Unadhalilisha wanawake Tanzania, ndio maana CCm tumekuona gunia la kokoto. Juu ya kujikomba kwa kila mtu, umebaki unachukiwa kama panya. Wewe lazima huko kwenye hukoo wa panya. Licha ya kutumia jina la Malechela, hata ukuu wa wilaya haupati. Mimi CCM tangu 1989, kwa hiyo kapige picha mibebs alafu urudi kuropoka !

Habari ndo hiyo......!

- Duh!! kweli elimu ni muhimu sana kwa maisha ya binadam ona kichwa cha mada na maneno yako tofauti kabisa kwa nini usianzishe topic inayonihusu na mabebs maana hapa uliyoandika yote hayahusu, huna hoja umejaa majungu majungu, sasa ulitaka Mkurugenzi wa Vodacom kama Mwanvita aishi vipi kama wewe mlalahoi? ha1 ha! ha! ha!, the mburulazzzz!!

- Kumbe Ukuu wako wa Wilaya umeupata kwa kujipendekeza huko Chadema? ha1 ha! ha!

Mchumba wako Flora Lyimo anakusalimia. I have no time to waste discussing anything with you. You are all a family of rats......! Come 2014 natupa kadi yangu ya CCM chooni. Hauna maana kabisa, kazi kudhalilisha wanawake. You are supposed to be a grand father not running around with 18 year old little girls. Shame on you !

Hiyo familia ni ya kifisadi
 
- Sina watoto na wajukuu kama Dr. Slaa so hayanihusu, nina watoto wawili tu pole sana mjadala hapa ni Januari Makamba naona unajaribu sana kunitoa kwenye mjadala ila unapoteza muda fungua thread ya LE Big Shoow na Mabebs kama una tatizo. Wewe kazi yako ni majungu majungu tu, onyesha Waziri alipoiba pesa za simu otheriwse nyamaza tu!!

- Kama una tatizo na maisha yangu fungulia thread yake hapa ni mada simu alizotoa Januari., ha! ha! mwanaume mzima umbeya umbeya tu!!

William
Ni bora ukahacha kujiingiza kwenye vitu vingine kama mtu mzima. Hauna uhakika kama huyo ni mwana CDM au CCM kwa maana January ana maadui wengi sana ndani ya Chama chetu. Zanzibar ilikuwa ni wana CCM kwa hiyo hapo sidhani ni chadema. Nchimbi anapiga majungu kinoma naye alikuwepo. Kuna baadhi ya watu nchimbi aliwaambia kuhusiana na hii habari ya simu, kwa hiyo nina uhakika 100% kwamba majungu yametoka kwa Nchimbi

Hii ni ngoma ya Nchimbi
 
- Duh!! kweli elimu ni muhimu sana kwa maisha ya binadam ona kichwa cha mada na maneno yako tofauti kabisa kwa nini usianzishe topic inayonihusu na mabebs maana hapa uliyoandika yote hayahusu, huna hoja umejaa majungu majungu, sasa ulitaka Mkurugenzi wa Vodacom kama Mwanvita aishi vipi kama wewe mlalahoi? ha1 ha! ha! ha!, the mburulazzzz!!

- Kumbe Ukuu wako wa Wilaya umeupata kwa kujipendekeza huko Chadema? ha1 ha! ha!

Le Mutuz

Nani kakwambia kwamba wewe una elimu? elimu ya ubaharia, Umiss Ilala au elimu ya kuunga unga ya mtandaoni? Dont dare going there. I will strip you bare naked. Unafikiri sikujui? I know you since 1982. Figure out !

Mimi siyo Flora Lyimo ambaye unakaa nay kwenye nyumba iliyojaa Panya ya babako !
 
Mimi huwa sipendi majungu, udaku na pia hii dhana ya kwamba kila tajiri nchini Tanzania ni mwizi na fisadi lakini vile vile Matajiri nao wangewatendea haki watu kama mimi kwa kuwa wawazi katika kazi, biashara na utajiri wao.

Wazungu wanaposema "There ain't no such thing as a free lunch" wanakuwa na maana nzito. Kama kweli Mh. Makamba Jn anasimama kwenye dhana ya ukweli na uwazi basi ni lazima AUFUTE usemi huo kwa kuwaeleza wananchi ni kina nani walifanikisha hii kitu anayoita 'Kaharambee kadogo' pale aliposema,

Alisema kabla ya kutoa simu hizo, umoja huo ulimkumbusha kuhusu ahadi yake kutokana na barua yenye kumbukumbu namba VMM/M.30/39/Vol.17/35 ambayo pia ilimwalika kuhudhuria kwenye mkutano wa juzi.

Makamba alisema ili kutimiza ahadi hiyo, alizungumza na baadhi ya makada wenzake na kuwaomba wamsaidie.

"Nilifanya kaharambee kadogo, mtu ukiombwa na wewe unahangaika huku na huko, walinipa na jana (juzi) tuligawa simu 138," alisema.
"kaharambee kadogo" ka kupatikana kama inavyodai simu zipatazo 138 zenye dhamani ya Ths 96,600,000 siyo kadogo kwa macho ya wananchi wengi ambao ni walalahoi nchini. Inahitaji maelezo na pia siyo kitu cha kuficha kama waliofanikisha "kaharambee kadogo" ni watu halali na wametoa kwa uhalali ndani ya moyo kama wa masaritan wa enzi za biblia walivyokuwa wanafanya kule Samaria.

Nje ya hivyo, tutaendelea kujiuliza maswali mengi yenye sintofahamu zenye mitazamo hasi kulingana na nafasi yake katika jamii na serikali.
 
Mimi huwa sipendi majungu, udaku na pia hii dhana ya kwamba kila tajiri nchini Tanzania ni mwizi na fisadi lakini vile vile Matajiri nao wangewatendea haki watu kama mimi kwa kuwa wawazi katika kazi, biashara na utajiri wao.

January ni fisadi na mtu hatari mwenye huchu wa madaraka.........
Wazungu wanaposema "There ain't no such thing as a free lunch" wanakuwa na maana nzito. Kama kweli Mh. Makamba Jn anasimama kwenye dhana ya ukweli na uwazi basi ni lazima AUFUTE usemi huo kwa kuwaeleza wananchi ni kina nani walifanikisha hii kitu anayoita 'Kaharambee kadogo' pale aliposema,

"kaharambee kadogo" ka kupatikana kama inavyodai simu zipatazo 138 zenye dhamani ya Ths 96,600,000 siyo kadogo kwa macho ya wananchi wengi ambao ni walalahoi nchini. Inahitaji maelezo na pia siyo kitu cha kuficha kama waliofanikisha "kaharambee kadogo" ni watu halali na wametoa kwa uhalali ndani ya moyo kama wa masaritan wa enzi za biblia walivyokuwa wanafanya kule Samaria.

Nje ya hivyo, tutaendelea kujiuliza maswali mengi yenye sintofahamu zenye mitazamo hasi kulingana na nafasi yake katika jamii na serikali.

January ni fisadi, mwizi wa mtihani na mtu hatari kwa usalama wa nchi. Atuelezee fedha katoa wapi
 
Sasa ataweza kuwadanganya watu wa huku JF The Great Thinkers? wacha aingie hasara, naona na yeye anajaribu bahati yake kwani Nchemba alitumia mahela kibao ya CCM na Ya sembe lkn sasa anasambaratika

Kwa taarifa yako huju JF imevamiwa na kuvurugwa na mashabiki wa mafisadi kwa mbwe na bashasha hushabikia mada za

kizushi na propaganda kama za vita ya Rwanda na Tanzania ambayo kimsingi haipo. Niwengi ambao linapotoke jambo la

msingi wao kazi yao ni kukanusha na kutetea mafisadi. Fuatilia utapata majibu, njaa ni kitu kibaya sana.
 
January ni fisadi, mwizi wa mtihani na mtu hatari kwa usalama wa nchi. Atuelezee fedha katoa wapi
Kusema Makamba Jnr ni mwizi na fisadi kwangu mimi naona ni kutoa hukumu bila vidhibiti mbadala na kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunapigia chapuo ile dhana ya kwamba kila tajiri nchini Tanzania ni mwizi na fisadi.

Kitu cha muhimu hapa nimkufahamu mchanganuo wa hako "Kaharambee kadogo" ili kuondoa wingu la sintofahamu na fikra hasi kutoka kwa watu wenye kumtakia mafanikio katika kazi za kijamii na kiserikali.
 
Back
Top Bottom