January Makamba aibuka na Mbinu Mpya ya Rushwa

January Makamba aibuka na Mbinu Mpya ya Rushwa

Ole Shider

Member
Joined
Oct 17, 2014
Posts
16
Reaction score
15
Kuelekea miezi ya uchaguzi mengi yameendelea kujitokeza na wenye kutamani kufika pale alipo JK wameendelea kutafuta mbinu mbalimbali za kuweza kushawishi wapiga kula wao.

Asubuhi napita kusalimia katika ofisi za Umoja wa Vijana ambako ndiko ninako wajibika ghafla nashangaa kuona Katibu wangu ananipokea na Kitabu chenye nasaba ya mmoja kati ya Vijana wanaogombea Ulaisi Ndgu. January Makamba chenye kichwa cha habali Maswali 40 ya Kalugendo kwa January.....

Kwanza niliuliza kinauzwa bei gani nikaambiwa Mwenyekiti ni zawadi yako hiyo na imetolewa kwa viongozi wote wa Mkutano wa CCM wa Taifa.........

Sikushtuka sana manake akili ilinipeleka mbali kwamba sasa hii ni aina mpya ya rushwa ambayo Mangula hatokaa aione. Hivi kweli leo unawapa wajumbe Kitabu chenye kulasa zaidi ya 200 ili iweje?? Kwanza muda wa kusoma uko wapi?? Na kwanza nasoma nini?? Halafu huyu muhusika uwezo wake wa kiuandishi ameugundua lini?? Alikuwa wapi siku zote?? Na ni kwa nini afanye iwe dezo wa watu wa CCM tu tena wapiga kura ndani ya chama?? Hivi kama huu si upunguani ni nini

Yaani January kwa kweli umekuwa janga sasa. Umeanza staili mpya ya kuhonga Vitabu........ tatizo umesahau kuwa raha ya Kitabu ni mtu akitolee jasho kwa kukinunua ili awe na uchungu wa kukisoma blaza lakini hii ya kuhonga kwanza mi nimekichoma manake ni kama vile unanipotezea muda wa kwenda kuweka sawa kula za Mteule wa Mungu yule yule ambaye amekuwa jiwe kuu la pembeni, yule yule aliyetoka ili kulinda heshima ya Nchi, yule yule mwenye uwezo wa kiungu.....

Hivi Makamba wewe leo wenzio wanaumwa, wanatafuta ada wewe unapeleka Pamphlets zako....... Nawe wajifanya Dream from my father.........

Ludi Jimboni kapange madiwani wako usije ukakosa yote walisema wakubwa "Mtaka Yote Kwa Pupa Hukosa Yote....."
 
Vingine vinauzwa na kugawa kwenye foleni za magari barabarani
 
Wewe nawe!

Akili nyepesi imekariri mambo mepesi! Rushwa iko wapi hapo? Hata kama wewe ni 'team lowa-hasa' inabidi uwe na uvumilivu wa kusikia,tafakari,chambua mbinu na mikakati ya wapinzani wenu.

Tatizo unadhani huu ni ule muda wa 'kuhubiriwa' tu (ndiko mnapowapata wa-tz wengi maana mnahubiri uongo na ----- wakati mwingine). If the race took turn for the better, so be it. Acha machapisho yatoke, watu wasome,watafakari wafanye maamuzi!

Kila mtu angekua na fikra 'biased' kama zako Rais mstaafu Mwinyi asingemsifia Lowa-hasa majuzi kule Arachuga na ilhali ndie alieandika Dibaji ya kitabu cha maka-hamba. Learn to keep an open mind to everything, it will help you in the long run.

Yeyote anaetaka kwenda ikulu, acha apitie chujio zote, let him prove it, let him show he has what it takes to get there in these modern times, tusikariri mbinu za miaka hiyo ziendelee kuwa mbinu za miaka hii!
 
Mada nzuri Kiswahili chako kinachefua sana.

Mkuu,
Inasikitisha sana, uwezo wa vijana wa maCCM katika kuandika kiswahili.

Tazama mabandiko ya wana CCM ni aibu tu. Ndio maana muda mwingi hutumia waandishi habari njaa ili kuwasaidia.

Makosa madogomadogo ni sawa ila haya ya maCCM ni kichefuchefu.
 
Mimi nishasema kuwa wawaache wanachama tuamue haya mambo ya kulazimishana kusoma kitabu yametoka lini January? Hivi kweli kura yangu nikupe January kwa vigezo vipi? Kumbuka wengine tuko CCM kwa sababu kuna tumaini moja tu lililobaki.
 
Nimesoma kitabu cha padre Karugendo alipomuuliza January Makamba maswali yake arobaini. Majibu ya January katika maswali yale unfortunately, hayaoneshi kama ana vision yeyote ya kuweza kutatau kero za watanzania ; anachokifanya kwenye hicho kitabu ni kuorodhesha matatizo yanayoikumba nchi bila kutoa njia mbadala za kutatua matatizo hayo , na anapojaribu kufanya hivyo anakuwa superficial and unrealistic!! Swala la ajira kwa vijanakwa fano mmoja , ni kero kubwa sana hapa nchini lakini halijadili kwa kina na hasa hailezei jinsi interlinkage kati ya kilimo na viwanda inavyoweza kutatua kadhia hiyo. Wachumi wengi kutoka nje na wandani pia wanaowaiga siku hizi wanashauri kuwa mazao yetu ya kilimo yaongezewe thamani kabala ya kuyauza nchi za nje yakiwa raw as a way of increasing employment na export earnings lakini kwa nchi kama yetu ni bora kuwa na viwanda vya nguo kuliko kuexport YAWN kwani kufanya hivyo tutaajili watu wengi hapa nchini compared to exporting YAWN; na export earnings zitakuwa zaidi!!

Kwa bahati mbaya sana January ameingia kwenye mtego wa kumsifia sana Kikwete katika majibu yake kuwa huyo ndio kamjenga kisiasa hivyo ndio mentor wake mkubwa; hiyo inaweza kumsaidia HUKO KWENYE CHAMA CHA MAGAMBA LAKINI KWA REKODI YA UTENDAJI WA NCHINI HAPA KUMTAJA KIKWETE KAMA ROLE MODEL WAKO NI LIABILITY!!!. Sio siri kuwa utendaji wa Kikwete katika kuongaza serikalina hata katika chama chake umeonesha udhaifu mkubwa sana hivyo wananchi hawatakuwa tayari hata huko magambani kuona kuwa wanaongozwa na mtu ambae atakuwa kama Kikwete kiutendaji!! January kwa kumsifia Kikwete amejipaka matope yasiyosafishika. .
 
huwa siamini kuwa kuwa january yuko serious anataka urais.nadhani anatumika tu kama chambo lkn mhusika mkuu yuko pembeni.

hata wakati ule alipoanza hatakati za kugombea ubunge alitumia mbinu hiyo hiyo ya kutoa kitabu.anafikiri na sasa itafanya kazi
 
Back
Top Bottom