Jangili aliwa na Simba Mbugani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Mtu mmoja aliyeshukiwa kuwa jangili wa wanyama aina ya faru amekanyagwa na Tembo na kuliwa na Simba katika hifadhi ya taifa ya Kruger, nchini Afrika Kusini.

Familia ilipewa taarifa kuwa mtu huyo aliuawa na tembo siku ya Jumanne.

Ulipofanyika msako hatimaye fuvu la kichwa cha mtu huyo kilipatikana na suruali siku ya Alhamisi.

Mkurugenzi wa hiadhi hiyo ametoa salamu za rambirambi kwa familia.

''Kuingia kwenye mbuga ya Kruger kinyume cha sheria na kwa miguu si jambo jema,'' alisema Murugenzi huyo. ''ni mbuga yenye hatari nyingi na tukio hili linadhihirisha hayo.''

Hifadhi ya Kruger imekua ikikabiliwa na changamoto ya uwindaji haramu kutokana na uhitaji mkubwa wa pembe za faru kwenye nchi za bara la Asia.

Siku ya Jumamosi, mamlaka za kiwanja cha ndege Hong Kong zilikamata mzigo mkubwa wa pembe za faru, mkubwa zaidi kwa kuwahi kukamatwa katika kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya pauni milioni 1.6

Kuna takribani Simba 2,000 kwenye hifadhi ya Kruger
 
Nice

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe dada hua nakukubali nyuzi zako.
 

Tunamsikitia na kumwombea aliyepoteza maisha. Lakini pia tunashangilia kwamba wanyama sasa wameanza kujua kujilinda na kutoa adhabu kwa wanaowadhuru!!πŸ˜—πŸ˜—
 
Walijuaje kama alikanywagwana Tembo kisha kuliwa na simba na sio chui? Au aliliwa na simba/chii ndo akakanyagwa na Tembo?
Wamejuaje kama alikua Jangili?
 
Mbuzi kafia kwa muuza supu Bwana Simba

You are strong than what you think...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…