Janga la njaa: UN yashauri watu wale wadudu

Janga la njaa: UN yashauri watu wale wadudu

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
Ugali%2Bsenene.jpg


Umoja wa Mataifa (UN) umeshauri kula wadudu wengi ili kukabiliana na janga la njaa. Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Chakula na Kilimo la UN, kula wadudu wengi kunasaidia kuongeza virutubisho mwilini na pia kupunguza uharibifu wa mazingira.

Tayari watu zaidi ya bilioni mbili duniani wanakula wadudu kama sehemu ya mlo wao. Hata hivyo, UN imekubali kuwa bado kuna watu wengi hasa kutoka nchi zilizoendelea ambao wanaona kinyaa kula wadudu.

UN imesema kuwa kwa sasa wadudu kama manyigu na kombamwiko wanatumika kwa uchache sana kama sehemu ya mlo. Ripoti hiyo imesema kuwa wadudu wapo kila sehemu na wanazaliana kwa wingi sana lakini hawatumiki kama chakula.

Waandishi wa ripoti hiyo wanadai kuwa wadudu wana virutubisho, hasa protini, mafuta na madini. Wanadai wadudu ni muhimu sana kama chakula hasa kwa watoto ambao hawapati lishe ya kutosha.

Ripoti hiyo imeshauri kuwa sekta ya chakula inaweza kusaidia kwenye kampeni ya kula wadudu kwa kujumuisha recipes mpya za wadudu katika vyakula vyao na kuongeza wadudu kama menu kwenye mahoteli.

Uko tayari kula wadudu kama kombamwiko (mdudu wa jamii ya memde) kama sehemu ya mlo wako?
 
mdudu mbona dayl tunakandamiza.?(kitimoto)

back frm jf jail.
 
Ulaji na uzaji wa senene, kumbikumbi, majongoo, mchwa, beetles na wadudu wengine sasa umetambuliwa na Umoja wa Mataifa. Ni kutokana na nafasi yake katika kutatua matatizo ya lishe na njaa duniani.
Ni dhahiri sasa tunaweza kuwauza nje ya nchi na kuingiza fedha za kigeni. Hongereni wa Mkoa wa Ziwa kwa ugunduzi huu kwani uchumi wa Taifa unaweza kupaa. Kilo moja inaauzwa 1.5- 2.0 US dollar nchini Kenya.


Kumbikumbi.jpg



dudu.jpg
 
Niliona twitter nikashangaa. There is nothing wrong kula wadudu kama ni tamaduni zenu au taste zenu. but people should not eat them to reduce the number of hungry people. what's next? eat grass just to reduce the number of hungry people?
 
Unatupiatu mazaga kama mabaagaa yan ilatu yacchafue tumbo ukaanza kuhara au kutapika bt full kuchana mwili.
 
Du hii kali!kumbikumbi huliwa lakini mpaka mende nimechoka.
 
Hii inategemea sana, kuna watu wanaweza ona offense kwa maneno haya.

Kuna makabila yanakula wadudu for some reasons iwe utamu, njaa, dawa wanajua wenyewe
Wadudu ni pana kidogo, mie nagonga kumbi kumbi na senene kama kawa
Lakini hujanilisha prawns,

images


seafood muscle,


images


sijui Lobster

images
 
Wakati wa kula Wadudu ni sasa' Un

Umoja wa Mataifa unasema watu duniani watalazimika KULA WADUDU ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula

Unadhani chakula kimekwisha duniani kiasi cha watu kutakiwa kula wadudu kama sehemu ya lishe bora?
source:
Habari - BBC Swahili
 
hii inategemea sana, kuna watu wanaweza ona offense kwa maneno haya.

Kuna makabila yanakula wadudu for some reasons iwe utamu, njaa, dawa wanajua wenyewe
wadudu ni pana kidogo, mie nagonga kumbi kumbi na senene kama kawa
lakini hujanilisha prawns,

images


seafood muscle,


images


sijui lobster

images
Kongosho wantamanisha bure shost napenda sana hao wadudu
 
Last edited by a moderator:
nilikula kumbikumbi mara ya mwisho nikiwa na miaka 6.........na sasa mimi ni m'bibi.....huoni itanishinda.......?

Labda uliacha kuwala baada ya kusoma ile hadithi ya kisa cha samaki kuishi majini?

"Hapo zamani za kale samaki waliishi nchi kavu. Waliishi kwa kula wadudu kama vile panzi, mende na sisimizi.

Siku moja wadudu hawa walikaa kikao na kupanga namna ya kuwaondoa samaki. Katika kikao chao wengi
walichangia.

Ikafika zamu ya sisimizi. Sisimizi alisimama na kusema, "umoja ni nguvu na utengano ni
udhaifu".

Wote walisimama na kupiga kelele, "samaki wauaweee".

Samaki waliposikia hivi walikimbia na kujificha majini.

Hadi hivi leo samaki wanaishi majini."

http://www.uwezo.net/wp-content/uploads/2012/08/TZ_2010_DistrictRankingSheet.pdf

cc. Kongosho
 
Last edited by a moderator:
images
hili naweza nikalichokonoa.........

images
lakini hawa hunilishi.........
 
He he he, mie sigusi

Afu hii hadithi naenda kuisimulia leo

Labda uliacha kuwala baada ya kusoma ile hadithi ya kisa cha samaki kuishi majini?

"Hapo zamani za kale samaki waliishi nchi kavu. Waliishi kwa kula wadudu kama vile panzi, mende na sisimizi.

Siku moja wadudu hawa walikaa kikao na kupanga namna ya kuwaondoa samaki. Katika kikao chao wengi
walichangia.

Ikafika zamu ya sisimizi. Sisimizi alisimama na kusema, "umoja ni nguvu na utengano ni
udhaifu".

Wote walisimama na kupiga kelele, "samaki wauaweee".

Samaki waliposikia hivi walikimbia na kujificha majini.

Hadi hivi leo samaki wanaishi majini."

http://www.uwezo.net/wp-content/uploads/2012/08/TZ_2010_DistrictRankingSheet.pdf

cc. Kongosho
 
Mie nikikuta watu wanakula kitu chochote na wako fit, na mimi ntakula tu!
 
wadudu ni watamu sana kama kumbikumbi ,senene hata mende watu tule tu tutapata afya .Angalia Wachina, Wajapani na Wakorea wanapenda kula wadudu wa baharini,nyoka na samaki . Unaona walivyo na akili na kupenda kufanya kazi kwa bidii. sisi waafrika tunapenda kula nyama nyekundu tu ndio maana tunapenda kuwa wavivu na tunapata magonjwa mengi sana na kunenepa ovyo. wadudu na samaki ni poa sana. Karibu kwetu tutakukaribisha kumbikumbi kwa ugali. au mende kwa ndizi.
 
Back
Top Bottom