Janga kubwa lanyemelea taifa ukame, jangwa

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,712
1,906
Ndg zangu wana JF wapenda nchi yetu ya TANZANIA, hebu tukae tutafakali kuhusu hili janga kubwa la ukame.

Ukiangalia kwa macho ya kawaida utaona mambo ni kama kawaida, lakini kwa ukweli halisi Tanzania tunavamiwa na jangwa kwa kasi ya ajabu.

Hali halisi ni kwamba kila mahali watu wanajenga majumba, kama hapa Arusha maeneo yote ya mji majumba yanajengwa.

Maana yake ni nini kila mahali miti inakatwa kupisha ujenzi, na hiyo miti inayokatwa hakuna miti mbadala inaya pandwa.

Maeneo yote, nenda Burka Estate, Tengeru Mandera INST, Dory Farm hizo ni taasisi kubwa zinazo jengwa within Arusha. Kuna watu binafsi wananunua maeneo na kujenga miti inaangushwa. Miti mikubwa ya asili, ambayo watu walitumia kupumzika au kufanyia vikao, miti yenye umri wa miaka zaidi ya mia moja.Miti iliyo toa chemichemi za maji inaangushwa ovyo, ni chain saw tuu huko vijijini miti chini!!!!! Sasa tutapanda lini miti ifidie hiyo inayo poromoshwa chini.

Huo ni mfano wa Arusha tuu!!!

Lakini Tanzania yote mambo ni yaleyale kufyeka miti yote. Hivi kweli hiyo hewa ya oxigen itatoka wapi wakati miti yote ya kutoa hiyo hewa tunaifyeka, mvua zitatoka wapi??????????? !!!

Kwenye mbuga za Ngorongoro walikopewa Waarabu mambo ni mabaya zaidi, miti yote imekatwa hata ya asili, fikiria huko miti hiyo hata tukipanda itachukua muda gani kustawi ili kusigeuke jangwa na ukame huu wa kila leo???????????Ngororo ni jangwa tayari!!!

Inawezekana tukaanza kudhibiti kwa sasa ili tuweze kuponyesha hata vizazi vyetu vijavyo, kuepusha jangwa!!!!!

Serikali hasa wizara ya Aridhi Nyumba na maendeleo mijini waanzishe kauli mbiu ya kupanda miti kuokoa taifa. Nchi nzima kuanzia Lindi na Mtwara hadi Tanga,Musoma Mara, Mwanza, Kagera,Kigoma, Mbeya Mikoa yote kazi iwe moja kupanda miti!! Mikoa yote iwe kwenye mchakato maalumu wa kupanda miti kila eneo, hata kwenye ukame miti ipandwe na kunyeshea maji kila asubuhi na jioni. Watoto wetu tuwafundishe kupanda miti na kuitunza, mtu aone uchungu kukata miti ovyo.

Mabonde makubwa kama Ihefu, Ngono (Kagera Basin) yapandwe miti ili kutunza aridhi iweze kutunza maji tupate mvua za uhakika. Tusibweteke tufikirie maisha yetu na vizazi vya baada ya sisi vitaishi wapi??????????

Mliye karibu na Waziri wetu Prof Tibaijuka jamani mkumbushe huo wajibu, maana yeye ni mtaalamu katika nyanja hiyo na ni eneo lake atusaidie, hatua madhubuti zichukuliwe tuepuke janga la ukame!!!!!!!!!!!

Zitungwe sheria village by laws, kama zipo zisimamiwe ipasavyo ili watu wasikate miti ovyo kwa kutoa kitu kidogo kwa ma VEO na ma WEO. Janga hili ni la kitaifa, mifano halisi imeisha anza kujitokeza migao ya umeme maji pungufu kwenye mabwawa yetu, mwisho yatakauka kabisa.

Kuchimba migodi wawekezaji, mzingira yanahalibika ovyo.Hata wachimbaji wadogowadogo kuwe na taratibu za kuokoa mazingira. TUPANDE MITI KILA MAHALI TUJIOKOE NA JANGA LA UKAME!!!!!!!!!!


An honest witness tells the truth,a dishonest witness tells nothing but lies. Proverbs: 14: 5.

 
10 percent ipi tena???????

Hujui,? Huo mradi watu watataka wakae kwenye vikao na semina;miti ioteshwe ikaguliwe, isafilishwe n.k; waombe fedha za wafadhili; hata kwenye uhai wao watu wanataka wafadhili
 
Hujui,? Huo mradi watu watataka wake kwenye vikao na semina;miti ioteshwe ikaguliwe, isafilishwe n.k; waombe fedha za wafadhili; hata kwenye uhai wao watu wanataka wafadhili
Very sorry was on the positive side of thinking, kumbe unatengenezea wenzio ulaji!!!!!!!!!!
Si mladi kazi hiyo ifanyike tuokoe nchi yetu?????????Wafadhiri si ndo vizuri wakague kama kazi imefanyika au la??????????
 
Ni wazo zuri ulilo nalo,lakini I am sorry to say it's too late.

Halafu the culprit is not who you think he is,Kukata miti,kwa upumbavu wetu tumedanganywa na kuamini kwamba ndiko tatizo.Kwa bahati mbaya kabisa, hata wasomi wameingizwa mkenge kabisa!Tatizo limeletwa na heating up of the ionosphere by using ELF waves. Hii ime disturb system nzima including that of the atmosphere and hence the changes we see,including climate change.

Facilities kubwa za kutoa ELF waves wanazo Wamarekani. Hizi zipo Alaska mahali panapoitwa Gakona.Mradi wenyewe unaitwa High Frequeny Active Auroral Research Programme(HAARP). Facilities zingine ndogo wanazo Warusi na European Union.

Changes zinazoletwa na kukata miti ni ndogo wala zisingekuwa na impact kubwa kiasi hiki tunachokiona.
 
Ni wazo zuri ulilo nalo,lakini I am sorry to say it's too late.Halafu the culprit is not who you think he is,Kukata miti,kwa upumbavu wetu tumedanganywa na kuamini kwamba ndiko tatizo.Kwa bahati mbaya kabisa, hata wasomi wameingizwa mkenge kabisa!Tatizo limeletwa na heating up of the ionosphere by using ELF waves.Hii ime disturb system nzima including that of the atmosphere and hence the changes we see,including climate change.Facilities kubwa za kutoa ELF waves wanazo Wamarekani.Hizi zipo Alaska mahali panapoitwa Gakona.Mradi wenyewe unaitwa High Frequeny Active Auroral Research Programme(HAARP). Facilities zingine ndogo wanazo Warusi na European Union.Changes zinazoletwa na kukata miti ni ndogo wala zisingekuwa na impact kubwa kiasi hiki tunachokiona.
Naomba utufafanulie zaidi hayo maswala ya kisayansi bwana ecologia.Kwenye red!!!!!!
Inahitajika tujue maana, naona sehemu zenye miti mingi mvua vile vile ni nyingi !!!
 
Naomba utufafanulie zaidi hayo maswala ya kisayansi bwana ecologia.Kwenye red!!!!!!
Inahitajika tujue maana, naona sehemu zenye miti mingi mvua vile vile ni nyingi !!!

Naomba uelewe hapa kwamba kinacho ongelewa ni equillibrium na rate of change.Equllibrium imekuwa disturbed tena makusudi and hence the rapid rate of change.Kwa hiyo hata zile sehemu zilizokuwa na mvua nyingi sasa ni kidogo sana au hamna kabisa.The rate of change has been accelerated by mankind himself by intentionally manipulating the ecosystem.Wanatumia kukata miti kama scapegoat.Najua ni vigumu sana to come to terms na maelezo haya, kwa vike tumekuwa brainwashed kwa muda mrefu sana.
 
Back
Top Bottom