ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 643
- 1,603
Siku ya watu wenye ulemavu; Tuondoe vikwazo.
Utangulizi
Leo tarehe 3 Disemba, Duniani kote wadau mbalimbali wanaadhimisha siku ya watu wenye ulemavu. Siku hii hutumika kutathimini jitihada za kuweka mazingira sawa kwa kupangua vikwazo vilivyowekwa dhidi ya kundi hili muhimu, jitihada hizo ni pamoja na kushawishi umuhimu wa Sera, Sheria na Kanuni za kiutawala na kiuongozi ili kuzingatia mahitaji mahususi, kuondoa vikwazo na kutoa fursa sawa kwa kundi la Watu wenye Ulemavu kushiriki kwenye maamuzi, maendeleo na majukwaa mbalimbali.
ACT Wazalendo kupitia Msemaji wa Sekta ya Ustawi na Maendeleo ya jamii, inachukuliwa siku hii kwa umuhimu mkubwa kwa kutathmini uelekeo wa kisera kwa kuangalia hali halisi ya nafasi ya kundi hili katika jamii yetu, vikwazo vinavyozuia ushirika wao na namna (mapendekezo) ya kuongeza jitihada za kukabiliana na ubaguzi, unyanyapaa na kuachwa nyuma kwa kundi hili kwenye masuala yote yanayowahusu kama sehemu ya jamii.
Idadi ya watu wenye ulemavu katika jamii haipaswi kupuuzwa Takwimu za kimataifa kwa mfano Shirika la Afya Duniani (WHO), linakadiria kwamba asilimia kumi (10%) ya watu katika kundi lolote la jumuia wana ulemavu wa aina fulani.
Kwa Tanzania kwa mujibu wa Sensa ya mwaka (2012) ilionyesha asilimia 5.9 ya watu wote wana ulemavu ambao ilikuwa sawa na milioni 2.6. Idadi hiyo inajumuisha watu wenye aina mbalimbali za ulemavu; Ulemavu wa vioungo, wasioona, wasiosikia, wenye ulemavu wa akili na wenye ulemavu mchanganyiko. Kati yao asilimia 59 ni wanawake.
Wakati tunatathmini hali ya kundi hili changamoto kubwa ni Ubaguzi dhidi ya walemavu, ambayo ni unyanyasaji ulioratibiwa dhidi ya walemavu, matendo na imani zinawaona kama duni wakilinganishwa na watu wengine. Ubaguzi dhidi ya ulemavu unaathiri elimu, huduma ya afya, na kila sekta ya jamii. Unaweza kuwa ukosefu wa uwezo wa kutembea au ukosefu wa viwezeshaji katika mifumo ya usafiri wa umma, miundo ya majengo au hata mitazamo ya makusudi.
Takwimu zinaonyesha licha ya jitihada zinazofanywa katika ngazi mbalimbali Lakini bado changamoto zinazoikabili kundi hili ni kubwa na wazi wanaachwa nyuma. Mathalani Inakadiriwa kuwa asilimia 20 ya watu maskini zaidi duniani wana aina fulani ya ulemavu. Watu wa vijijini wanaoishi na ulemavu wanakabiliwa na changamoto zaidi kuliko wenzao wa mijini.
Aidha, katika sekta ya ajira na kazi Shirika la kazi duniani (ILO) linasema idadi ya watu wenye ulemavu kwenye nguvu kazi ni ndogo. Takwimu zinaonyesha duniani kote ni watu 7 wenye ulemavu kati ya 10 hawako kwenye ajira wengi wao wakiwa ni wanawake, ikilinganishwa na watu 4 kati ya 10 wasio na ulemavu.
Tanzania Takwimu za watu wenye uwezo wa kufanya kazi (2021) zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya watu wenye ulemavu wapo nje ya mfumo wa uzalishaji yaani hawana kazi.
Vilevile, kwenye eneo la uwiano wa upatikanaji wa huduma kama vile afya ni changamoto kubwa. Ushahidi mpya umedhihirisha kuwa watu wenye ulemavu wako hatarini zaidi kukumbwa na vifo vya mapema au magonjwa mengine kuliko watu wasio na ulemavu. Aidha, mazingira ya utolewaji wa huduma kutokuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu.
Hili pia lipo katika sekta ya Elimu, kwa mujibu wa ESDP (2016/17 – 2020/21), kuna wastani wa watoto 400,000 wenye umri wa kwenda shule wenye ulemavu nchini Tanzania. Hata hivyo, ni watoto 42,783 tu waliosajiliwa katika shule za msingi na watoto 8,778 tu waliosajiliwa katika shule sekondari.
Hii inapelekea kuwepo kwa kundi kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi walio nje ya mfumo wa elimu, ikiwa ni pamoja na wasichana na wavulana wenye ualbino, tawahudi, down-syndrome, viziwi, wasioona, viziwi wasioona, watoto viwete na wenye matatizo ya akili.
ACT Wazalendo tunaona hali ilivyo sasa kuna uhusiano wa karibu sana kati ya ulemavu na umaskini, watu wenye ulemavu wanakosa fursa za kupata huduma za msingi, fursa za ajira na kazi, kuwepo kwa ushirika mdogo kwenye shughuli za uchumi, kijamii na utamaduni. Hivyo, kwenye kuadhimisha siku ya watu wenye ulemavu katika muktadha watanzania ni muhimu kuweka mkazo kwenye maeneo yafuatayo ili kuvunja vikwazo, kutoa fursa sawa na kukuza ushirika wao kwenye shughuli za kuwaingizia kipato;
i. Katika upatikanaji wa huduma muhimu kama vile afya, Elimu na Mafunzo Serikali itoe kipaumbele kwa kundi hili kwa kuondoa vikwazo vya kifedha na ugharamiaji.
ii. Tunatoa wito kwa Serikali kusimamia sheria ya watu wenye ulemavu katika kuhakikisha haki ya kupata ajira na kuzuia ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu kazini.
iii. Kusimamia vizuri mikopo ya Halmashauri kwa kundi la watu wenye ulemavu kama ilivyokusudiwa na Sheria ya mwaka 1982.
iv. Kuna umuhimu wa kukusanya na kutunza takwimu za watu wenye ulemavu katika utumishi wa umma, sekta binafsi na maeneo mengine ya huduma;
Kwa kuwa ACT Wazalendo tunaamini Ulemavu sio kulemaa, bali wanachohitaji watu hawa ni ujumuishwaji pamoja na kuwapo miundombinu rafiki na mahsusi itakayowawezesha kutimiza azma iliyokusudiwa ya kuwapatia maendeleo endelevu kama ilivyo kwa watu wa makundi mengine.
Sisi ACT Wazalendo tunaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na jamii ya kimataifa, kikanda na kitaifa kwa ajili ya kundi hili la Watu wenye ulemavu ambalo yamekuwa yakichagiza fursa zaidi na kuwa na jamii jumuishi zisizowaacha nyuma.
ACT Wazalendo tunaikumbusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba wachukue wajibu wao kwa kufanyia mabadiliko Sera ya Watu wenye ulemavu ya mwaka 2004 kwa kuwa imepitwa na wakati na haiendani na mazingira ya sasa tuliyomo.
ACT Wazalendo tunaamini Sera hiyo ikibadilishwa na kutungwa mpya basi Tanzania tutakuwa tumepiga hatua kubwa ya kulenga kuhakikisha kundi hili la Watu wenye Ulemavu linaondokana na mwenendo wa kudhani kuwa fursa kwa watu hawa si haki yao baki ni ihsani.
Tunawasihi Watanzania kuachana na unyanyapaa wa aina yoyote kwa Watu wenye Ulemavu badala yake ni kuungana pamoja na kuweka hamasa ya kupiga vita aina yoyote ya unyanyapaa nchini mwetu.
Imetolewa na;
Ndg. Janeth Joel Rithe
Msemaji wa Sekta ya Ustawi na Maendeleo ya jamii, wanawake na watoto,
ACT Wazalendo
03 Disemba, 2022.