Jana nilitangaza rasmi nia yangu ya kugombea ubunge jimbo la Singida Mjini

ADRIAN

Senior Member
Dec 31, 2012
113
27
cdm.png

TAARIFA YA NDG MUTTA, Anselimi KWA WANASINGIDA NA WATANZANIA KWA UJUMLA.

Ndg, waandishi wa habari mliohudhuria hapa, ndg. Viongozi wa chama wa ngazi mbali mbali mlioko hapa, ndg wageni wote mabibi na mabwana. Karibu katika mkutano wangu huu leo tarehe 6.4.2015 ambao una agenda mbili tu muhimu.
Ndg waandishi wa habari, namshukuru Mungu wangu leo hii nipo hapa nazunguza na nyinyi kwani tarehe ya leo kwangu ni ya kipekee katika historia ya maisha yangu. Nakumbuka ilikuwa tarehe 6 April 2014 majira ya saa 7 mchana nikiwa natokea DODOMA kuhudhuria kikao cha CHADEMA cha kanda ya kati ambayo inaunganisha mikoa ya SINGIDA, DODOMA NA MOROGORO, NILIPATA AJALI PALE BAHI hatua chache kabla ya kuingia wilaya ya Manyoni.
Katika ajali hiyo nilipata maumivu makali, nilipata jeraha kwenye bega langu la mkono wa kulia ambalo hadi sasa imebaki kuwa kumbukumbu yangu ya harakati za kuwakomboa watanzania wenzangu wanaoishi maisha ya mateso chini ya utawala ccm. Nachokumbuka ni kwamba, nilipoteza fahamu mara kwa mara hadi saa kumi (10) alfajiri ndipo nilipoanza kujitambua kuwa nilikuwa nimeumia sana kwani hata shingo haikuwa inageuka vizuri.

Ndg waandishi wa habari, baada ya kupata ajali hiyo wasamalia wema waliinichukua na kunipeleka kwenye dispensary iliyoko hapo BAHI ambapo nilipatiwa huduma ya kwanza na hatimaye nurse aliyekuwepo alipompigia simu dada yangu JESCA D. KISHOA ambaye kwa sasa ni mke wa mhe David Kafulila na hatimaye makamanda wenzangu akina DAVID DJUMBE, SHABAN LYIMU waliponifuata na kunihamishia kwenye hospatali ya mkoa wa DODOMA kwa matibabu zaidi.

Wakati nipo hapo Hospitalini nilipatiwa matibabu na hatimaye kuruhusiwa na kurudi Singida ambapo niliendelea na dawa nilizopewa huko hospitalini. Kwa ufupi hicho ndicho kilitokea na leo hii natimiza mwaka mmoja tangu ninusurike kifo kutokana na ajali hiyo.

Ngd waandishi wa habari, waswahili wanasema "Kufa, kufaana" katika ajali hiyo niliibiwa simu moja aina ya Tecno L3 yenye thamani ya Tsh 165,000/= kwa bei niliyonunulia, niilibiwa Tsh elfu 50,000/= kutoka kwenye pochi yangu na nilibakiwa na simu moja dogo pamoja na elfu 16000/= nilizokuwa nimehifadhi kwenye mfuko mwingine. Ila ninachoshukuru nilipona na ninaendelea kuchapa kazi zangu vizuri za kujenga chama na shughuli zingine za kijamii.

Ndg waandishi wa habari, katika kukumbuka tukio hili leo tarehe 6 April 2015, napenda NITANGAZE NIA YANGU RASMI YA KUGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA. Natangaza kugombea ubunge kwani sifa, vigezo na uwezo wa kufanya hivyo ninao, naweza kuwatumikia wananchi wenzangu katika jimbo hili. Endapo chama kitaniamini kikaniteua niko tayari kupambana kuhakikisha tunapata ushindi wa viti vya udiwani, ubunge na urais kwa wagombea wa wa CHADEMA / UKAWA. Na endapo sijateuliwa mimi akateuliwa mwingine, ntamuunga mkono ili tushinde.

Mimi ni mwanachama hai niliyejiunga na chama hiki toka mwaka 2010 hadi sasa na kadi yangu ya uanachama ni CDM NO. 0266461.

Ndg Waandishi wa habari, napenda nitumie fursa hii kuwashukuru wote walionisaidia wakati nimepata ajali hiyo wakiwa ni pamoja na:-

1. NDG. SHABAN LYIMU - MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA SINGIDA.
2. DAVID DJUMBE - MTIA NIA WA UBUNGE SINGIDA KASKAZINI.
3. JESCA KISHOA - KAMANDA WA CHADEMA.
4. WAFANYAKAZI WA SINGIDA SEKONDARI.
5. NA WOTE WALIONITAKIA HERI WAKATI WOTE.

Mwisho kabisa naomba wananchi wa Singida Mjini waniunge mkono ili tuweze kupanda mbegu yenye kuchipua na kuzaa fikra mpya ndani ya jimbo letu na kuachana na fikra za sahani za wali na usafiri wa maroli.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

………………………
MUTTA, Anselimi
Mtia Nia Ubunge – Chadema jimbo la Singida Mjini.
0784 462 729
0767 462 729
E-mail:muttabkm@gmail.com
 
Pole na hongera kwa ujasiri kamanda, nchi hii inahitaji watu wazalendo na majasiri kama wewe.... Komaa
 
View attachment 241042

TAARIFA YA NDG MUTTA, Anselimi KWA WANASINGIDA NA WATANZANIA KWA UJUMLA.

Ndg, waandishi wa habari mliohudhuria hapa, ndg. Viongozi wa chama wa ngazi mbali mbali mlioko hapa, ndg wageni wote mabibi na mabwana. Karibu katika mkutano wangu huu leo tarehe 6.4.2015 ambao una agenda mbili tu muhimu.
Ndg waandishi wa habari, namshukuru Mungu wangu leo hii nipo hapa nazunguza na nyinyi kwani tarehe ya leo kwangu ni ya kipekee katika historia ya maisha yangu. Nakumbuka ilikuwa tarehe 6 April 2014 majira ya saa 7 mchana nikiwa natokea DODOMA kuhudhuria kikao cha CHADEMA cha kanda ya kati ambayo inaunganisha mikoa ya SINGIDA, DODOMA NA MOROGORO, NILIPATA AJALI PALE BAHI hatua chache kabla ya kuingia wilaya ya Manyoni.
Katika ajali hiyo nilipata maumivu makali, nilipata jeraha kwenye bega langu la mkono wa kulia ambalo hadi sasa imebaki kuwa kumbukumbu yangu ya harakati za kuwakomboa watanzania wenzangu wanaoishi maisha ya mateso chini ya utawala ccm. Nachokumbuka ni kwamba, nilipoteza fahamu mara kwa mara hadi saa kumi (10) alfajiri ndipo nilipoanza kujitambua kuwa nilikuwa nimeumia sana kwani hata shingo haikuwa inageuka vizuri.

Ndg waandishi wa habari, baada ya kupata ajali hiyo wasamalia wema waliinichukua na kunipeleka kwenye dispensary iliyoko hapo BAHI ambapo nilipatiwa huduma ya kwanza na hatimaye nurse aliyekuwepo alipompigia simu dada yangu JESCA D. KISHOA ambaye kwa sasa ni mke wa mhe David Kafulila na hatimaye makamanda wenzangu akina DAVID DJUMBE, SHABAN LYIMU waliponifuata na kunihamishia kwenye hospatali ya mkoa wa DODOMA kwa matibabu zaidi.

Wakati nipo hapo Hospitalini nilipatiwa matibabu na hatimaye kuruhusiwa na kurudi Singida ambapo niliendelea na dawa nilizopewa huko hospitalini. Kwa ufupi hicho ndicho kilitokea na leo hii natimiza mwaka mmoja tangu ninusurike kifo kutokana na ajali hiyo.

Ngd waandishi wa habari, waswahili wanasema "Kufa, kufaana" katika ajali hiyo niliibiwa simu moja aina ya Tecno L3 yenye thamani ya Tsh 165,000/= kwa bei niliyonunulia, niilibiwa Tsh elfu 50,000/= kutoka kwenye pochi yangu na nilibakiwa na simu moja dogo pamoja na elfu 16000/= nilizokuwa nimehifadhi kwenye mfuko mwingine. Ila ninachoshukuru nilipona na ninaendelea kuchapa kazi zangu vizuri za kujenga chama na shughuli zingine za kijamii.

Ndg waandishi wa habari, katika kukumbuka tukio hili leo tarehe 6 April 2015, napenda NITANGAZE NIA YANGU RASMI YA KUGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MJINI KWA TIKETI YA CHADEMA. Natangaza kugombea ubunge kwani sifa, vigezo na uwezo wa kufanya hivyo ninao, naweza kuwatumikia wananchi wenzangu katika jimbo hili. Endapo chama kitaniamini kikaniteua niko tayari kupambana kuhakikisha tunapata ushindi wa viti vya udiwani, ubunge na urais kwa wagombea wa wa CHADEMA / UKAWA. Na endapo sijateuliwa mimi akateuliwa mwingine, ntamuunga mkono ili

Mimi ni mwanachama hai niliyejiunga na chama hiki toka mwaka 2010 hadi sasa na kadi yangu ya uanachama ni CDM NO. 0266461.

Ndg Waandishi wa habari, napenda nitumie fursa hii kuwashukuru wote walionisaidia wakati nimepata ajali hiyo wakiwa ni pamoja na:-

1. NDG. SHABAN LYIMU - MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA SINGIDA.
2. DAVID DJUMBE - MTIA NIA WA UBUNGE SINGIDA KASKAZINI.
3. JESCA KISHOA - KAMANDA WA CHADEMA.
4. WAFANYAKAZI WA SINGIDA SEKONDARI.
5. NA WOTE WALIONITAKIA HERI WAKATI WOTE.

Mwisho kabisa naomba wananchi wa Singida Mjini waniunge mkono ili tuweze kupanda mbegu yenye kuchipua na kuzaa fikra mpya ndani ya jimbo letu na kuachana na fikra za sahani za wali na usafiri wa maroli.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

………………………
MUTTA, Anselimi
Mtia Nia Ubunge – Chadema jimbo la Singida Mjini.
0784 462 729
0767 462 729
E-mail:muttabkm@gmail.com
Mkuu mimi nilidhani wakati wa kutangaza nia unatangaza na vipaumbele vyako. Sasa wewe sehemu kubwa ya kutangaza nia unaelezea ajali na pia kwamba dada yako sasa ni mke wa Mh. David Kafulila!

Pia naona unatoa masharti kwa Chama kwamba kikikuteua utakuwa tayari kupambana kuhakikisha mnapata ushindi wa udiwani, ubunge na urais kwa wagombea wa chama/ukawa; kama hutateuliwa utamuunga tu mkono atakayeteuliwa! Ungesema hata kama hutateuliwa bado utahakikisha unapambana ili chama kishinde ubunge, udiwani na urais.

kila la kheri.
 
Kwa hiyo kupata ajali ndo sifa ya kuwa mbunge?
Au unatafuta huruma ?

Uwe mwelewa............. Kwanza utambue ajali yenyewe aliipata akiwa katika harakati za kuipigania chama, na amesema amejitathmini anazo sifa zote za kuwa mbunge, na bado kasema atakuwa tayari kumuunga mkono yeyote atakayepitishwa na chama kugombea.
 
Mkuu mimi nilidhani wakati wa kutangaza nia unatangaza na vipaumbele vyako. Sasa wewe sehemu kubwa ya kutangaza nia unaelezea ajali na pia kwamba dada yako sasa ni mke wa Mh. David Kafulila!

Pia naona unatoa masharti kwa Chama kwamba kikikuteua utakuwa tayari kupambana kuhakikisha mnapata ushindi wa udiwani, ubunge na urais kwa wagombea wa chama/ukawa; kama hutateuliwa utamuunga tu mkono atakayeteuliwa! Ungesema hata kama hutateuliwa bado utahakikisha unapambana ili chama kishinde ubunge, udiwani na urais.

kila la kheri.

Agenda za jana zilikuwa mbili tu.

Mambo mengine yatatangazwa wakati wa mchakato rasmi. Unachotakiwa kujua kwa sasa ni kwamba ametangaza nia
 
Kwamba agenda ilikuwa ajali na kusema atagombea basi. Lakini hilo la ajali limechukua nafasi kubwa isiyo ya lazima.
 
Mkuu mimi nilidhani wakati wa kutangaza nia unatangaza na vipaumbele vyako. Sasa wewe sehemu kubwa ya kutangaza nia unaelezea ajali na pia kwamba dada yako sasa ni mke wa Mh. David Kafulila!

Pia naona unatoa masharti kwa Chama kwamba kikikuteua utakuwa tayari kupambana kuhakikisha mnapata ushindi wa udiwani, ubunge na urais kwa wagombea wa chama/ukawa; kama hutateuliwa utamuunga tu mkono atakayeteuliwa! Ungesema hata kama hutateuliwa bado utahakikisha unapambana ili chama kishinde ubunge, udiwani na urais.

kila la kheri.

Mkuu. Hana hoja huyu dogo, mwache akajipange kwanza...
 
Uwe mwelewa............. Kwanza utambue ajali yenyewe aliipata akiwa katika harakati za kuipigania chama, na amesema amejitathmini anazo sifa zote za kuwa mbunge, na bado kasema atakuwa tayari kumuunga mkono yeyote atakayepitishwa na chama kugombea.
Kamanda Mungi usiwe too defensive, msaidieni mwenzenu jinsi ya kufanya wasilisho. Sasa kwa mfano hiyo habari ya dada yake ambaye ni mke wa Kafulila ina maana gani hapo? Nilidhani baada ya dada kupigiwa simu alitoa msaada, kumbe msaada ulitolewa na makamanda wenzake. Kulikuwa na haja ya kumtaja dada yake hapo? Au anataka kuonyesha kwamba Kafulila ni shemeji yake?
 
Last edited by a moderator:
Singida hakuna wa kumtoa Mohamed Dewji, ni kama rais wa Singida, Dewji amewaletea wana singida maji,barabara kwa kutumia pesa zake mwenyewe, Singida sasa hivi ni kama Dubai
Mkuu wapo watakaomtoa kwani ni demokrasia ila atatoka ccm pekee
 
Singida hakuna wa kumtoa Mohamed Dewji, ni kama rais wa Singida, Dewji amewaletea wana singida maji,barabara kwa kutumia pesa zake mwenyewe, Singida sasa hivi ni kama Dubai

Dewji abaki na hela zake, tunachohitaji ni uwakilishi wa wana singida mjini bungeni.
 
sasa huyu mtu ambaye ubongo wake umetingishika jamani. Kweli tumpe ubunge kweli???? Sio aibu nyingine hii

Mkuu kwanini usitulie alafu pumbazako ukaziweka kwenye comment moja kuliko kujaza server kwa viji comment hivyo?,au tukuachie pekeyako?.Au kuna jamaa yuko kisogoni kwako?
 
Back
Top Bottom