Jana kidogo niwape askari wa usalama barabarani walichokuwa wanataka kwangu, nilijikuta naichukia Serikali kwa kiwango kibaya sana

Hujanielewa mkuu Jana na Leo siku zote izo nilikua safarin natoka mkoa narud dar sio kwamba nilikua mjin kwaio matatizo yote yamenikuta wakat niko njian kurud mjin
Sasa wewe ndugu yangu gari haina bima unaitembeza mchana bila uoga tena ukiwa highway safarini?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ulihisi mapai ni baba zako wadogo na mashangazi au?
 
Hutakiwi kuendesha gari isiyo na bima kwahio ukilimwa fine Sawa, ukikamatwa tena unaendesha bila bima unalimwa tena na ingekuwa nchi za wengine walioendelea wangechukua Hilo gari wakaenda kuliponda scrap yard na wewe ungeenda jela kwa kurudia kosa.
Hata mimi nilikua bingwa wa majibu kama haya kwenye matatizo ya watu ila kwakua mimi yamenikuta basi hata wewe jiandae.
 
Mkuu una uhakika ni hii ya siku saba?! Kwamba unaruhusiwa kuendesha bila bima kwa siku saba,likitokea la kutokea nani anabeba dhamana?!
Mkuu, sikuzote linapo tokea lolote kuhusu bima kimsingi ni wewe mhusuka ndie utakae wajibika kama unayo bima ama hauna bima.

Sikuzote linapo tokea swala lolote kwenye gari lako, polisi ujihusisha kwa kuangalia na kuidhinisha mwenye kosa. Na swala la dhamana ama kuwajibika/malipo ni lako wewe na bima husika.

Hii ya siku saba iliwahi kunitoke mimi mwenyewe na nikapewa onyo kwa mdomo.
 
Mie nilinusurika kutiwa nyavuni pale kamata nikatia akili. Toka siku ile gari nikawa naitoa jioni tu kuelekea usiku mpaka nilipokata bima upya hivi karibuni.
 
Hata mimi nilikua bingwa wa majibu kama haya kwenye matatizo ya watu ila kwakua mimi yamenikuta basi hata wewe jiandae
Unataka nikujibu unavyopenda kusikia? Bima sio kitu cha mchezo mchezo. Kama hujijali wewe kata third party ulinde wengine wewe upambane na hali yako.

Bima haiishi ghafla unajua kabisa lini inaisha kama hujakaa vizuri paki gari.
 
Aisee haya mkuu, leo nimejifunza Bima ina 7 days grace period! Amazing
 
Mkuu - kutembea na gari iliyokwisha bima ni kosa, hiyo ni haki uadhibiwe, ila sio kwa kiwango hicho ulichofanyiwa. Huyo Trafiki aliekuita "MBWA" ; na yeye alifanya makosa, ulitakiwa either na wewe umuadhibu hapohapo; au umpeleke mbele - hata kumfungulia mashtaka kwa kosa la kukuita wewe mbwa. Sidhani kama alishawahi kukukuta ukibwaka, mpaka akuite "MBWA".
 
Mie nilinusurika kutiwa nyavuni pale kamata nikatia akili. Toka siku ile gari nikawa naitoa jioni tu kuelekea usiku mpaka nilipokata bima upya hivi karibuni.
Ni heri kutembea bila leseni, lakini sio bima.
 
Siku nyingine kuwa mwanaume, ulipaswa uchukue namba zao za vitambulisho vya upolisi, ungeziweka hapa ungeona jinsi ambavyo wangeshughulikiwa, hao ni traffic wapuuzi wachache wanaoharibu taswira ya jeshi la polisi, wanapaswa kushughulikiwa kama waharifu wengine. Hivyo usiilamu serikali wala chama chetu cha CCM, hao ni waharifu kama walivyo waharifu wengine ambapo huwezi kusema vijana wote wezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…