TUSHIRIKISHANE JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

Aug 9, 2016
13
67
Mtandao wa JamiiForums.com umezindua rasmi mradi wa unaowashirikisha viongozi wa kuchaguliwa(hususani wabunge na madiwani), Serikali(Halmashauri) na Wananchi katika kurahisha upatikanaji wa maendeleo.

Mradi huu unaotambulika kama "Tushirikishane" una malengo ya kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi.

Pia Tushirikishane inalenga kuzisaidia Halmashauri kuboresha utoaji huduma za jamii kwa ufanisi zaidi. Mwitikio(maoni, ushauri na kero) wa wananchi katika mnakasha wa Jimbo/Halmashauri utachukuliwa kwa umakini na viongozi hawa ili kuhakikisha mrejesho unatolewa kwa wananchi.

Akizungumza mbele ya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba Mjini, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na Mwanzilishi-Mwenza wa mtandao wa JamiiForums.com, Bwana Maxence Melo aliwapongeza viongozi wa Wilaya, watendaji wa Halmashauri, Madiwani na Mbunge kwa mwitikio mkubwa walioonyesha katika kuupokea mradi wa Tushirikishane.

Maxence aliwafahamisha kwamba Mradi huu utatekelezwa katika majimbo sita (6) kwa kuanzia na Bukoba Mjini limekuwa Jimbo la kwanza katika kuanza utekelezaji wake. Jimbo la Pili katika mradi huu limekuwa la Nzega, litafuatiwa na la Kigoma mjini na kisha Sengerema. Majimbo ya Mtama, Kigamboni na Arumeru Mashariki yatafuatia.

Alifafanua kuwa mradi huu utachukua miezi 9 na hivyo Wabunge wanaohusika kwenye mradi huu wanatakiwa kukubaliana na wananchi juu ya ahadi zisizozidi 4 za kuweza kuwa sehemu ya mradi huu zinazoweza kutekelezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa mradi huo.

Bwana Maxence pamoja na timu yake ya wataalam walikuwa Bukoba Mjini kwa siku tano kuendesha warsha iliyowawezesha wadau kuuelewa mradi kwa ufasaha, kutambua majukumu yao na kujua njia zitakazotumika katika kutekeleza mradi kwa faida yao.

Warsha ya Tushirikishane ilifanyika Bukoba Hotel na wadau wanaowakilisha Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Wapiga kura na wananchi wa Bukoba Mjini, Madiwani wa vyama vyote pamoja na Mbunge wa Jimbo walishiriki.

Malengo ya Tushirikishane

Pamoja na lengo kuu tajwa hapo juu, Mradi huu una malengo mahususi yafuatayo:
i. Kupanua wigo wa mawasiliano kati ya Wananchi na viongozi wa kuchaguliwa na serikali yao (kwa njia ya mtandao, magazeti, redio, televisheni na mikutano ya wazi)
ii. Kurahisisha upatikanaji wa habari na taarifa za umma zikiwa kwenye lugha rahisi
iii. Kuchochea majadiliano ya wazi, yenye tija na staha kati ya wananchi na viongozi wao
iv. Kusaidiana na viongozi wa kuchaguliwa katika kutengeneza nyenzo za muhimu katika kutekeleza ahadi.​

Matarajio ya Mradi

Shughuli za Mradi huu zinatarajia kuchangia katika mabadiliko ya muda mfupi na muda mrefu kwenye tasnia ya uongozi wa Uwakilisha nchini Tanzania. Miongoni mwa matarajio hayo ni:

i. Kujengeka kwa utamaduni wa majadiliano yenye staha kati ya viongozi na wananchi kwenye mitandao ya kijamii
ii. Kuboreshwa kwa mfumo wa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi katika utekelezaji wa sera na ahadi za wakati wa Uchaguzi.
iii. Kuongezeka kwa ufanisi katika utekelezaji wa sera na ahadi za kipindi cha uchaguzi.​

JamiiForums itakuwa inakuletea matukio yote kuhusiana na mradi huu kwa kadiri utekelezaji wake utakavyokuwa unaenda katika kila Jimbo.

Nukuu toka kwa Maxence akimjibu Kichuguu:
Tupo Nzega tayari. Tutamaliza baada ya siku 3 zijazo.

Tunafanya upembuzi kwanza kubaini kama wananchi wanatambua majukumu ya Mbunge na kama wanakumbuka ahadi zake. Aidha, tunafuatilia kama wanafahamu wajibu wa Halmashauri kwao na wajibu wa madiwani kwao.

Tuna mengi tumeona na tumewahamasisha wananchi katika kuyapata maendeleo katika maeneo yao. Bahati wananchi wanatuelewa na viongozi wao wanauona mwitikio wa wananchi katika maeneo tunakopita.

Mradi huu upo katika hali ya majaribio (pilot project) na lengo la awali lilikuwa ni kuufanya katika majimbo matatu kwanza lakini mwitikio wa waheshimiwa wabunge ulipelekea nasi kujisogeza na kujikuta idadi inaongezeka zaidi.

Nafasi za ajira ya Afisa Mawasiliano ambaye atakuwa anatuwakilisha katika kila jimbo zilitangazwa hapa JamiiForums katika jukwaa la Nafasi za Kazi.

Kukiwa na ufanisi katika hatua hii ya awali, tutajisogeza zaidi (scale-up) na kufanya katika majimbo zaidi na tutajitahidi tukatafuta wahisani ili mradi uweze kuwafikia wengi na kuongeza tija zaidi.

Mbunge, Halmashauri na wananchi watakaofanya vema watatuzwa mwishoni mwa mradi (top 3).

=========
KATIKA PICHA:

image.jpeg

image.jpeg

Hatua ya awali katika uzalishaji wazo.

image.jpeg

image.jpeg

Timu ya Jamii Media ilipoenda Dodoma kuwashirikisha wabunge juu ya wazo la mradi

IMG_7629.JPG

Timu ya Jamii Media ikitambulishwa mbele ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Bukoba.

Baraza Bukoba.jpg

Baraza la Halmashauri ya Bukoba, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Pamoja na Timu ya Jamii Media katika picha ya Pamoja

Diwani.JPG

Diwani wa Kata ya Bakoba, Mhe. Mwakyoma akiwasilisha kundi lake juu ya Wajibu wa Mbunge kwa wapiga kura wake.

Max na madiwani.JPG

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media akibadilishana mawazo na waheshimiwa madiwani Kalumuna(katikati) ambaye ni diwani wa Ijuganyondo(CCM) na Kabaju (kulia) ambaye ni diwani wa Kashai(CHADEMA).

image.jpg

Mbunge wa Bukoba Mjini, akishirikiana na wapigakura wa Jimbo lake katika zoezi la kuchambua kazi na wajibu wa mbunge kwa wapiga kura wake.

IMG_7631.JPG

Mbunge wa Bukoba Mjini, Mhe. Wilfred Lwakatare akijibu baadhi ya maswali na kutolea ufafanuzi hoja zilizotoka kwa wapiga kura.

Max mafunzo.JPG

Mkufunzi akitoa maelezo juu ya matumizi sahihi ya mtandao wa JamiiForums.

Makubaliano.jpg

Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane.

image.jpeg

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo akimkabidhi kitendea kazi mwakilishi wa JamiiForums (Afisa Mawasiliano) katika Jimbo la Bukoba Mjini, Bi. Happiness Essau

washiriki bukoba.JPG

Washiriki wa Warsha ya Tushirikishane katika Jimbo la Bukoba Mjini wakiwa katika picha ya pamoja.

=======
NZEGA:
image.jpeg

image.jpeg

image.jpeg

Warsha ikiendelea katika Ukumbi wa Lake Tanganyika
image.jpeg

Sheikh na Mchungaji nao walishiriki

image.jpeg

Picha ya pamoja na washiriki toka Nzega. Waliokaa ni madiwani

Kuhusu mjadala na taarifa za kinachojiri katika majimbo husika tembelea

TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigoma Mjini

TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

TUSHIRIKISHANE | Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Mtama
 
Hii ni hatua kubwa kabisa kuwahi kutokea.

Mkuu Max big up sana, na nnakuunga mkono kwa asilimia 100.

Nipo Mnyusi nawasiliana na wadau pale kilimani Potwe najaribu kuhamasisha ili elimu ienezwe kila mahali.
 
Back
Top Bottom