screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,829
- 15,791
Kwa miaka kadhaa ambayo nimekuwa member wa JF nimeweza kuexperience mambo yafuatayo;-
1. Anacho komenti mtu wa kwanza kwenye post maranyingi huwa ndio msimamo wa wengine wanaofatia kukomenti ( yaani wengi ni wafata upepo). Wakwanza kukomenti akikuponda na wengine watakuponda, wakisifia na wengine watasifia.
2. Unaweza ukatukanana na mtu kwenye thread hii then mda huohuo ukamgongea like kwenye thread nyingine na kummwagia sifa kibao.
3. Kwavile tunatumia Fake ID's, si ajabu ukajikuta unabishana na bosi wako na kumvimbia kwamba unahela sana na unauwezo hata wa kuajiri ukoo wao mzima, pia unaweza ukamuita babaako 'dogo' au 'boya' bila kujua.
4. Ukienda kwenye jukwaa la Vyombo vya usafiri unaweza fikiri kila mwana JF anamiliki gari, tena gari kali. Maana ukiulizia VITZ unaambiwa uwe mvumilivu uendelee kujikusanya ununue 'GARI', na uachane na vi'baby-walker'.
5. Ukienda MMU Wanaume wote wanajifanya 'MANDINGO', hakuna anayekubali kwamba yeye kibamia, na akianza kupiga gemu goli 1 ni kuanzia dakika 30, hakuna anayemaliza kwa dakika 5. Hilo ni kwa upande wa wanaume, kwa wanawake wao kila mmoja ni 'MNATO', hakuna Mtera kule.
6. Ukienda kule jukwaa mama 'SIASANI' yaani ndio vurugu tupu, kila mtu anajiona jiniazi na ndio maana ni jukwaa linaloongoza kwa povu. Utasikia "hizo hoja zako za kitotototo peleka kwa watoto wenzio facebook".
7. Watumiaji wa JF wanadhani kila mtu yuko Dar. Hata wanapoweka matangazo yao unaona kabisa akilini mwao wanajua kila mtu anaishi Dar.
8......
9......
10......
Mengine ongeza wewe...