Jamii yasisitizwa kushiriki michezo

Jamii yasisitizwa kushiriki michezo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Mei 21, 2023 jijini Dar es Salaam amefungua wiki ya michezo kuelekea Siku ya Afrika Mei 25, 2023 iliyoandaliwa na Umoja wa Wanadiplomasia wa Afrika.

Akifungua michezo hiyo Mhe. Chana ameisisitiza Jamii kushiriki katika michezo na mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasioambukiza pamoja na kulinda afya zao.

"Mhe. Rais Samia ameshatuelekeza kufanya mazoezi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, hivyo nasisitiza jambo hili kifanyika na kusimamia ipasavyo. Nawashukuru Wanadiplomasia Hawa kuunga mkono juhudi hizi za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuandaa siku hii ya michezo hongereni sana" amesema Mhe. Chana.

Bonanza hilo la michezo limeshirikisha timu za mpira wa miguu za watoto wa mabalozi, timu ya wake wa mabalozi na timu ya mabalozi dhidi ya timu ya Wizara ya Mambo ya Nje.View attachment 2630294View attachment 2630295View attachment 2630297View attachment 2630299View attachment 2630296View attachment 2630298
IMG-20230521-WA0004.jpg
 
Back
Top Bottom