JF sio forum ya kulani- mafisadi, mambo ya vita dhidi ya ufisadi ni kipengele kimoja tuu kati ya vingi ndani ya-JF, ni Jukwaa la Siasa. Vipenhele vingine vingi bado vipo. Hata vita vikiisha mambo mengine kibao muhimu yatapata nafasi nzuri mfano ni hoja ya kila Mtanzania ni tajiri, anatakiwa kumiliki gari, kuwa na nyumba nzuri na kuishi vizuri ikiwa ni pamoja na kula vizuri na kupata starehe. Tatizo hapa sio mafisadi, ni mfumo wa uchumi uliopelekea wachache wamiliki mali na wengi wahangaike.jF inatakiwa ikusaidie wewe usie na nyumba, gari na pesa za kutosha na ziada ya kununulia stock ili kubadili maisha yako, yangu na yake kwa kifupi maisha yetu. Sio suala la ufisadi ni zaidi ya hapo,. Hii ndio JF ijayo baada ya vita na 2010 kupita salama.