Jamhuri: Pinda agongana na bilionea Dar!

Jamhuri: Pinda agongana na bilionea Dar!

Ilikuwa yule wa HSC, leo Lake Oil, huu utamaduni wa kiarabu...

Arusha, kilimanjaro,Mara wanafanyiana unyama zaidi huu kila kukicha mpaka Polisi wameugawa Mkoa wa mara kwa uhalifu. Alex Masawe na Papaa Masofe wamefanya nini fuatilia. Je ni waarabu? Wale wanaoitwa Mabilionea wa Arusha walio uwawa kinyama waliuwawa na Waarabu? Wale Wafaransa walio uwawa znz nakufukiwa ktk kisima je Waliuwawa na waarabu. Acha kuchafua watu wengi humu wameadika uhalifu wa mtu 1 wa jamii fulani usichukuliwe kama ni wa jamii nzima.
 
Arusha, kilimanjaro,Mara wanafanyiana unyama zaidi huu kila kukicha mpaka Polisi wameugawa Mkoa wa mara kwa uhalifu. Alex Masawe na Papaa Masofe wamefanya nini fuatilia. Je ni waarabu? Wale wanaoitwa Mabilionea wa Arusha walio uwawa kinyama waliuwawa na Waarabu? Wale Wafaransa walio uwawa znz nakufukiwa ktk kisima je Waliuwawa na waarabu. Acha kuchafua watu wengi humu wameadika uhalifu wa mtu 1 wa jamii fulani usichukuliwe kama ni wa jamii nzima.

Kula like kubwa
 
Ilikuwa yule wa HSC, leo Lake Oil, huu utamaduni wa kiarabu...

Mtu mwenye akili Kama zako ni rahisi sana kahadaiwa na kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile
 
Mimi siamini kama unyama huu unaweza kufanyika hapa Tanzania
 
Mtu mwenye akili Kama zako ni rahisi sana kahadaiwa na kukubali kuingiliwa kinyume na maumbile

mimi itakuwa vigumu si nimeshawashtukia, wewe sasa ambaye unawachukulia poa.....
 
pinda hiyo yote nguvu ya soda muhindi imekula kwake labda asaidiwe na wahindi wezake coz hata watu weus tuna kesi kama hzo nyingi tu polis hazifanyiwi kaz,kawaulize wananch wa mbarali wanavyopata taabu kama wahamiaj kwenye ardh za mama zao
Kwani ally ameshawalawiti waswahili pia ila hao wanaona aibu kuji peruzi ktk vyombo vya habari aibu jamani kwetu huu mchezo wa kulawitia
 
kweli CCM inakazi kubwa ya kufanya, maisha haya mtu hawezi kufanyiwa unyama hivyo asikamatwe
 
Ibia mwarabu huponi lazima akufunze adabu, bora muhindi ingawa nao hutumia sana ndumba...huyu mtu afikishwe kotini haki itendeke,ntashangaa sana kama Pinda atakaa kimya nitaamini nchi inaongozwa na wenye fedha hao hao ndio watakaogaramia kampeni za hicho chama. CCM hapa ndio tutawapima kwa weledi wenu
 
hivi uislamu unaruhusu bilionea mwisilamu alawiti ,waislamu wenzake wanashangilia na anafadhili misikitini yeye na swahiba wake badae wanaenda kula 0713 za mwanaume mwenzao it shame

- Ni Ally Awadh wa kampuni ya mafuta ya Lake Oil
- Atuhumiwa kumfanyia unyama mtumishi wake
- Polisi Oysterbay, Kanda Maalumu wamgwaya

Jumanne, Februari 11, 2014

Mlalamikaji anayedaiwa kupigwa na mabaunsa wa mfanyabiashara bilionea Ally Awadh (Lake Oil)

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua “kujipima uzito” dhidi ya bilionea Mtanzania, Ally Edha Awadh ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Lake Oil ya Mikocheni jijini Dar es Salaam inayoagiza, kuuza na kusafirisha mafuta na biashara nyingine nyingi.Awadh anayetajwa kama mmoja wa mabilionea vijana nchini, amefunguliwa mashitaka Polisi ya kumteka, kumdhalilisha kinyume cha maumbile na kumpora mali mmoja wa wafanyakazi wake.

Uamuzi wa Waziri Mkuu Pinda umekuja baada ya Jeshi la Polisi nchini, katika kile kinachoonekana ni kumgwaya bilionea huyo, kupuuza kumsaidia mlalamikaji huyo mwenye umri wa miaka 32. Kwa sababu za kiutu na za kitaaluma, jina la mlalamikaji tunalihifadhi kwa sasa.

Hatua ya Pinda imetokana na barua ya mlalamikaji ya Novemba 29, mwaka jana aliyomwandikia baada ya Jeshi la Polisi-kuanzia Kituo cha Oysterbay, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na hata Makao Makuu, kupuuza kumsaidia mlalamikaji ili aweze kutendewa haki.

Baada ya kuipata barua ya mlalamikaji, Pinda alimwagiza msaidizi wake, Leila Mgonya, amwandikie barua Katibu wa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kazi hiyo ilifanywa Desemba 29, mwaka jana.

Katika barua hiyo ya Pinda iliyoandikwa kwa niaba yake na Mgonya, inasema, “Miongoni mwa mambo aliyofanyiwa mlalamikaji na mwajiri wake (Awadh) ni pamoja na kupigwa na kujeruhiwa mwili mzima kama picha zilizoambatanishwa na barua ya mlalamikaji zinavyoonyesha, kudhalilisha pamoja na kudhulumiwa mali zake kama inavyobainishwa katika barua ya mlalamikaji.

“Kwa kuwa suala hili limejikita zaidi katika utendaji wa Jeshi la Polisi, imeelekezwa kuwa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ishughulikie suala hili kikamilifu kwa lengo la kumsaidia mlalamikaji kupata haki yake kwa mujibu wa sheria na kuona kuwa haki inatendeka.

“Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu angependa kupata mrejesho kuhusu suala hili. Tafadhali mfikishie Mheshimiwa Waziri maelekezo hayo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu.”
Pamoja na maagizo hayo ya Waziri Mkuu, JAMHURI imebaini kuwa hakuna hatua zozote za maana zilizokwishachukuliwa dhidi ya Awadh na washirika wake.

Barua ya mlalamikaji kwa Waziri Mkuu

Mlalamikaji katika barua yake kwa Waziri Mkuu, anaanza kwa kusema, “Mheshimiwa, jina langu lipo hapo juu ni kijana wa Kihidi (Mtanzania) umri wangu ni miaka 32 mzaliwa wa Tanga, nina mke na watoto.

“Mheshimiwa, nimesomea uhasibu na nimefuzu mwaka 2004 masomo yangu… na nikaajiriwa na Ally Edha Awadh katika kampuni yake iitwayo Lake Oil Ltd Septemba, 2010 na kuwa Finance Manager (Meneja Fedha) katika kampuni yake.

“Bila matarajio yangu, ilipofika Mei 2, 2013 mwajiriwa mwenzangu aitwaye Ahmed alifika ofisini kwangu na kuniarifu ya kwamba naitwa na Mkurugenzi Ally Edha, ilikuwa saa 11:30 za jioni Alhamisi na bila kusita nikaongozana naye hadi kwa Ally Edha nikifahamu naitwa kwa ajili ya kazi kiofisi.

“Nilishangaa nilipofika tu ofisini kwake akahitaji simu yangu, nikampa mara akamuagiza stafu mwingine aitwe Fahim akafuate laptop yangu na vifunguo ya gari yangu ofisini kwangu na ofisini kwake tulipobaki mimi, yeye na Ahmed. Alianza kunitukana na kuniambia mimi ni mwizi nimemwibia dola milioni 10 za Marekani (Sh bilioni 16).

Mara ilipoletwa laptop yangu na funguo za gari akanichukua na kuniagiza nimfungulie e-mail yangu. Nilikataa na kumwambia hii ni mail yangu binafsi na siyo ya ofisi yake, siwezi kufungua pana kazi za wateja wangu wengine (mimi ni mhasibu wa wengi). Akanitishia kunipeleka Polisi, nami nikamkubalia.

“Mheshimiwa, tukifuatana na wafanyakazi wake wengine, Ahmed, Fahim, yeye na K.V Choudry, tulishuka chini na kuingizwa katika gari ya Ahmed. Gari ikawashwa na mara akamuagiza dereva Ahmed lile gari tulilopanda lipelekwe godown (ghala) ili abadilishe gari kwenda Polisi. Cha kushangaza nikaamrishwa nishuke pale godown na kuingizwa ndani, pamoja na wale tuliofatana nao. Nilishangaa kuwakuta wengine wawili (yeye Ally Awadh anadai ni mabaunsa wake) wanaitwa Waitey na mwingine ni Abeid.

Mabaunsa waanza kumlawiti

“Mheshimiwa, wakajumuika pamoja wakanivua nguo, wakanilawiti. Wakanipiga sana kwa kutumia nondo, mikanda mizito, makonde ya nguvu na huku huyo mtumishi mwenzangu Ahmed akiwa ameielekeza pistol (bastola) kichwani kwangu kwa kuniambia leo ni kifo changu endapo nitakataa kuyakubali anayotaka bosi wake, yaani Ally.

“Mheshimiwa, mateso haya yalikuwa zaidi ya masaa mbili na nusu (zaidi ya saa mbili na nusu) nikilazimishwa nikubali kutoa kila kitu changu (assets) nimpatie yeye, vinginevyo wataniua na wakanionesha picha za maiti wawili zilizokuwepo katika simu ya baunsa wake akidai (Ally) angeniua kama hao, na kunifunga katika mfuko wa plastiki na kunipeleka shambani kwake Soga kunizika.”

Mlalamikaji anaendelea kumweleza Waziri Mkuu kwamba kutokana na mateso makali na vitisho alivyopewa, alilazimika kukubaliana na maelekezo aliyopewa, yote hiyo ikiwa ni mbinu ya kunusuru uhai wake.

Apigwa picha akiwa uchi

“Ndipo Ally Edha akanipiga picha nikiwa uchi na kusema endapo nitaenda Polisi, yeye atazitoa hizo picha kwenye mitandao ya intaneti kunidhalilisha. Hivyo nikapewa shati langu nivae na kupelekwa ofisini kwake na kulazimishwa niandike kukubali kwamba vitu vyangu vichukuliwe,” anasema.
img-20130504-wa0009.jpg


Mlalamikaji anayedaiwa kupigwa na mabaunsa wa mfanyabiashara bilionea Ally Awadh (Lake Oil)


Kwa mujibu wa mlalamikaji, mali zilizochukuliwa ni:

A: Nyumba yangu na mke wangu iliyopo Nairobi, Kenya
B: Gari zangu mbili (i) Toyota IST T786 BZG (ii) Toyota Fortuner T503 BQC
C: Bastola yangu 6mm niliyonunua Mzinga.
D: Fedha taslimu dola 100,000 (Sh zaidi ya milioni 160)
E: Mkataba wangu wa nyumba na duka (vyangu) vilivyoko Uhuru Heights
F: Ofa zangu tatu za viwanja Kigamboni

Asainishwa kwa nguvu

“Ndipo nikasainishwa; na majira ya saa 3 za usiku wakanitia katika gari aina ya Navara nyekundu mali ya kampuni –dereva akiwa Ahmed wakiwamo mabaunsa wawili, Ally Edha, na mimi. Hadi nyumbani kwangu Upanga.

“Mheshimiwa, inasikitisha kwa sababu mke wangu alipopiga simu nikiwa kwa Ally alinilazimisha niongee na mke wangu kwa lugha ya Kiingereza, na siyo Kihindi. Alikuwa anapiga kwa kutoamini kwa nini niongee Kiingereza badala ya Kihidi hadi simu ikaisha pesa ndipo tulipofika tukamkuta yupo chini anangoja aletewe vocha na mlinzi.

“Wakanibadilisha shati na kunivisha la Abeid (langu lilijaa damu). Wakamweka chini ya ulinzi mke wangu. Tukapanda juu nyumbani hadi sitting room wakamnyang’anya simu na kumkalisha chini. Ally Edha akanilazimisha nimpeleke bedroom (chumba cha kulala), ndiye akazichukua documents (nyaraka) zote na hizo pesa na mara wakaingia Choudry, Sree Kumar na Ramana ambao wote ni wafanyakazi wake; na ni Wahindi wakiwa na laptop na printer.

“Ghafla wakiwa na hizo laptop huyo Choudry na Kumar wakaelekezwa kuandika maneno ya mkataba ambayo mimi na mke wangu tukalazimishwa kuweka sahihi zetu kukubali kuzitoa mali zetu kwa huyo jambazi Ally. Nakumbuka hata watoto wanalia kutaka maziwa nyumbani Ally Edha alizuia wasipewe.”

Mlalamikaji anaendelea kusema kwamba akiwa na maumivu makali, Ally Edha alitaka siku ya pili amtolee pesa katika akaunti yake iliyopo katika Benki ya STANBIC, Tawi la Nyerere Road; na akasema angezifuata hizo fedha siku ya Jumamosi.

“Alizijua hizo fedha kwa sababu ni akaunti niliyoitumia kuweka pesa za mshahara. Mshahara wangu ulikuwa Sh. milioni 6 kwa mwezi. Kama hilo halikutosha, alikuta chumbani kwangu vitabu vitatu vya hundi za akaunti ya pamoja na mke wangu; Standard Chartered (Nairobi, 2), Benki ya Exim (3), Benki ya NBC, akatulazimisha tuzitie sahihi zetu- na tukafanya hivyo.”

Mlalamikaji, mkewe waonywa watauawa

“Siku hiyo aliniambia mimi na mke wangu kwamba kama angesikia tumemueleza mtu yeyote haya mambo, angetuua. Kweli tukaogopa sana hadi siku ya tarehe 4, 2013 ndipo alipomtuma Sree Kumar kuja kuchukua zile milioni 22 alizoagiza nizitoe katiba akaunti yangu ile siku ya tarehe 2 Mei 2013. Nilimkabidhi Sree Kumar akampelekea Ally Awadh.

“Mheshimiwa, nakumbuka namna tarehe 8 Mei, 2013 Choudry (Mfanyakazi wa Ally Awadh) alinitumia meseji mbili kwa kutumia simu yake kwamba angependa aje nyumbani waniletee pochi waliyochukua siku ya tukio nyumbani kwangu ambayo ni ya mke wangu yenye kadi yake ya ATM na kopi ya leseni ya udereva. Nikawaambia sitokutana nyumbani, tukapanga anikute Mtaa wa Morogoro/Jamhuri akaleta akanikabidhi bila ya kunisalimu.”

Danadana za Polisi Oysterbay

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, siku ya Jumamosi tarehe 4 Mei 2013 nilipatiwa wakili aitwaye Mwanganga. Nikamueleza, akaamua tukamuone RPC Kova (Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam). Tulifika saa za mchana, nikamueleza na nilipotaka kumwonyesha majeraha yangu alikataa na kusema kuangalia majeraha sio kazi yake ila alipiga simu Oysterbay akatuagiza twende. Tukafuatana na wakili hadi Oysterbay.

“Mheshimiwa, hiyo tarehe 4 Mei 2013 tulifika Oysterbay tukamuona ofisa mmoja simfahamu jina ila sura namfahamu (wakili wangu anamfahamu). Hakuonekana kujali sana, ndipo akatupeleka ofisi nyingine (wakili anaifahamu). Hapo huyo askari akamuita mama mmoja polisi ndipo akatupeleka ofisi nyingine, ofisa akamuagiza andike maelezo naye akanisikiliza na akanipeleka kwa ofisa mwingine. Huyo ndiye aliandika maelezo yangu.

“Cha kushangaza huyo ofisa alianza kusema ‘wewe tayari umetajwa kwenye kesi nyingie ya Lake Oil’, lakini tukamwambia aandike maelezo yangu. Yeye alidai ‘pana Mhimdi mmoja, Mukesh ambaye ni Internal Auditor (Mkaguzi wa Ndani) wa Lake Oil yupo ndani rumande hapo, na wewe pia unapaswa uwekwe ndani’. Lakini huyo ofisa na mwanasheria wangu walitoka nje. Cha kunishangaza wakili akanimbia eti inatakiwa niweke dhamana nikatibiwe ili Jumatatu nirudi au nipelekwe kutibiwa nirudishwe rumande. Lakini wakili baadaye alinifahamisha wameyamaliza- kampatia Sh 100,000; hivyo ningepaswa nimrejeshee hizo pesa.

“Hivyo statement (maelezo) iliandikwa na nikapewa medical examination report yenye case file no. OB/RB/7853/2013 ya tarehe 4 Mei, 2013. Ndipo nilipoenda Sinza Hospitali kwa matibabu.”

Woga wamfanya akimbilie Zanzibar

Mlalamikaji anasema kutokana na woga wa ahadi za mateso zaidi au kuuawa kama alivyoahidi Awadh, aliamua Mei 5 aende mafichoni Zanzibar.

“Tarehe 6 Mei nilipigiwa simu na Mutafungwa aliyejitambalisha kwangu kwamba yeye ni OCD wa Kinondoni akisema amesikitishwa kuisoma statement yangu na angependa kukuona. Hivyo nikarejea Dar es Salaam na tarehe 7 Mei nikaenda na kaka yangu na wakili wangu. Tukamwona, akaagiza kwa ofisa mwingine wa CID kumweleza hiyo kesi ni ya ukweli kwa hiyo wakamatwe wahusika mara moja na kuniagiza nishirikiane naye.

“Baada ya siku mbili, yaani Mei 9, nikapigiwa siku na Salum (CID Osysterbay) akanieleza yeye ndiye mpelelezi wa kesi yangu na angependa kuniona. Tahere 12 Mei nilimuona Salum. Kwa sababu ya kuwa Zanzibar ndiyo maana nilichelewa kumuona. Akanisikiliza na kusema angepeleleza hiyo kesi na angeniita.

“Mheshimiwa, kila mara huyu Salum hakunipa msaada ipasavyo kwa madai kwamba hajamuona Ally Edha. Nilishangaa sana sababu ofisi ya Ally Edha ipo, wanaijua na iweje waseme hawamuoni? Baada ya muda, katikati ya Mwezi wa Ramadhani, Salum aliniita na kuniambia mwenzake aitwae James angeweza kunisaidia kuipata silaha yangu kutoka kwa Ally na nikamuona huyo James ambaye aliahidi Ally Edha akirudi safari yake kwa asilimia 90 nitapata pistol (bastola) yangu. Akasisitiza pia akimuona siku ya kwanza tu Ally angenipatia hiyo bastola.”

Aombwa chochote akishasaidiwa

“Nakumbuka katikati ya Oktoba, mwaka jana Salum alinipigia simu akasema James anauliza endapo akinisaidia kuipata hiyo bastola mimi ningempa zawadi gani. Nikamjibu, ‘Nitampatia anachotaka’ ilimradi nipate bastola na vitu vyangu.
“Mheshimiwa, Nashangaa tangu wakati huo walipoanza kutaka chochote kwangu, hawajanipigia tena, wala kunisaidia.

Nami nilishajiandaa kuwakamatisha kwa rushwa. Nikaendelea kupata matatizo ya kujificha kwa kuamini Ally Edha ana mamlaka ndani ya Jeshi la Polisi na anaweza kunifanyia chochote atakacho.

“Mheshimiwa, Nikashauriwa niende kutoa taarifa Makao Makuu ya Polisi (wizarani). Hivyo tarehe 27 Novemba, mwaka jana nilienda huko nikamuona Bwana Laizer ambaye ni Kamishna. Nikamueleza na nikamuonesha vielelezo. Alisikitika sana na hapo alimuagiza RPC wa Kinondoni ashughulikie hilo jambo na amueleze kwa kila kinachoendelea.

“Hadi leo tarehe 29 Novemba, nimeamua nikatumie barua hii na vielelezo vyangu ili unisaidie, kwani polisi hawanisaidii tangu nifanyiwe unyama huu. Najiuliza na kujiona mkiwa kwa kuamini kwamba huyu Ally Adha Awadh yupo juu ya sheria? Iweje polisi wamlinde tangu Mei 2013 hadi leo pasipo kukamatwa? Mheshimiwa Naomba msaada wako.”

Barua hii ya mlalamikaji aliweza kupeleka nakala kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Utawala Bora, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa.

Kwa upande wake, Awadh amegoma kuzungumza na JAMHURI. Mara kadhaa amepigiwa simu yake, lakini amekataa kuzungumza hata pale simu ilipopokewa. Ametumiwa ujumbe kwa nyakati na siku tofauti, lakini hadi tunakwenda mitamboni alikuwa hajajibu.
Ujumbe mmoja ulisema, “Habari za kazi.

Hapa ni gazeti JAMHURI. Tuna habari za kesi ya … dhidi yako. Tunaomba kujua kama hili suala unalijua kabla hatujaichapisha. Tangu jana tunaomba utupatie majibu- bila mafanikio. Tumetekeleza wajibu wetu kitaaluma kwa hiyo hatustahili lawama. Mhariri”.

CHANZO: Gazeti la Jamhuri
 
hivi uislamu unaruhusu bilionea mwisilamu alawiti ,waislamu wenzake wanashangilia na anafadhili misikitini yeye na swahiba wake badae wanaenda kula 0713 za mwanaume mwenzao it shame
We khanit,hi umetoka wapi na kuingiza UISLAMU humu. Watu tushaongea humu way back we leo unakurupuka na genye mshindo zako na kutaja dini kwa ujumla wake wakati mtuhumiwa na jina umewekewa??????!!!!!

Unataka bwana kwa nguvu au nini????!!!!
Mgese sana wewe!!!!!
 
Punguza jazba uislamu huchukia mambo machafu je waislamu wenzangu ni sahihi mwenzetu kumlawiti mwenzake kwa kuwa yeye ni bilionea anauza mafuta na kununulia mashekh sendozi ,mwislamu atakae kaa kimya anaunga mkono vitendo vya kulawitiana ,hapa Tanzania sijawahi sikia mwislamu tajiri anakodi watu kwenda kulawiti ,tuige mifano ya kina bakhressa anatoa misaada kwa yatima,je waislamu wenzangu huyu mlawiti anatudhalilisha Kama Alubadili ipo tutaiona
 
Punguza jazba uislamu huchukia mambo machafu je waislamu wenzangu ni sahihi mwenzetu kumlawiti mwenzake kwa kuwa yeye ni bilionea anauza mafuta na kununulia mashekh sendozi ,mwislamu atakae kaa kimya anaunga mkono vitendo vya kulawitiana ,hapa Tanzania sijawahi sikia mwislamu tajiri anakodi watu kwenda kulawiti ,tuige mifano ya kina bakhressa anatoa misaada kwa yatima,je waislamu wenzangu huyu mlawiti anatudhalilisha Kama Alubadili ipo tutaiona

Unawezaje kuwa muislamu halafu ukasema kuwa mlawiti ni mwenzetu????!!!
Mnakutana wapi na mnashare interest gani mpaka useme "mwenzetu"????!!!

Hawezi kuwa mlawiti na.bado akawa muislamu kwa maana ya dini ya haqi; ashahadie kuwa hakuna mola apaswaye kuabudiwa kwa haqi isipokuwa Allah na mtume Muhamad(S.A.W) ni mjumbe wake!!!!!

Ulawiti hauwez kuwa ni matendo ya Muislamu anayeabudu kwa haqi huku akimtakia rehma mtume (S.A.W)!!!!!!!

Nb; Kama kweli alifanya hivyo basi huyu Allahu yaallam sidhani kama yupo kundini!!!!
 
Kama hayupo kundini mbona miskitini wanapokea misaada yake na kipindi cha ramadhani anafuturisha ,jamani tuwe makini tunafurahia matunda ya watu wachafu bila ayana kila kukicha yuko na kanzu na ijumaa msikitini anagawa kumi kumi kwa mashekhe zetu ,msikiti anaosali najiuliza nikasali ikumaa ijayo au? Kwani hata mazulia kanunua yeye,kipaza sauti kipya,AC Mpya kwa kweli naama msikiti
 
Kama hayupo kundini mbona miskitiniwanapikea misaada take na kipindi cha ramadhani anafuturisha ,jani tuwe makini tunafurahia matunda ya watu wachafu bili ayana kila kukicha yuo na kanzu ijumaa msikitini anagawa kumi kumi kwa mashekhe zetu ,msikiti anaosali najiuliza nikasali ikumaa ijayo au? Kwani hata mazulia kanunua yeye ,kwa kweli naama msikiti


Huwa unachunguza sadaka za watu wote???!!!!
Maadam umepata huo ufahamu(kama kweli) sasa hapo si unajua nini unatakiwa kufanya???!!!!

La huna hakika basi uliza kwa wanazuoni wenye ujuzi zaid juu ya hukmu ya hali hiyo!!!!!

Quran haikuacha any case in a pending status
 
Kwenye gari anatembea na kitabu kitukufu quran je hii ni sahihi ndugu zangu waislamu mtu mchafu mchafu ana beba kirahisi kuran yetu lazima tuandamane
 
Kwenye gari anatembea na kitabu kitukufu quran je hii ni sahihi ndugu zangu waislamu mtu mchafu mchafu ana beba kirahisi kuran yetu lazima tuandamane
Ushahidi wa zinaa ni mgumu ati sasa kwa nchi za sharia hili saa hizi lingekuwa historia tayari lakini huku vugu vugu ndio kama hivi!!!!!!!

Ukiandamana na kuambiwa utoe maegemezi utaanzia wapi maalim????
 
Tunangojea tamka kutoka kwa Kiongozi mkuu wa waislamu ,mpka sasa kakaa kimya inaonyesha karurahishwa na kitendo hicho wenzetu viongozi wao maaskofu wakuu washazungumzia wameeleza ni ukiukwaji wa haki za binadamu na wamefafanua ni hatua gani watazifuata na wametoa pole kwa familia je sisi tumefurahia na kuchekelea ulawiti
 
Tunangojea tamka kutoka kwa Kiongozi mkuu wa waislamu ,mpka sasa kakaa kimya inaonyesha karurahishwa na kitendo hicho wenzetu viongozi wao maaskofu wakuu washazungumzia wameeleza ni ukiukwaji wa haki za binadamu na wamefafanua ni hatua gani watazifuata na wametoa pole kwa familia je sisi tumefurahia na kuchekelea ulawiti

Viongozi wa kiislamu wa "dini" au wa."serikali" au "bakwata"!!!!
Hivi huwa.wapo???!!
 
Kwa nini muislamu alawiti anafundisha nini jamii ya kislamu ,anafundisha watoto wetu bilionea kulawiti ni ruksa,je angekuwa mwanao kalawitiwa ungefurahi kwa kuwa kalawitiwa na bilionea ,usiwe mahamuma ,uislamu ni usafi wa kila kitu kuanzia unavyoishi ,sio kupeleka maubwabwa misikitini ramadhani ,leo unalawiti
 
Back
Top Bottom