Jamhuri Kiwelo atimuliwa Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jamhuri Kiwelo atimuliwa Simba

Discussion in 'Sports' started by Kipanga, Oct 6, 2008.

 1. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna habari kuwa aliyekuwa kocha msaidizi wa timu kongwe ya soka Tanzania Simba Sports Club, Jamhuri Kiwelo (Julio Alberto) ametimuliwa. Kwa mujibu wa taarifa zilizorushwa hewani na kipindi cha michezo cha kituo cha radio cha TBC Taifa, baadhi ya wanachama wa Simba wanamshutumu Julio kwa kuyumbisha benchi la ufundi la Simba hali iliyopelekea timu hiyo kongwe kufanya vibaya katika mechi zake kadhaa za ligi ya Vodacom inayoendelea. Akihojiwa na mtangazaji wa TBC Taifa Philip Cyprian, Julio alisema yeye hababaishwi na maamuzi ya kutimuliwa kwake kwani siku zote Simba inapofanya vibaya basi lazima atafutwe mchawi na safari hii hali hiyo imemuangukia yeye..... Hii ndio soka yetu wadau
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Njaa mbaya sanaa....julio si atafute cha kufanya jamani kwani lazima kila siku iwe Simba tuu ,mbona wanamdhalilisha sana jamani.....anatia huruma sana Julio...................pole zako kaka
   
 3. P

  Paullih Member

  #3
  Oct 6, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Julio nimjuavyo mie ana kinyongo na kuwepo kwa kocha mkuu mzungu Simba ndio maana anaweza kufanya lolote kuhujumu timu. Hata katika moja ya kauli zake wakati akihojiwa baada ya mojawapo ya michezo alisema anasikitishwa sana na baadhi ya waandishi kutokuwathamini makocha wazawa na hukimbilia kwa wazungu kupata information.... Alisema hivi baada ya kocha mzungu kuuchuna kuzungumzia kipigo kimojapo cha timu hiyo na waandishi kumgeukia Julio.

  Julio ni kocha mwenye mafanikio makubwa na Simba na mara nyingi inapotokea ukata au timu kufanya vibaya mara nyingi viongozi na wanachama humwangukia na kumwomba aokoe jahazi. na amekuwa akifanya vyema.... sijui ni kwasababu ya mbinu zake za kiufundi au ni kwa maneno yake ya majigambo pale anapokaribia kukutana na timu fulani, hasa Yanga... na amekuwa akifanya vyema sana. Yanga watafurahia sana kutimuliwa kwa Julio.

  Simba walipopata kocha mwingine walipaswa kumweleza Julio na kumweka kando... kwani mafahari wawili hawalali zizi moja. Hili lingeondoa msuguano na kunyosheana vidole kama ilivyo sasa.

  Nilipata kuiona Simba katika mechi mbili za Kombe la ubingwa afrika mashariki... Kiwango ilichokionyesha kilikuwa cha juu mno na ni moja ya timu iliyoogopewa sana, si kwa jina lake bali kiwango cha ubora wake. Mojawapo ya mechi hiyo ni ile dhidi ya Tusker ya Kenya. kwahiyo hivi vipigo vinavyoiandama Simba vina sababu nyingine zaidi ya uwezo wa Timu uwanjani. Simba ile si ya kufungwa mfululizo na timu kama Azam au Ruvu JKT. Wachezaji ni walewale, na klabu ni ileile, kuna kitu... na kuondoka kwa Julio kunaweza kuwa ni Suluhisho pia.
   
 4. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Paullih,
  Lakini unadhani hii tabia ya hizi timu Simba au Yanga kila inapotokea kufungwa mechi 2 au 3 basi lazima lawama zitupwe kwa aidha makocha (na hasa wale wazalendo) au wachezaji kuwa kuna hujuma? litatufikisha wapi katika purukushani za kuinua kiwango cha soka hapa bongo? Mi nadhani viongozi, makocha, wachezaji, wanachama na mashabiki wafike mahali waelewe kuwa katika soka kufungwa ni sehemu ya mchezo kwani hata timu pinzani hata kama hazina majina bali nazo zina lengo la kupata ushindi. Tuache ila tabia ya kukariri kuwa zinapocheza Simba, Yanga na timu nyingine basi ushindi lazima. Tunaona katika ligi ya Uingereza ambayo nina imani idadi kubwa ya mashabiki wa soka Tz wanaifatilia Timu kubwa kama Manchester Utd, Liverpool, Chelsea au Arsenal hukumbana na vipigo na timu ndogo (Mfano hai Arsenal kufungwa na Hull City ) wiki iliyopita na viongozi, Kocha na wachezaji walikubali kuwa ni matokeo ya mpira. Mi kwa kweli inanitia huzuni kuona kuwa soka Tz inaendeshwa kienyeji sielewei hatima yake ni nini??
   
 5. M

  Masatu JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wakati mwingine Simba kama tumerogwa.... Julio ni muhimu pale ondoa zeruzeru bakisha Julio case closed...
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Oct 6, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Wanamtimua halafu baada ya muda anarudishwa tena baada ya inaosemekana wanachama kuuomba uongozi umsamehe duh hii kali

  lakini nimesikia kwamba ana offer ya kwenda azam fc pindi huyo mbrazil mkataba wake ukiisha au wakati wowote ule sasa inawezekana safari ndio hiyo ameshaanzishiwa
   
 7. P

  Paullih Member

  #7
  Oct 6, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kipanga unayosema ni kweli... ushindi hutokana na mikakati, nidhamu na umoja klabuni. kama hivyo hakuna timu itaboronga tu. Sijaiona hii ligi toka ianze ndio maana nimetumia mashindano ya Klabu bingwa afrika mashariki kama kigezo cha Simba kutakiwa kufanya vizuri kwani walionesha kandanda safi wakati ule. Labda walibweteka na timu nyingine zimekuja na mikakati ya ushindi.Nimefurahia post yako Bro!
   
 8. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2008
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani Simba inabidi itafakari kwa kina chanzo cha vipigo hivi vyote. Sidhani, na wala sikubali moja kwa moja kuwa Julio ndio chanzo cha yote. Mara ngapi hii timu Julio kaitoa kimasomaso katika matatizo makubwa ya kiufundi, tena kwenye mashindano makubwa, na bado akaiokoa!

  Hebu uongozi wa Kiswazi uliioota mizizi kwenye timu zetu kubwa kama Simba na Yanga uache taratibu zake za kuongoza soka Kiswazi na kibabaishaji.

  Nani kafanya uchunguzi tadidi wa kubaini kuwa chanzo cha yote ni Julio-stupid guys! Soka haliendeshwi hivi, ndo maana hatufiki popote. Ni huyu huyu Julio juzi tu kwenye mashindano ya CECAFA kaifanya Yanga iikimbie Simba, ambayo ilikuwa nii moto wa kuotea mbali chini ya Julio kwa mazoezi ya muda mfupi.

  Wakati wa soka la floani leo kaamka hivi, tayari anachukua maamuzi ya kipuuzi umepita. Hatujifunzi kwa wenzetu Wakenya ambo kocha mzalendo Francis Kimanzi kaifikisha Harambee Stars hap[o ilipo, na sasa karibu itafuzu kucheza kombe la mataifa ya Afrika na dunia, huku akiendelea na kuinoa timu yake ya Mathare.

  Siasa zetu ni stupidity, na soka nalo stupidity, eeh jaman, stress zetu tutazitolea wapi!!!
   
 9. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2008
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sio ndo huyu jamaa alishausishwa na ushoga, vipi tena apate heshima ya kuwa kiongozi wa timu? Labda kama yupo pale kwa masilahi ya watu.

  Nimemsikia mwenyewe jana kupitia mahojiano na TBC radio akisema yupo pale na riziki yake anapata hasa kwa viongozi wakubwa serikalini ambao ni wapenzi wa simba (JULIO) na sio kwamba anaitegemea timu sana
   
 10. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  eebanae siyo Julio tu hata Mzee Dalali kaachia ngazi baada ya kufanyiwa vituko nyumbani kwake leo akiwa mbele ya familia yake. Simba bana, wamekosa ustaarabu kabisa. Mtu mmemchagua kwa kura halafu mnaenda kumzomea nyumbani mbele ya familia yake. Mbaya sana.
   
 11. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Julio mwenyewe alishasema kuwepo kwake Simba ni kama "DAFU KWA MAANA HALINA MSIMU" kwahiyo hamna cha kushangaza muda wowote anaweza kurudi.
   
 12. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Simba na Yanga enzi zao zilipita bado wana desturi na mindset ya kizamani sana kiasi kwamba hawawezi kuendelea wanachukulia mpira kama ni burudani na wala sio kazi.
   
 13. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nyie simba mmekwisha tu wajameni, wacheni sisi yanga(wabrazil na wana ccm)tutese sasa, manake mmetunyanyasa kwa mda mrefu sana.lo.
   
 14. M

  Magehema JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2008
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nadhani mechi ya Simba na Tusker hukuiona ndugu yangu. Simba walicheza hovyo kupita kiasi, ni mechi ambayo Tusker walistahili kushinda kwa magoli mengi sana kuliko waliyoyapata, walishinda 3-2. Any way kimsingi hyo sio hoja, hapa hoja ni kwamba club zetu haziendeshwi professionally. Nini mchango wa mwanachama katika kuendelze kuendelza mpira? ni fujo tupu
   
Loading...