Yanga Bingwa wa Ubingwa wa Jamhuri ya Muungano 1983

Dec 17, 2019
19
41
Yanga ambayo ilikuwa nje ya mategemeo ya wapenzi wengi wa soka hapa nchini ya kuweza kuchukua Ubingwa wa Tanzania. Ilionyesha ushujaa wake wa kulisaka soka katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Small Simba ya Zanzibar ambapo yanga ilishinda kwa magoli 4-1 mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa. Yanga ilichukua ubingwa huo kwa mbinu ya hali ya juu kiasi hakuna mpenzi yeyote wa soka aliweza kutabili ushindi huo.

Yanga ilikuwa inashika nafasi ya tatu kabla ya michezo ya mwisho ya ligi hiyo. Yanga ilihitaji ushindi mkubwa dhidi ya Small Simba kuweza kuwa bingwa na hivyo ndivyo Yanga ilifanya ikiwa imetingisha wavu wa lango la Small Simba mara nne na hapo waliweza kupata uhakika wa kutwaa ubingwa huo.

Timu ya Yanga ilimaliza ligi ikiwa na alama 7 sawa na timu ya KMKM na Simba, lakini timu ya Yanga ilipata nafasi ya kuwakilisha Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika kwa magoli mengi ya kufunga.

Yanga bali na ubingwa, pia ilikuwa na rekodi safi ikiwa imefungwa mchezo mmoja tu kati ya jumla ya michezo ishirini iliyochezwa katika msimu huo na kuweza kutwaa Ubingwa wa Bara na Ubingwa wa Jamhuri ya Muungano.

Yanga ilianzamchezo huo kwa machachari huku wakiwa na lengo la kufunga magoli mengi. Yanga iliwachukua dakika tisa kuweza kupata bao la kwanza ambalo lilifungwa na Charles Boniface Mkwasa ambaye alikuwa nahodha waTimu ya Taifa na alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kuweza kufunga magoli matu na kuhusika kwenye goli la nne.

Boniface alipokea pasi ya juu toka kwa Juma Mkambi na bila kuusimamisha aliusindikiza hewani kwa mguu wa kulia. Bao hilo liliongeza moto wa Yanga na baada ya dakika tano Makumbi Juma aliuweka mpira wavuni lakini mwamuzi aliamua ameotea.

Katika dakika ya ishirini ya kipindi cha kwanza Small Simba iliweza kusawazisha bao lilifungwa na Suleiman Omar baada ya kupokea pasi kutoka kwa Rashid Khamis na kuachia mkwaju kutoka mita ishirini hadi wavuni.

Dakika ya thelathini na saba Abeid Mziba aliongeza bao la pili kwa upande wa Yanga. Dakika nne kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika , Yanga ilijihakikishia ushindi wa bao la tatu. Mfungaji wa bao hilo alikuwa Charles Boniface Mkwasa tena alifunga kwa ufundi sana. Alipokea pasi kutoka kwa Juma Kampla na akaruka juu kwa mbwembwe na kuweka mpira wavuni kwa kichwa.

Katika kipindi cha pili Yanga iliweza kuongeza goli. Goli hilo lilifungwa katika dakika ya thelathini na moja ya kipndi cha pili. Charles Boniface alipokea pasi ya chinichini kutoka kwa Hussein Iddi na akiwa amelala chini aliupitisha mpira katikati ya walinzi wa Small Simba na kuweka wavuni. Hadi kipen
IMG_0076.png

ga cha mwisho Yanga 4-1.

Kutokana na mchezo uliochezwa huko Zanzibar KMKM dhidi ya Simba ambao walitoka sare ya bila kufungana. Yanga alinyakulia Ubingwa wa Tanzania kwa kuwa na pointi saba, magoli nane ya kufunga na magoli manne ya kufungwa. Timu ya KMKM ilishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi saba magoli sita ya kufunga na magoli matatu ya kufungwa. Simba ilishika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi saba, magoli tano ya kufunga na magoli matano ya kufungwa. Small Simba ikashika nafasi ya mwisho kwa kuwa na pointi tatu, magoli ya kufunga manne na magoli kumi na moja ya kufungwa.
 
Kutokana na mchezo uliochezwa huko Zanzibar KMKM dhidi ya Simba ambao walitoka sare ya bila kufungana. Yanga alinyakulia Ubingwa wa Tanzania kwa kuwa na pointi saba, magoli nane ya kufunga na magoli manne ya kufungwa.
historia za akina KMKM, yaani Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo!
Jaribuni kuweka za giants kama Al Ahly, Zamalek, ASEC Mimosas, TP Mazembe, Hearts of Oak, Asante Kotoko, Hafia Conakry, Al Merrikh, Al Hilal, Raja Casablanca, Wydad Casablanca, Etoile De Tunis, Esperance, Mouloudia d'Oran, JS Kabylie, Simba SC, Mamelodi Sundowns, Kaizer Chiefs, Orlando Pirates, DC Motema Pembe, AS Vita Club, Africa Sports d'Abidjan, Enyimba, Stationery Stores FC, Canon Yaounde, Tonnere Yaounde, CARA Brazzaville nk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom