James Sinclair: A Friend or Foe?

Lets not nill down kwani hadi sasa kuna mabadiliko makubwa na hata wabunge wengine wanaelekea kuhoji juu ya jambo hili hivyo ni suala la muda tuu huyu kama anaona kuwa sisi sio raia na yeye ndiye basi ajue kuwa tutamshughulikia kwani hata SISIMIZI NI MDOGO ILA ANAWEZA KUMUUA TEMBO MNYAMA MKUBWA .sisi sisimizi its a matter of strategy......

Na kama kuna kiongozi wa serikali amejeribu kumpotosha kuwa hao yaani sisi ni wafa maji basi amekwisha huyu jamaa tutakula naye mpaka kieleweke.

Endeleeni kusambaza barua husika kila kona na mabunge ya Commonwealth kila uchwao, kuna wabunge wa nchi za kiafrika wataanza kuhoji nasi tusiwe nyuma hata kidogo.
 
Barua yetu tuwapelekee stake holders wake hadi wachanganyikiwe ili ashindwe kuwahadaa ,na inampasa ajue kuwa kwa sasa hapatakuwa salama kama uwekezaji wenyewe ndio huu wa kuitukanisha nchi na viongozi wake .

Hata kama Rais wetu ni mwenye uwezo mdogo hatutaruhusu hata siku moja kutukanwa na the so called mwekezaji.

Mr.President we are expecting what you did in the MAPANKI issue not less than that we will awaken the public on this matter.
 
[/FONT]

Jamani huyu jamaa anaonekana ni powerful kiasi kwamba anawanyang'anya uraia wa Tanzania Kuhani Mkuu,MKJJ na JF members

Na unajaua watu wengi hawajagundua kuwa hii ndio ingekuwa main concern yetu.

Kuuuchezea utaifa wetu!! Kuuchezea Utu wetu kwa vijisenti vyake.

Nidharaua kiasi gani?

Alafu ona...

... whose commentary reads like it comes from a standard playbook

Kweli tumedharauliwa kuliko mababu zetu wale wazamani..Tukaeni vema kuanza kupigania uhuru mara ya pili!

Lakini ninchaojifunza kwa huyu bwana...sioni anatatizo sana ..tutambwagachini..unajua vipi?

Basicaly nature yake haijatulia kabisa... anafaa kuviringisha.

NA

Tukimpeleka hivi....Inaonekana kabisa ata Loose control. Kitakachofuatia ataropoka, na sisi..tutanyoosha goti mpaka 120Km/hr.

Tutampleka. Huyu hata akiamabiwa jinsi tutakavyo m_Manage atatupuuzia kama viongozi mafisadi wanvyo puuzia ..kuja kushtuka wameshapoteza mchezo.

Wameshakuwa fully exposed to what they are...Sin C. hanatofauti. Hizo dharau na Nyodo zake zinatupa picha...Ni kwenda naye tu!
 
JK lazima ajisafishe kwenye hili la sivyo tutajua kuwa kumbe kamati zake zote ni feki na huwa ni mpaka aruhusiwe na wakina Sinclair ndipo anafanya maamuzi.

Tunasubiri tamko rasimi la serikali juu ya huyu mtu ASASP
 

Mbona anasema alivyochangia hasemi alivyochukua?
 

It will be wise as well kuituma kwa magazeti tofauti na stock exchanges za Toronto na USA, lazima kuna mtu au kikundi wataichukua na kuiweka kwenye media. Hawa walafi wanaokula bila kunawa mikono lazima tuwaanike.

Naona tuitume tena hii weekend akifika Jumatatu akute moto bado unawaka au kama anaingia huko nyumbani kusilalike.
 




MAJIBU YAKAJA HAYA:-





MUHIMU: Kwa wale mtakaotuma barua pepe kwenda kwa Jim tafadhali tuma nakala kwenda kwa madini@africaonline.co.tz
 
Enyi Wadanganyika nani aliye waroga?.Badala ya kulaumu matokeo kwa nini msiweke nguvu zenu kwenye chanzo?. Ina maana huyo sin-clear aliiba hiyo riport? na kama alipewa na rafiki yake sasa yeye ana kosa gani kuizungumzia pia kwa rafikize?.
Aliyempa hakujua kama ni siri? na kama angeona ni siri naamini angemwambia kuwa amempa ripoti lakini asiitoe hadharani na yeye angemsikiliza kwa vile ni maswahiba tangu mwaka 1994 alipopewa mgodi wa Bulyahulu badala ya Butobela kulingana na mkataba.
Kwa vile rahisi wenu alishawasoma wadanganyika kuwa hamnazo ni watu wa filimbi,wala hawamnyimi usingizi ndo maana hakuwa na wasiwasi wowote kumpa rafikiye/mwanahisa mwenzie taarifa hiyo muhim kwa biashara yao.
Maoni yangu badala ya kukimbilia kuandika 'petition' kwa sin-clear ni bora hiyo petisheni ielekezwe 'gulioni' kwamba sasa mpangaji aliye pale hafai ameendeleza kupafanya gulio kwa ajili ya wakwapuaji badala ya kurudisha jina la awali la 'ikulu'.Mfano halisi ni EPA,MEREMETA,TANGOLD na hili la sasa
Hiyo petisheni ianze sasa huyo chekacheka aondoke.Tutibu chanzo cha maradhi sio matokeo yake
 

Ndiyo ni lazima amejua maana kama tulivyokubaliana katika forum hapa tulimtumia ile barua na kama tulikuwa waaminifu kutuma barua nyiingi sisi wa jf basi lazima ujumbe ulikuwa message sent na lazima umkelekete na lazima atapetape. Hakuna suala la kwamba kuna mtu anampeleke taarifa lakini kwa ile barua tu tayari mambo yako shingoni.
Mimi ningeshauri iandikwe barua nyingine na atumiwe swahiba wake Kikwete.
Na kama tulivyoandika kwa sinclair tumtumie pia barua nyingi JK kumuonyesha hasira yetu kwamba aliapa kutotoa siri za nchi na sasa anazitoa ovyo kwa wazungu. Hii itakomesha tabia hii.
Jamani sisi tusijali kwamba hizi kelele za mlango eti hazitamzuia mwenye nyumba kulala bali tujue kwamba kadri kelele za mlango zitakavyoendelea kuongezeka ndivyo mwenye nyumba atakavyozidi kupata shida na kukosa usingizi.
Iandikwe barua moja na wana jf tushirikiane kwa wingi na kuituma kwa wingi kwa huyu mwenye nyumba ya tanzania na tuone kama atalala.
Natoa hoja.
 
Jana hili jambo liliingizwa bungeni rasmi ila naona media yetu haikulipa attention ya kutosha .

Nitaweka hapa hicho kipande kilichowasilishwa ndani ya bunge jana kwa ajili ya kumtaka aombe radhi.
 
Sehemu ya Hotuba ya Dr.Slaa jana ,je?huyu jamaa atajitokeza tena?
Ni vema basi, Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu akaliarifu Bunge lako Tukufu Kamati ya Bomani imetumia shillingi ngapi na Wakaguzi wa EPA wamelipwa kiasi gani. Hizi ni fedha za Wananchi ni lazima zitolewe taarifa kwa chombo chao ambacho ni Bunge.



Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani imetishwa zaidi na Taarifa iliyosambaa katika Mtandao inayoonyesha kuwa Taarifa hizo za Kamati ya Rais, ambayo ni Siri kubwa kwa Wabunge na kwa Watanzania tayari inajulikana na watu wa nje wakiwemo wawekezaji. Kambi ya Upinzani imefadhaishwa sana na Taarifa aliyotoa CEO wa Kampuni ya Tanzanian Royalty Exploration Corporation bwana James E. Sinclair Mwenyekiti na CEO, ya Tarehe 30 May, 2008 yenye kichwa cha habari "changes To Tanzanian Mining Law Certain to benefit Mineral Exploration" na pia ya tarehe 11 June, 2008 yenye kichwa cha Habari " A special note to Shareholders". Taarifa ya Bwana Sinclair ya 30 May, 2008 inatamka wazi kuwa " I have had the privilege of reviewing the Committees Recommendations-along with comments from the Chamber of Mines –and have no serious issues with them…What is important to know, however is that the man who will make the final decision on the recommendation is the President not the Committee…" na "As one might expect, any legislation involving such an important segment …has generated heated debate. In my opinion, a small percentage of this rhetoric is instigated by special interest groups in the west whose commentary reads like … a standard play book".
Mhe Spika, Kambi ya Upinzani inadhani haya ni madharau makubwa kwa Watanzania, matusi kwa Wabunge, na pia inajenga picha kuwa Wabunge wanaopiga "kelele" kuhusu mali na rasilimali zao sio watu wanaoweza kufikiri wenyewe bali "wanatumika" …… Matusi haya hayawezi kuvumilika hivyo basi, tunamtaka Bwana Sinclair aombe Radhi kwa Bunge hili na watanzania wote kwa ujumla. Mheshimiwa Spika, kiburi hiki amekipata baada ya Bunge lako Tukufu kudharauliwa kwa kunyimwa Taarifa muhimu kama hii. Hivyo Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali kuacha mara moja tabia ya kuthamini vyombo na watu wa nje.

Mheshimiwa Spika,
Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali iwasilishe mara moja Bungeni katika kipindi hiki cha Bunge Taarifa ya Kamati ya Bomani, pamoja na Taarifa zote za Kamati za awali ili wabunge waweze kutimiza majukumu yao ya ‘Kuisimamia' Serikali. Mhe. Spika, tumekwisha kusema mara nyingi, Wabunge ni watu wazima, waliokula kiapo, wanajua kutunza siri kwa vile na wao ni wazalendo, hivyo suala la Siri haliwezi kuwepo kwa Wabunge vinginevyo Kiapo wanachokula hakina maana yeyote.
 
Dr. Slaa ni mdesaji mzuri sana wa JF. Sijui kwa nini wengine nao hawafanyi hivyo au hawajui kuwa JF kuna speaking points?
 
john cheyo, yule mbunge wa bariadi yuko bungeni anazungumza sasa hivi, anashangaa ripoti ya tume ya madini ya jaji makani kuwa kwenye web site ya mtu anayejiita rafiki wa kikwete. anataka achukuliwe hatua kama yule mauritius aliyefukuzwa na nyerere baada ya kusema ameiweka serikali mfukoni.....
 
naomba kusahihisha ni ripoti ya jaji bomani na wal siyo jaji makani
 
teh teh teh, achukuliwe hatua na aliyempa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…