James Ole Milya anafaa kugombea ubunge Arusha mjini

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
2,956
Reaction score
1,115
Wakuu kuna tetesi kuwa James ole Milya anataka kugombea ubunge Arusha mjini mwaka ujao. Mimi naona anafaa zaidi ya mbunge wetu wa sasa Godbless Lema. Godbless Lema amefanya kazi kubwa kuimarisha chama chetu CHADEMA na amewaimarisha vijana na kuwafanya jasiri wa kujua na kudai haki zao. Ni vema sasa akapandishwa cheo na apewe nafasi iliyoachwa na John Mnyika ya Ukatibu Mwenezi na uhamasishaji ili apewe wigo mpana wa kuongeza wanachama na wapenzi nchi nzima. Kwa wasiomfahamu James ole Milya yeye ni mwanasheria, ni kijana wa Kimasai na anaweza kutuletea mawazo mapya ya maendeleo katika jiji letu hasa pale halmashauri ambapo mikataba ya hovyo na ya kifisadi inatengenezwa na hatuoni maendeleo.
Wakuu mwaonaje ?
 
Hakuna anayebisha kuwa Ole Milya hafai kuwa mbunge. lakini ingekuwa busara ukatueleza nini chanzo cha tetesi zako?
 
Lema hang'oki Arusha,Ole Millya anakwenda kumng'oa sendeka simanjaro.
 
ć

James ole Millya ni msomi mzuri. Ni mwanasheria. Ni kijana mwenye msimamo. Ni mpenda haki. Kuhusu kugombea jimbo la Arusha na kushinda hata kwenye kura ya maoni nafasi yake ni ndogo sana. Hawezi kushinda hata kidogo. Siasa za Arusha zina acrobatics nyingi sana.

Kuhusu jimbo la Simanjiro kumgoa ole Sendeka ni kazi kubwa sana. Pengine CCM wasimpitishe kwenye kura za maoni. Sendeka hata hii leo akisimama kama private candidate atashinda kwa kura nyingi sana.

Maeneo ambayo Sendekaa anaweza kupata upinzani mkali ndani ya jimbo la simanjiro niš mererani tu. Hata hivyo mererani haiwezi kuamua kura za simanjiro. Wakaazi wake wengi ni wahamiaji na sidhani wamejiandikisha kupiga kura.

James Millya pia tangu alipoamua kuanzisha vita na Sendeka reputation yake ilishuka sana. Alipoamua kuhama chama alidhihirisha kuwa siyo kiongozi mvumilivu kisiasa. Angepambana ndani ya mfumo aliyokuemo ingemkomaza kisiasa zaidi. Tusubiri time will tell.
 
Wakuu kuna tetesi kuwa James ole Milya anataka kugombea ubunge Arusha mjini mwaka ujao. Mimi naona anafaa zaidi ya mbunge wetu wa sasa Godbless Lema. Godbless Lema amefanya kazi kubwa kuimarisha chama chetu CHADEMA na amewaimarisha vijana na kuwafanya jasiri wa kujua na kudai haki zao. Ni vema sasa akapandishwa cheo na apewe nafasi iliyoachwa na John Mnyika ya Ukatibu Mwenezi na uhamasishaji ili apewe wigo mpana wa kuongeza wanachama na wapenzi nchi nzima. Kwa wasiomfahamu James ole Milya yeye ni mwanasheria, ni kijana wa Kimasai na anaweza kutuletea mawazo mapya ya maendeleo katika jiji letu hasa pale halmashauri ambapo mikataba ya hovyo na ya kifisadi inatengenezwa na hatuoni maendeleo.
Wakuu mwaonaje ?

Nimeipenda hiyo ya Lema kuwa KAtibu Mwenezi, azunguke nchi zima kukieneza chama na kuwapa vijana Ujasiri kama alivyowapa vijana wa Arusha
 
ć

James ole Millya ni msomi mzuri. Ni mwanasheria. Ni kijana mwenye msimamo. Ni mpenda haki. Kuhusu kugombea jimbo la Arusha na kushinda hata kwenye kura ya maoni nafasi yake ni ndogo sana. Hawezi kushinda hata kidogo. Siasa za Arusha zina acrobatics nyingi sana.

Kuhusu jimbo la Simanjiro kumgoa ole Sendeka ni kazi kubwa sana. Pengine CCM wasimpitishe kwenye kura za maoni. Sendeka hata hii leo akisimama kama private candidate atashinda kwa kura nyingi sana.

Maeneo ambayo Sendekaa anaweza kupata upinzani mkali ndani ya jimbo la simanjiro niš mererani tu. Hata hivyo mererani haiwezi kuamua kura za simanjiro. Wakaazi wake wengi ni wahamiaji na sidhani wamejiandikisha kupiga kura.

James Millya pia tangu alipoamua kuanzisha vita na Sendeka reputation yake ilishuka sana. Alipoamua kuhama chama alidhihirisha kuwa siyo kiongozi mvumilivu kisiasa. Angepambana ndani ya mfumo aliyokuemo ingemkomaza kisiasa zaidi. Tusubiri time will tell.

Siamini hiyo kazi kubwa iko wapi. Usianze kutishia watu washindwe kisaikolojia... au ndo wewe mwenye jimbo unajihami?
 
Habari iko kwenye gazeti la Mbiu ya Jamii toleo la tarehe 2 Oktoba - 8 Oktoba,2014. Ni gazeti jipya linachapishwa Haydom, mkoa wa Manyara. linauzwa sana Arusha na Manyara.
 
LEMA anaenda Jimbo la HAI litakaloachwa wazi na Mbowe anayeenda Moshi Mjini.

Arusha imeshamchoka huyu Kamanda.

Kweli kabisa.. Ni muda wa wana Arusha kuwa na mbunge mzawa.. Lema anafanya vurugu Arusha kwa sababu sio kwao..Aende akagombee ubunge kwao Moshi
 
ć

James ole Millya ni msomi mzuri. Ni mwanasheria. Ni kijana mwenye msimamo. Ni mpenda haki. Kuhusu kugombea jimbo la Arusha na kushinda hata kwenye kura ya maoni nafasi yake ni ndogo sana. Hawezi kushinda hata kidogo. Siasa za Arusha zina acrobatics nyingi sana.

Kuhusu jimbo la Simanjiro kumgoa ole Sendeka ni kazi kubwa sana. Pengine CCM wasimpitishe kwenye kura za maoni. Sendeka hata hii leo akisimama kama private candidate atashinda kwa kura nyingi sana.

Maeneo ambayo Sendekaa anaweza kupata upinzani mkali ndani ya jimbo la simanjiro niš mererani tu. Hata hivyo mererani haiwezi kuamua kura za simanjiro. Wakaazi wake wengi ni wahamiaji na sidhani wamejiandikisha kupiga kura.

James Millya pia tangu alipoamua kuanzisha vita na Sendeka reputation yake ilishuka sana. Alipoamua kuhama chama alidhihirisha kuwa siyo kiongozi mvumilivu kisiasa. Angepambana ndani ya mfumo aliyokuemo ingemkomaza kisiasa zaidi. Tusubiri time will tell.

Sendeka kule Simanjiro anapumulia mashine. Akisimama na Ole Milya atajamba cheche na sidhani kama ccm watakuwa wajinga kiasi hicho kumrudisha Ole Sendeka eti asimame na Ole Milya! Mpango uliopo ni kumsimamisha Mkuu Wa wilaya ya Kakonko nimemsahau jina lake, pia kuna yule mkurugenzi Wa shirika lenye ile radio ya ORS huwa anapigiwa chapuo na ccm achukue nafasi ya Ole Sendeka!
 
ole milya alikimbia na Pesa zetu Ccm. ni fisadi Sana. hata ubalozi hafai.chadema mmepokea oil chafu
 
Arusha imeishakumbwa na siasa chafu za ubaguzi, zilizoasisiwa na Ole Medeye, kuwa Wachagga Arusha wameifanya kama ndio kwao na haina wenyewe!. Japo raia yoyote Mtanzania, anao uhuru wa kugombea jimbo lolote, ila ni kabila moja tuu ndilo linaloongoza kwa kutoa wabunge wa kabila hilo kwenye mikoa ya wenzao!, wewe nenda kagombee huko kwao, kama hutasikia neno anani amchague "kyasaka!".

Sikumbuki mara ya Mwisho kwa jimbo la Arusha kushikwa na mtoto wa nyumbani ni lini?!. Tatizo la Arusha ni mji wa machalii, Lema ni chalii, sijui kama Milya ni chalii, ushindi wa Lema, ulifanikishwa na ma Don wa Kichagga wakiongozwa na Mrema wa Impala, Naura na Ngurdoto!, kufuatia zile vurugu za maadamano, don huyu alijuta!, akajiapiza Lema harudi 2015!, Arusha haiongei siasa, inaongea pesa tuu!. Chadema msimamisheni tena kipenzi cha wana Arusha na jimbo mlirudishe CCM kama mgombea wa CCM ataungwa mkono na ma don wa AR!.

Pasco.
 
Back
Top Bottom