James Mwakibinga amuomba radhi Dr Nchimbi juu ya uzushi aliomzushia wakuhujumu mali za CCM

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
2,609
2,000
Itakumbukwa mwaka jana kada wa CCM alitoa tuhuma dhidi ya Dr Emmannuel Nchimbi kwamba amejimilikisha floor moja kwenye jengo la umoja wa vijana sambamba na kujigawia viwanja 200 mali za CCM tuhuma ambazo amekiri kwamba hazikuwa za kweli.

Kutokana na tuhuma hizo Dr Nchimbi alifungua shauri mahakamani kwakuchafuliwa jina lake kesi ambayo shauri lake bado lilikua likiendelea kusikilizwa.

Kutokana na kada huyo kumuomba radhi Dr Nchimbi,wakili wa Emmannuel Nchimbi ameahidi kufanya mawasiliano na Dr Nchimbi ili waweze kuifuta kesi hiyo.

Chanzo Channel ten.
 

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
3,652
2,000
Huyo Mwakibinga ni kifaranga, mnamjua Mama mtu? Nchimbi ataachana tu na hiyo kesi maana kifaranga ametumwa tu yeye na Nchimbi analijua hilo maana yeye ni jasusi mzuri sana
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,180
2,000
Huyu Nchimbi ndio Ludacriss wa Bongo? Viwanja mia mbili sio mchezo eti....
 

Ngonidema

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
2,648
2,000
Nchimbi hanaga mambo ya kipuuzi, kwa jinsi nimjuavyo alisha msamehe, Na pia alisha Msamehe bure ndugu yetu [HASHTAG]#Lizabon[/HASHTAG]
 

othiambo

JF-Expert Member
Nov 15, 2014
1,603
2,000
Hao waarabu wapemba,mtu useme mwenyewe halafu ukubali kua sio hivyo ulivyosema kuna walakini... ndo pale Mpoto anaposema nauli imemshinda maana watu wenyewe hawaaminiki..
 

Mpira wa kona

JF-Expert Member
Nov 25, 2016
350
500
Mwakibinga mnajifanya mnajua majungu Na matusi oho Nchimbi kajimilikisha floor nzima utadhani wewe ndio ulimmilikisha Aibu umripata mwanaume mzima majungu
 

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
Who is Mwakibinga, nimeona picha zake twita ni kajamaa flani kachafu kachafu hiviiii,,,,,,nao waandishi wakiitwa na wajinger km huyu wanaenda msikiliza?
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,771
2,000
Kwani Mwakibinga ameshapewa ka cheo flani njaa iishe? Maana shida ni njaaa mweeeee!!! Nchii hiii Lumumba njaaa mweee
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,042
2,000
Michezo ya CCM kama ya wauza unga, wanakua na Urafiki Kwa terms maalum tu!!/
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom