GE2025 James Mbowe: Mbowe anatukanwa na Heche yupo kimya

GE2025 James Mbowe: Mbowe anatukanwa na Heche yupo kimya

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
James Mbowe ambaye ni mwanachama mwaminifu wa chama cha ukombozi wa umma (CHAUMMA) anasema moja ya kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza ndani ya CHADEMA ni Mheshimiwa Mbowe kutukanwa kwenye mitandao na viongozi ndani ya chama kuwa kimpya.

"Hakuna kitu kibaya kama viongozi kuruhusu muasisi wa chama kushambuliwa na kutukanwa kwenye mitandao. Freeman ametukanwa sana kwenye mitandao – anatukanwa kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi, na anatukanwa na vijana wa CHADEMA hawa Gen Z; watoto ambao wameingia kwenye hiki chama hata hawakijui kimetoka wapi wala kinaelekea wapi. Wamepewa tu Hadidu za Rejea, wao ni kushambulia, ni kutukana."

"Hebu nambie, mtu ambaye mnamtukana kuanzia asubuhi mpaka jioni, yeye amenyaamaza kimya – na anamtukana kwenye magroup ya chama ambako Makamu Mwenyekiti yuko, kwa maana ya John Heche, aliyekuwa Katibu Mkuu John Mnyika yupo, na baadhi ya viongozi waandamizi wa chama wapo. Freeman anatukanwa kule na vijana, lakini wenyewe wanakaa kule, wanasoma, wananyamaza kimya."
 
James Mbowe ambaye ni mwanachama mwaminifu wa chama cha ukombozi wa umma (CHAUMMA) anasema moja ya kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza ndani ya CHADEMA ni Mheshimiwa Mbowe kutukanwa kwenye mitandao na viongozi ndani ya chama kuwa kimpya
Hivi mpumbavu kuitwa mpumbavu ni tusi 🙄🙄🙄🙄 KWELI UANITHI WA AKILI NI UGONJWA MBAYA KULIKO YOTE
 
Lissu amewanyang'anya ulaji wao wa kijanja janja lazima waione Chadema ni mbaya. Kama Mbowe anatukanwa, yeye alitaka Heche afanyaje? Aache kutafuta vijisababu vya kuficha aibu ya kukimbia chama baada ya mirija ya ulaji kukatwa.
 
Ilibaki kidogo hii familia iuwe CDM
Nimwambie tu Mbowe

"You can fool some of the people all of the time, and all of the people some of the time, but you cannot fool all of the people all of the time."
 
Ponjoro mwingine huyu mirija imekatwa imekua nongwa, au pengine baba yake alikua ana muandaa kuja kushika kiti chake?
 
Jamani Heche kamtukana lini Mbowe?
Hajasema Heche kamtukana Mbowe mama yoyo.
Kasema vijana wanamtukana kwa magruop yao ya whtsapp ambamo Heche yumo na amekaa kimya hawakatazi vijana kumtukana Mbowe.
Kwa maana hiyo wanatafsiri Heche huenda anawasaport vijana wamtukane Mbowe ndo maana Hawakatazi.
 
Back
Top Bottom