mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 1,153
- 2,700
Nichukue nafasi hii kipekee kuwapongeza Air Tanzania kwa namna wanavyo badili ratiba za ndege mara kwa mara. Mfano leo ndege ya Air Tanzania iliyokuwa iruke kwenda Kigoma saa 5:40 imesogezwa mpaka saa 9:30 sababu wanasema ni Operation yaani siyo hata kwamba hali ya hewa ni mbaya au ndege mbovu bali ni sababu za Uendeshaji.
Yaani mnaacha Abiria wanatoka majumbani usiku wanawahi Airport alafu kwa Urahisi kabisa bila Aibu mnatangaza ni sababu za kiuendeshaji.
Kwa kweli kutoka Moyoni niwapongeze sana hii inaonyesha ni kwa jinsi gani Shirika letu linavyowajali wateja wake. Kuna mtu aliwahi kuniambia Kirefu cha ATC ni Anytime Cancelation, sasa nimeanza kumwelewa.