GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
James Mbatia: Haikuwa kazi rahisi tulipoamua kuanza kuandaa makongamano ya mabadiliko ya katiba tukiwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam mwishoni mwa miaka ya 1988 kuelekea 1989 na tuliita hayao mabadiliko kama National Construction and Constitutional Reform Tanganyika and Zanzibar.
James Mbatia: Tulikuwa watu 18 tulioanzisha hayo Mageuzi kabla hata serikali haijaunda Tume zake kuuliza watanzania wanataka mfumo gani chama kimoja au vyama vingi.
James Mbatia: Mabadiliko hayo yalisimamiwa na watu wawili kama viongozi wetu tuliowachagua Chief Fundikira na Mabere Nyaucho Nyarandu.
James Mbatia: Hali hii ikapelekea mimi James Mbatia kufukuzwa Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa mwisho wa masomo yangu.
James Mbatia: Tulianzisha vuguvugu la vyama vingi tukiamini nguvu ya vijana Vyuoni na mabadiliko ya siasa za vita baridi tungeweza kulazimisha serikali ikubali mfumo wa vyama vingi kutokana na msuguano uliokuwa unaendelea duniani juu ya ubepari na ujamaa.
James Mbatia: Enzi hizo chuo kikuu cha Dar es Salaam kilikuwa ni sehemu ya mawazo mbadala ambayo tulikaa Nkurumah Hall kuyajadili wanafunzi na walimu kama Prof Issa Shivji, Tenga na akina Dokta Sengondo Mvungi
Tuliamua kuanza kufanya choko choko hizo kabla hata serikali Haijafikia au kuwaza kuwa na mfumo wa vyama vingi
James Mbatia: Katika uasisi wa Mageuzi ya NCCR ( National construction and Constitutional reform) wakati huo nilipewa kadi namba 6.
James Mbatia: Baada ya Serikali kuunda Tume ya Francis Nyalali na kuridhia mfumo wa vyama vingi Tanzania miaka ya 1991, Sisi Tuliamua Kuongeza neno Mageuzi kwenye NCCR hivyo tukakisajili kama chama kamili mwaka 1992.
James Mbatia: Agustino Mrema tulimkaribisha NCCR -mageuzi mwaka 1995 mwezi march.
Hata baada ya kufukwa chuo nilienda kugombea ubunge kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na nikashinda nikawa mbunge wa kwanza kijana mdogo Bungeni mwaka 1995
James Mbatia: Mwaka 1992 nilifukuzwa chuo moja kwa moja na wanafunzi Wengine tisa hivyo sikumaliza shahada yangu ya Civil Engineering na nilibakiza miezi miwili tu tulionekana watukutu na vinara wa mabadiliko chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa kusababisha chuo kufungwa mwaka mzima