Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Mbunge wa Vunjo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, Jamse Mbatia, ametoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao kwenye ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv. Nyerere, kilichozama siku ya jana ambayo hadi sasa inaripotiwa kuwa zaidi ya watu 50, wamepoteza maisha.
Ajali iliyotokea jana, ile tunaweza kusema ni ajali ya kujitakia, na waliohusika wameua kwa kukusudia, kwa sababu hii dhana ya kutothamini uhai wa mwanadamu hapa nchini imezidi kukithiri - Jamse Mbatia Mbunge wa Vunjo ( NCCR Mageuzi).
Zaidi ya 96% ya majanga yanasababishwa na wanadamu na 4% ni nguvu asilia - Mbunge wa Vunjo, Jamse Mbatia.
Mbunge wa Ukerewe alilitahadharisha hili ndani ya Bunge, na alitoa mapendekezo lakini bado kivuko hakitoshelezi japo kilinunuliwa injini mpya, sasa nani alijali - Jamse Mbatia.
"Mbunge wa Vunjo James Mbatia ameitaja ajali ya jana ya MV. Nyerere kuwa ni janga la kujitakia, amesema kwa mujibu wa elimu aliyoipata ya namna ya kukabiliana na majanga kuwa hilo ni janga la kujitakia na waliohusika wameua kwa kukusudia" 1/2.
Katika ufafanuzi wake James Mbatia amebainisha kuwa asilimia 96 ya majanga yanayotokea yanasababishwa na binadamu na ni asilimia 4% huwa ni yale yanayosababishwa na nguvu asilia. 2/2.
"Ukirejea ajali ya MV. Bukoba miaka 20 liyopita ile Ilikuwa ni elimu tosha kwetu sisi ya kutufanya ajali hii isitokee." James Mbatia - Mbunge wa Vunjo
"Mbunge wa Ukerewe, Serikali ilimpa majibu na haikumpa majawabu sahihi na endapo ingempa majawabu sahihi hili lililotokea leo lisingetokea" - James Mbatia.
Hasara inayotokana na kuzama, kwa Mv. Nyerere huwezi kufananisha na kitu chochote, hata uuze Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huwezi kurudisha uhai wa watu - Jamse Mbatia, Mbunge wa Vunjo.
Cha kushangaza, eti wanasitisha zoezi la uokoaji kwa sababu ya giza, karne hii, haingii akilini, hapa tulipofikia mungu atusamehe - Jamse Mbatia.
NUKUU: Kujibu kabla ya kutafakari ni upumbavu na aibu kwako - Jamse Mbatia.
Habari zaidi, soma=>Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 125 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa! - JamiiForums